Thanks God for Giving us Kikwete

Thanks God for Giving us Kikwete

chezea JK wewe vijana mnalipwa kumsafisha mitandaoni enh..... na watz ni hasara yaan full kuyumbishwa kisa vijisent wakat ukweli mnao. hahaha heri yetu sie waangaliaji wa huu mchezo mchafu ngoja nasi tufanye yetu kwenye vitengo vyetu. nyie mnaotokwa mapovu umu for nothing hata posho hupatiii ur a total looser lkn kama bahasha ya kaki imepita kila la kheri zenuu.
kweli akili ni mali, hata wewe unapost ulimbukeni wako hapa? kweli ushamba shapu kazi sana. umezoewa kupakatwa na Babu Slaa unazani wote? wengine tupo kwa kutetea Taifa na si Watu binafsi.
 
Mwenyezi Mungu huwa ana makusudi kwa kila jambo linalokuja kwa wanadamu, zuri au baya! Imani yangu inanituma kuwa alimleta Kikwete ili Tanzania ipate ukombozi kamili toka kwa CCM (wakoloni weusi). Hizi ndo sababu zangu: -

1. Baadaya Kikwete kushindwa kura za maoni 1995 alianzisha mtandao wa kusaka urais tangia hapo. Mtandao ambao ndio chanzo cha makundi ya CCM na ambayo hayawezi kuisha ndani ya chama hicho. (Kikwete muasisi wa makundi)

2. Kikwete na mtandao wake walinunua wahariri wa vyombo vya habari ili kumpamba Kikwete na kuwachafua washindani wake. (Rejea kauli za Sumaye) Walipoingia madarakani na seriksli yao ikawa legelege wakawageuka waandishi wanaowakosoa na kufungia vyombo vyao. (Mwanahalisi, Kulikoni, Mwananchi, Mtanzania nk) Ccm ikatengeneza uadui na waandishi.

3. Kikwete katika uchaguzi uliopita baada ya kukabwa vilivyo na Dr Slaa, washauri wake na chama chake wakamshauri kuelekeza siasa misikitini kujaribu kuokoa jahazi. Yanayotokea baada ya hapo kila mmoja anaona. (Kikwete muasisi wa udini) Wenye macho wanaweza kuona CCM itakavyoangushwa na udini.

4. Kauli yake ya maisha bora iliwapa matumaini watanzania kuwa inawezekana wamepata mkombozi mpya. Matumaini yoa yanayeyuka kama barafu na sasa tafiti zinaonyesha watanzania hawana imani na serikali, Kikwete na CCM.

5. Amevuruga uhusiano wa kidiplomasia na nchi zinazotuzunguka (Rejea kutengwa kwa Tanzania EAC na mgogoro wa Malawi)

Yote haya yakiweza kufanyiwa kazi na upinzani sioni CCM ikiokoka. Ni mpango wa Mungu Kikwete kusababisha ukombozi?

