Thanks God for Giving us Kikwete

Reverand you did thank this person for this quote.

But i didn't understand it for he quoted me while refering at you and other stuff that i cant understand!

Nitashukuru!
 
Reverand you did thank this person for this quote.

But i didn't understand it for he quoted me while refering at you and other stuff that i cant understand!

Nitashukuru!

Nimetoa shukrani kwa kuchangia mada, pamoja na kuwa vidole vyake vinaonekana vinapingana na mawazo yake!
 
Nimetoa shukrani kwa kuchangia mada, pamoja na kuwa vidole vyake vinaonekana vinapingana na mawazo yake!
Mimi huwa natoa shukrani kwa kukubaliana na point.
Is asante ok regardless of the ambiguity?
Thanks anyways Rev.
 
Mimi huwa natoa shukrani kwa kukubaliana na point.
Is asante ok regardless of the ambiguity?
Thanks anyways Rev.

So goes your definition of Shukrani. If someone has different views wouldn't you acknowledge him/her and say thank you for your views?

Mimi hutoa shukrani hata pale ambapo sikubaliani.

Kwa kuwa nilianzisha mada hii, kwa mtu yeyote kuchukua fursa kusoma na kuchangia, nampa shukrani kwa kitendo hicho. Si lazima tuwe na msimamo mmoja wa mawazo au utata wa majibu.
 
Tatizo sio msimamo ila ni kwamba sijaielewa kabisa ile posting kwasababu kama umeiona ameni quote!

Sasa utasemaje asante kwa kitu kisichoeleweka?

Si ndio maana nikaomba unieleweshe baada ya kuona umetoa asante?

Naomba unieleweshe maana ya posting yake since aliniquote na mimi sikuelewa jibu!
After all that then nitaweza na mimi kumpa shukrani!

Once again Shukran!
 
Mushi,

IO anakuita wewe Profesa na anaongelea kuhusu hypocricy na kuonyesha kuwa kuumina na kutaabikia kwa wananchi, hakuendani na theory zangu kuwa kuwepo kwa Kikwete ndio njia bora ya kuondokana na taabu na mihangaiko.
 
Rev, Kishoka,

Tatizo la Imani yangu pale anaposimama Mungu ni kwamba uchaguzi wa rais MATAKWA yetu, hivyo Mungu hujalia kile tulichokiomba.

kwa hiyo hii habari ya mtaka yote kukosa yote ni matokeo ya mwanadamu ktk tamaa zake hazihusiani na mapendekezo ya Mungu.

hapo ndipo kidogo nilikwama kwa sababu hapa tunaingiza maswala ya imani ya dini na pengine tofauti zilizopo kati ya imani yangu na yako ndiyo yananipa shida kuelewa hata hivyo, nakubaliana na mchango wako kwa kiasi kikubwa kwamba makosa tuliyoyafanya ya kumchagua JK imekuwa rehma kwetu kupata nafasi ya kuyatupia macho maswala ya UFISADI kwani hakuna akti yetu anayeweza kupiga ramri la Uongozi wa Freeman chini ya Chadema...

Yet, pamoja na yote haya ni lazima tukubali tulifanya makosa sisi wenyewe pengine leo hii chini ya Chadema ama CUF tunmgekuwa ktk hatua nyingine kabisa..Mkapa angekuwa akichekea kizimbani, nyumba za serikali zimerudishwa, swala la EPA, Richmond, Buzwagi wala Balali yasingekuwa kweli.
 
Ukweli ni kwamba hatujui ingekuwaje kama tungemchagua Freeman. Huenda sasa tungekuwa pazuri, au huenda nchi ingekuwa imevurugika kiasi cha kutawaliwa na maafande.

Tunachojua ni hiki: JK ameanzisha kampeni ya kutokomeza angalau baadhi ya mafisadi. Kwa sasa amemgeukia Karimagi. Mkataba wa kiwizi wa nyongeza ya muda aliowekeana na mafisadi serikalini unavunjwa.

Asidhani mtu hapa kwamba hawa Wabunge wanathubutu kuwavaa Mkapa na wakuu wengine bila ruhusa ya JK.

Pamoja na kumshukuru JK kwa kazi hii, tunamwomba awafukuze CCM hawa mafisadi.

Mikataba ya Madini huenda itamshinda JK kwani wezi wa nje walihakikisha kunakuweko kipengele cha kusema kwamba kisheria, ni London pekee ndiko wanaweza kuzungumzia mikataba yao. Kilichobak ni JK kuwaambia hawa wezi kwamba wasipokubali mabadiliko yatakayoleta HAKI, basi serikali haitawapa ushirikiano. Wanahitaji huo ushirikiano wa serikali ili kulinda mirija yao.
 
Tafadhali be specific kwenye highlighted!
 
Huoni amewatoa mkuku Lowasa, Msabaha, Karimagi, Chenge na Balali? Au ulitaka awaue?

Tunasubiri washtakiwe baadaye, na wafukuzwe CCM
 
Naomba nilinukuu Mwanahalisi na hasa kwenye huo msisitizo. Ukifuatilia pia na mada ya Mwanakijiji ya Illusion of Power, utabaini kuwa Shukrani hii haikuwa na makosa.