hakuna kama Kikwete tangu tupate uhuru....chuki zenu hizo hazina dawa ila kuumia ndani kwa ndani
lakini JK amefanya mengi sana kuliko marais wote walomtangulia....
na amefanya mapinduzi makubwa katika nyannja zote za uchumi
yapo wazi....tena mazuri yakukumbukwa na vizazi vijavyo..
  • katiba mpya ya watanzania...hili hakuna rais yoyote aliyekua tayari kubadilisha
  • muungano...JK amekubali na kuna uwezekano mkubwa muungano ukarekebishwa kuondoa dosari
  • miundo mbinu ..amefanikiwa kufikisha na kuinganisha TZ kwa Lami..kuna maeneo hayakuwahi kupata lami tangu uhuru..mfano kigoma na Zitti hilo amelithibitisha
  • amewezesha maeneo kama kigoma na njombe nk kupata umeme wa uhakika
  • amekubali kuwalazimisha wenye migodi ambayo mkapa aliwapa chee kulipa zaidi
  • amewezesha wananchi wenyewe kujadili sera ya madini na mafuta..hili hapo nyuma hakuna rais aliekubali
  • alizirejesha kampuni za Reli kwa serikali baada ya mkapa kuiuza kwa rites ya india..hii ni kutokana kuwa msikivu
  • migodi ya mawe pia ameirejesha mikononi mwa serikali
  • alio ndolea mbali kampuni ya mkapa ya net solution ilio kuwa ikiendesha Tanesco...hii pia ni hatua muhimu kuweka maslahi ya nchi mbele
  • alizuia jaribio la mwisho la kuuzwa kwa NIC NATIONAL INSURANCE CORP.....kulikua na mipango kuliuza kwa bei ya poa wakati wa mkapa..kama alivo uza NBC,
  • Mgogoro wa zanzibar ulimshinda nyerere......wakati akiwa hai watu walikua wakiuliwa kule kwenye uchaguzi wa 1995 na nyerere hakukemea ...mgogoro uliendelea mpaka uchaguzi ulopita, watu wali pelekwa wakimbizi , wengi walikuwa raped wengine vilema.....lakini JK Kwa kujali maslahi ya nchi yake aliwaweka Wazenji na kuwapatanisha ...aliridhia hatua zote ambazo karume alikua anachukua...hili pekee ni jambo kubwa sana kwa wenye kujua.
  • usalama wa raia umeimarika
  • kilimo chetu kimekuwa zaidi sasa....wakulima sasa wanauza mazao yao na kupata faida..kilimo kwanza ni mpango madhubuti alio ubuni
  • umeme sasa umeimarika zaidi ..na serikali yake imekua ikijitahid sana
  • shule nyingi zaidi zimejengwa za serikali...kuliko kipindi chochote
  • amejenga chuo kikuu cha dodoma.....ni kikubwa na kina uwezo mkubwa..na lengo lake ni kuwa chuo kikubwa zaidi east and cetral afrika.....hili ni jambo kubwa sana
  • ajira nyingi zimepatikana kutokana na kuongezeka kwa miradi mingi ya nje na ndani...
  • uhusiano wetu na mataifa makubwa umeimarika sana kuliko kipindi chochote
  • madaktari wengi zaidi wanatarajia kuhitimi baada ya muhimbili kupanuliwa na majengo mapya ya chuo hicho yana jengwa nje ya dar
  • mradi mkubwa wa kupanua bara bara za dar es salaam kuondoa foleni na kulifanya jiji la kisasa
  • mradi mkubwa wa daraja la kigamboni...ni mafanikio makubwa.....walio mtangulia wengi walikua wakitia na kutoa
  • mradi wa mji mpya wa kisasa kule kigamboni ni moja katika mambo ya kusifia upeo wake na kuipenda nchi yake
  • ni kiongozi msikivu...na wapinzani wanafahamu kuwa amekua akiwasikiliza sana kwenye mambo ambayo yana maslahi na nchi
  • mradi wa vitambulisho vya taifa pia ni jambo moja kubwa ambalo amelifanya....limechelewa sana lilikuwa lifanywe mara baada ya uhuru....hili amelifanya...
  • kuhusu nchi za afrika ya mashariki amekua akiangalia maslahi ya nchi kwanza...mambo ya mashiriakiano na muungano hayahitaji haraka..na yanataka kwenda kwa uangalifu...nadhani sisi tuna muungano wa tz nz znz hivyo tuna uzoefu kutokana na matatizo yanayo patikana kama mungano unakua wa haraka haraka ..hivo anajali maslahi ya nchi yake...na ndio muhimu
  • serikali imewezesha kupatikana mkonge wa taifa kurahisisha mawasiliano ya internt
  • miradi mikubwa ya gas inayo endelea kule mtwara ni mambo ya maslahi na taifa
  • kulifufua shirika la reli ambalo limekufa...na ikifika mwakani reli litakuwa na vichwa karibu 15 vipya na litabadilisha kabisa hali ya usafiri
  • tanzania chini ya JK imekuwa ndio iko mbele kupokea fedha za uwekezaji kutoka nje
  • mradi mkubwa wa bandari mpya ya bagamoyo ni moja katika mambo ambayo yatafanyiaka.....huu ni mradi mkubwa kabisa kuweza kufanyika....utabadilisha kabisa hali ya upakuaji mizigo
hivyo jk kaifanyia nchi hii mambo mengi makubwa.....kuna makosa ya hapa na pale..lakini aloyafanya ni mazuri na walomchagua hawakukusea...
ya nyerere kutomchagua sijui lakini huyo alomweka yeye yaani mkapa hakuna hata moja alofanya katika nchi hii zaidi ya kuuza mabenki, dawasco tanesco,makaa ya mawe, sioni jambo ambalo nitasema hili kafanya mkapa
tusifie penye haki..
 
Kuwaletea MAENDELEO watanzania


Wewe ni kijana wa bongo fleva au? Maendeleo? Mkuu husomi taarifa ama habari? Kwani hukusikia taarifa ya UN ya hivi karibuni kuwa watanzania wengi wamekata tamaa na hawana furaha? Sasa maendeleo gani aliyoleta huyu msanii ambayo wewe unayaona? Pita pita mtaani utasikia watu wanaongea nini juu ya Kikwete kwani siyo siri tena, huyu jamaa ni bomu na hafai hata kidogo.
 