 
...kiasi cha kufanya watu waliozoea kufanya mambo watakavyo kuwa na wakati mgumu...

Heeh..So President anawapa watu wakati mgumu....! Na hawa ni wale ambao hawana nia njema ya kuijenga nchi..!!

AND..?

In that case then..He is doing very well!!
 
Jamani mumemuelwewa vibaya,sio kama anamsifie Kikwete,someni upya mutafahamu nini anamaanisha.
Ni tungo tata mno inayohitaji uyakinifu kuipembua,hicho ni kiswhili cha mafumbo.
Mungu wabariki wazaramo.

Ni kweli kabisa,tafadhali muwe na upeo wa kuchanganua mambo,hapo hajasifiwa"positively" bali ni "negatively".Sidhani kama kusifiwa uzembe,kulea ufisadi ni sifa nzuri.
 

LIMBANI, tatizo la JK si kusikia vilio vya watanzania. Naamini JK ni msikilizaji mzuri na anataarifa kamili za vilio vyetu. Tatizo lake kubwa ni kutochukua hatua kwa wakati muafaka! Hii ni kasoro kubwa kwa uongozi kwa kuwa kuchelewesha mno uamuzi kunaweza kuligharimu pakubwa Taifa. Mifano ni mingi: Kumchelewesha DG wa PCCB mfumbia macho Ufisadi, kumpuuza DG wa TIC na kauli zake za kikabila na uongozi wa enzi za mawe, Kuwavumilia Mawaziri wabovu n.k. Yote haya yanagharama. Na si utetezi unaokubalika kila wakati kwa JK kusema eti kwamba anaogopa kumuonea mtu. Yeye Malaika?
 
Shangilieni sana uongozi wa Kikwete, maana 2010 kunaweza kutokea ambayo hayajawahi kutokea.

Get the popcorn, pepsi and smell the coffee!
 
Rev.Kishoka,

..my reading ni kwamba huyo ni Kikwete akitafuta huruma za wapiga kura.

..wakati wa Mkapa kila kashfa[biashara,mashamba,majumba ya kifahari..] alikuwa akisukumiziwa sumaye. kila mtu mwenye ufahamu anajua hizo zilikuwa ni harakati za kikwete na wanamtandao.

..ninachojiuliza mimi ni lini Kikwete ataacha kampeni na kuanza kazi? tumefika mahali nchi inaendeshwa kwa kampeni.

..badala ya mawaziri kutekeleza bajeti, wanasafiri mikoani "kuwaelimisha" wanachi kuhusu kampeni!!
 
Itakuwa kazi kubwa sana kumwangusha Kikwete iwe ndani ya CCM ama nje labda tu Kikwete mwenyewe awe ktk kundi la hao wanaojipanga kumvua Urais. Nikiwa na maana ni mmoja kati ya hao MAFISADI ambao kwa hila zao wanajaribu kuendeleza Utawala wa mkoloni mweusi..

Trust me, Kikwete hawezi kushindwa na mtu yeyote kwa kura ikiwa hawa jamaa watajitenga kwa sababu haya machache aliyoyafanya tayari ni kinga yake kubwa sana ktk uchaguzi ujao hasa akiwa against hao Mafisadi...Jamani hawa jamaa wamechoka ile mbaya kisiasa, hata wengine hali zao sasa hivi inabidi tuwaombee Mungu!.. fedha wanayo lakini macho ya watu ni laana tosha!

Ni kundi moja tu ambalo linaweza kumwangusha Kikwete nalo ni UMOJA wa WAPINZANI kama wataungamna na kuacha kabisa mpango wa wagombea binafsi badala yake wasimamishe wabunge waliofanya vizuri mwaka 2005 hasa wale walioshika nafasi ya pili ktk majimbo. Yote hii inategemea nguvu ya UMOJA wa Wapinzani lakini kama watabakia kuwa hivi walivyo leo basi CCM wanaweza kuchukua tena kwa sababu madai yao yatakuwa wameisha safisha jungu Mafisadi wote wako nje na hawagombei nafasi yoyote!..Kama sahani huwezi kutokula chakula kwa sababu sahani hiyo aliitumia Fisadi.. imesafishwa na hivi sasa safi kabisa!..

Jokakuu,
Tanzania hakuna viongozi kwani kampeni ndio ushindi wa kila kitu kwa kila hawa watawala wetu. Bila kushinda kura huwezi kuwa waziri hivyo shina la Uwaziri ni kampeni ya ushindi na ndio maana kila kiongozi anayo kamati yake ya Ufundi. hakuna kiongozi hata mmoja anayefikiria nini atawafanyia Watanzania kwani kulingana na mfumo huuu tuliochukua viongozi wetu wanafikiria kuwa sasa hivi nchi inajiongoza yenyewe wao wanatawala tu kuhakikisha ufalme wa CCM unawafikia wananchi, yaani kujichana tu na hiyo Free Market Economy ambayo kwetu sisi ina maana moja tu - KILA MTU NA MZIGO WAKE!.
 
Mzee Walioba Alisha Sema Viongozi Wetu Ni Dhaifu,hizo Ni Sifa Za Udhaifu Wa Muungwana Na Mganga Wake Wa Kienyeji Kingunge,hivi Huyu Mzee Wa Nini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…