Wewe ni kijana wa bongo fleva au? Maendeleo? Mkuu husomi taarifa ama habari? Kwani hukusikia taarifa ya UN ya hivi karibuni kuwa watanzania wengi wamekata tamaa na hawana furaha? Sasa maendeleo gani aliyoleta huyu msanii ambayo wewe unayaona? Pita pita mtaani utasikia watu wanaongea nini juu ya Kikwete kwani siyo siri tena, huyu jamaa ni bomu na hafai hata kidogo.

Maendeleo yapo
Na maisha bora yapo
Tatizo unafikiri yatakuja bila kufanya kazi
Fanya kazi utapata nyumba na sasa nhc wanakopesha nyumba za kisasa
Utapata gari yamejaa tele
Chakula kipo cha kutosha mpaka cha nje
Shule zipo nyingi
Club za kwenda jioni zipo nyingi
Katafute kazi ufanye utapata kila kitu
Kikwete ameshakuwekea huduma zote
Dubai ipo hapa hapa bongo
Wacheni uvivu
Wanakuja ma tx wakimaliza muda wao wanaomba uraia kwa raha na nafasi za kutafuta pesa
Otherwise msubiri slaa 2090
 
Mungu hana kusudi lolote ni kitu feki kama vitu vingine sokoni, machine error.
 
Mungu alitaka watanzania wapitie mateso kama Ayubu, na wana wa Israel kabla ya kupata ukombozi wa kweli 2015.

Watanzania Tuzidi Kuwa wavumilivu kwani Nchi ya Ahadi sasa tunaikalibia T 2015 CDM.

Mimi siyo mwana CCM, wala sina chama, ila kama unadhani Chadema chaweza kumkomboa mtu, unahitaji tiba.
 
Mungu ameumba na kuleta wabaya nyakati za ubaya.Huenda ameletwa kuangamiza taifa hili baada ya maovu kuzidi ila kamwe naye JK hatapona!
 
Kwa hiyo mnataka kuunga mkono wale waliosema eti Kikwete ni chaguo la Mungu???? Sidhani na sitaki kumhusisha Mungu na hilo!!
 
Mwenyezi Mungu huwa ana makusudi kwa kila jambo linalokuja kwa wanadamu, zuri au baya! Imani yangu inanituma kuwa alimleta Kikwete ili Tanzania ipate ukombozi kamili toka kwa CCM (wakoloni weusi). Hizi ndo sababu zangu: -

1. Baadaya Kikwete kushindwa kura za maoni 1995 alianzisha mtandao wa kusaka urais tangia hapo. Mtandao ambao ndio chanzo cha makundi ya CCM na ambayo hayawezi kuisha ndani ya chama hicho. (Kikwete muasisi wa makundi)

2. Kikwete na mtandao wake walinunua wahariri wa vyombo vya habari ili kumpamba Kikwete na kuwachafua washindani wake. (Rejea kauli za Sumaye) Walipoingia madarakani na seriksli yao ikawa legelege wakawageuka waandishi wanaowakosoa na kufungia vyombo vyao. (Mwanahalisi, Kulikoni, Mwananchi, Mtanzania nk) Ccm ikatengeneza uadui na waandishi.

3. Kikwete katika uchaguzi uliopita baada ya kukabwa vilivyo na Dr Slaa, washauri wake na chama chake wakamshauri kuelekeza siasa misikitini kujaribu kuokoa jahazi. Yanayotokea baada ya hapo kila mmoja anaona. (Kikwete muasisi wa udini) Wenye macho wanaweza kuona CCM itakavyoangushwa na udini.

4. Kauli yake ya maisha bora iliwapa matumaini watanzania kuwa inawezekana wamepata mkombozi mpya. Matumaini yoa yanayeyuka kama barafu na sasa tafiti zinaonyesha watanzania hawana imani na serikali, Kikwete na CCM.

5. Amevuruga uhusiano wa kidiplomasia na nchi zinazotuzunguka (Rejea kutengwa kwa Tanzania EAC na mgogoro wa Malawi)

Yote haya yakiweza kufanyiwa kazi na upinzani sioni CCM ikiokoka. Ni mpango wa Mungu Kikwete kusababisha ukombozi?

kweli uongo kazi,2015 kikwete alishindwa kura za maoni?
 
Mkuu, yaani umeonesha udhaifu mkubwa saba katika kufikiri. Kwani JK alishindwa kwenye kura za maoni mwaka 2005? kama ndo hivyo, je alishindaje nafasi hiyo ndani ya chama?

Hoja ni ya msingi hapo inaeleweka ni 1995 kakosea kidogo tatizo nini kisichoeleweka hapo mkuu
 
kwa hiyo mnataka kuunga mkono wale waliosema eti kikwete ni chaguo la mungu???? Sidhani na sitaki kumhusisha mungu na hilo!!

tunawaunga mkono tena sana ! Mwanzoni ilikuwa ngumu kuwaelewa , na kuanzia sasa namsamehe rasmi askofu kilaini , ubarikiwe baba !
 
Kikwete pia ndo aliyetufundisha kua ukiiba unatakiwa urudishe tu basi...
 
Katika hiki Kitab Alf Layla wa Layla, napenda kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Subhana Wataala kwa kutupa Jakaya Mirisho Kikwete kuwa Raisi wetu.

Through Jesus Christ our Lord, Amen, Amen, Amen
Through Muhamed our Lord, Amen, Amen Amen
By the Grace of Allmighty Lord, Amen, Amen, Amen

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Tubariki watoto wa Tanzania.

Where is Rev. Kishoka, is he still alive?
 
Through Jesus Christ our Lord, Amen, Amen, Amen
Through Muhamed our Lord, Amen, Amen Amen
By the Grace of Allmighty Lord, Amen, Amen, Amen

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Tubariki watoto wa Tanzania.

Rev Kishoka,

Napenda nikupongeze kwa maono yako ambayo pasi na shaka yoyote kwako umeona yapo sahihi kutuwekea hapa.
K
Kubwa nililotaka nikujuze naona labda ilikupuruchuka ni kuwa Mohammad S A W is not a Lord BUT HE IS A MESSANGER OF God(ALLAH)


Pole sana

 
Katika hiki Kitab Alf Layla wa Layla, napenda kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Subhana Wataala kwa kutupa Jakaya Mirisho Kikwete kuwa Raisi wetu.

We need to thank God for so much blessings to have Kikwete as man in charge.

Yes I have been critical of his leadership, I have mocked him, I have challenged him for his in-activeness and forgot that it was blessings in disguise from our Lord God!

Mungu ni wa ajabu sana, na nafikiri ni mapenzi yake tumepewa Kikwete awe kiongozi wetu. Ni mapenzi ya Mungu leo hii tupo hapa tukipiga kelele na baragumu tukitumia vinubi, zumari na tarumbeta kufukuta hasira zetu, vilio vyetu, aibu yetu na umoja wetu.

Si kwa mapenzi yake Jakaya Kikwete, bali ni mapenzi ya Mungu, kuwa yanayotokea sasa hivi, yalipangwa mapema na Mola.

Nasi tumkubali Jakaya Mrisho Kikwete kwa mapungufu yake yote, ukimya, uzembe, uvivu, uzubaaji, kutokuchangamka, kutokuwajibika na dhana kuwa analinda wale wahujumu. Mapungufu yake, ndiyo ngao na silaha yetu tuliyopewa na Mungu dhidi ya wale wenye kutaka kutufanyia dhuluma na kutuumiza.

Kuporomoka kwa Mawaziri wakubwa na mashuhuri wanne si mapenzi yake Kikwete, maana alitoa machozi. Lakini ni mapenzi ya Mungu leo hii nchi nzima si vilio kuhusu ufisadi tuu, bali mazungumzo ya kutaka uwajibikaji, mazungumzo ya kuimarisha ufanisi, na kulitakia Taifa letu maisha mema na Baraka za Mungu ndiyo yaliyotawala.

Tunataka mshikamano, tunataka uongozi madhubuti, tunataka tufaidi matunda ya utajiri wetu wa asili, uhuru wetu na matunda ya jasho letu bila kunyonywa, kudhulumiwa, kuonewa au kudhihakiwa.

Haya yote yasingetokea kama Kikwete wetu, mtalii, Vasco Da Gama, Sinbad, Chekacheka, Kisura asingekuwa madarakani.

Najiuliza je tungekuwa na mwamko mkubwa namna hii wa kutetea haki zetu kama tungekuwa chini ya Nyerere? Labda ungekuwako, lakini tungekuwa na woga.

Najiuliza je tungekuwa na ukali namna hii wakati wa Mwinyi, yawezekana, lakini bado tungekuwa na woga.

Najiuliza tena tungekuwa na uwezo wa kuchambua mambo muhimu kwa Taifa letu, kuishupalia Serikali, kutafuta ushahidi na hata kuimbua Serikali yetu wakati wa Mkapa? tungeweza, lakini angetupuuza na angetumia ujeuri na dharau zake kutokutusikiliza.

Sidhani kama Kikwete ni msikilizaji mzuri, ila ni baraka za Mungu kuwa kujivuta vuta kwake ambao wengine wamekuita Uyakhe yakhe, Ukwerekwere na Usaigon, ndio umetusaidia sana.

Yeye mwenyewe sijui kama analijua hili, lakini tafadhali sana wewe uliye mwakilishi wa Mheshimiwa Kikwete unayepita kuchungulia JF wamesema nini, mnapoamka Ijumaa hii na kujiandaa na Gwaride la Muungano, mwambie Mheshimiwa Raisi, tunamshukuru Mungu kwa kuwa yeye ni Raisi wetu.

Mapambano yetu bado hayajaisha. Tuendelee kutumia kudra, rehema na baraka hizi za Mwenyezi Mungu, kuendeleza Libeneke la kutaka uwajibikaji, ufanisi, umahiri kupiga vita Uhujumu, Uzembe, Dhuluma, Umasikini, Ujinga na Maradhi.

Kila jamii ina njia yake ambayo Mungu kawatengenezea. Njia yetu ya Ukombozi ni wakati huu wa ndugu yetu Muungwana akiwa Raisi!

Tutumie fursa hii kupigana na wale mahasidi wasiotutakia mema, tuendeleze shinikizo letu kwa viongozi wetu wawe watii wa sheria, walinzi wa katiba, wafuata haki na wanaothamini utu.

Through Jesus Christ our Lord, Amen, Amen, Amen
Through Muhamed our Lord, Amen, Amen Amen
By the Grace of Allmighty Lord, Amen, Amen, Amen

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Tubariki watoto wa Tanzania.

Rev Kishoka,

Kuna mengi sana umeandika na kwa kuwa kwa busara zako na cheo chako umeandika ukiwa na mantiki nzuri ILA BILA SHAKA ULISAHAU NENO ZAMA. KWANI SOTE TUNAAMINI KILA MTU NA ZAMA ZAKE.


Kwa bakhati kubwa KIKWETE ndio ameangukia katika zama hizi za uwazi na ukweli kwa uhuru mkubwa na mpana sana na technology za kisasa zaidi ikiwa na uhuru wa kujieleza na hata kuandika na ndio maana mnaweza kumchambua na kusema lolote bila mushkira.
E
nzi za Nyerere kulikuwa hakuna kitu kama hicho. Alichotamka yeye basi watu ni kufuata tu na ndio maana hata sera zakeza ILI WA TZ waendelee walihitaji vitu vinne akitaja watu, ardhwi, siasa safi na uongozi bora hazikuweza kumsaidi katika kuinua uchumi wa Tz japo kila kitu kilikuwepo hapa Tz.

lakin vile vile Azimio la Arusha, Siasa ni kilimo, Vijiji vya ujamaa nk vyote vilipita bila mafanikio na hilo ni kwa sababu wasomi wote walizibwa midomo kuchambua sera hizo za Nyerere lakin kwa kikwete kuna uhuru mpana wa watu kujadili ikiwa pamoja na hata kumdhihaki na kumtusi kiongozi wenu.

Mwinyi alifungua soka huria kwa wote wenyewe uwezo waweze kuogelea.

Mkapa kauza na kubinafsisha viwanda vyote ili kuleta ufanisi na kuinua uchumi wa nchi yenu.

Kikwete ameweka miundombinu mizuri tu ya kukuza uchumi wenu kwani ameimarisha barabara, viwanja vya ndege, reli na kustabilize Umeme kwa kuunga gas kutoka mtwara na kuimarisha bandari na vile vile kuzijengea uwezo taasisi binafsi za wazawa nazo kuanza kuchunguia na kuona fursa mbali mbali za kuinua uchumi wenu.

NDIO maana tunasema kila mtu na zama zake. Kwa kila kiongozi amejitahidi sana kwa kuleta maendeleo kwa upande mmoja na amefeli kwa upande mwingine huo ndio ubin'Adam hakuna mkamilifu.

Ni msingi mkuu kwenu sasa KUCHAGUA VIONGOZI SAHIHI NA SIO VIONGOZI BORA ILI WAFANYE MAAMUZI SAHIHI kwa mustakabali wa kukuza uchumi wenu.

Shukran


 
Back
Top Bottom