Thanks God for Giving us Kikwete

Thanks God for Giving us Kikwete

Mwalimu Augustine,

Mimi nimempa Mungu tukuzo. Nimempa shukrani, soma magazeti ya tangu mwaka huu uanze, mpaka leo, soma mijadala ya watu kama sisi JF na wengine, ni ishara wazi kuwa mapenzi ya Mungu kulipa Taifa letu neema yanatimilika, ila si kwa utashi wetu au kwa umahiri wa kiongozi wetu.

Yanayotokea ni dhahiri kuwa hata kama kwa nafsi zetu tunamuona JK hafai na ni batili, lakini ni JK huyohuyo ambaye katupa nafasi (kwa kudhamiria au hata bila kudhamiria) kuyazungumza yale ambayo yalikuwa hayazungumziki.

Mchungaji!

Ni Negative Progress!

Pia mimi nitoe shukrani zangu kwa Muumba Mungu Baba!

Kama umepoteza kipande kimoja cha almasi ndani ya vichaka 100; Kila unapokikosa kwenye kichaka kimoja kati ya hivyo mia, huo ni ushindi maana unahakika hapo kwenye hicho kimoja haipo. Umeikosa lakini umeshinda maana katika kuitafuta hapo hutarudia tena. Ni maedeleo mema kwenye safari ndefu ya utafutaji wako.

Hata unapoikosa kwenye kichaka cha 98, bado hayo ni maendeleo na shukrani kwa Mungu, kwani kwa hivyo vichaka unahakika haipo, na hata kama kuna wafadhili wanataka kukusaidia....hawatagharamikia kupitia vichaka 98, Hayo ni Maendeleo ya kusifiwa!

Wengi wanaweza wasione kuwa haya tunayoogelea hapa ni maendeleo ya kishindo lakini ndio ukweli.

Unapokuwa na werevu wa kutosha unawea kuwaona Viogozi wengi wa sasa Katika taifa letu watakavyotupa ushindi wa Bure sisi watanzania tuliosahauliwa! Tumshukuru Mungu kwa werevu wetu na UUPUUZI NA USINGIZI WALIOLALA MAFISADI.

Mimi ninafuraha,na pia nimtanguliza Mungu kwani Huyu Mtu wao atakaopokwenda kueleza kuwa tumewaita nilivyowaita hawa Mafisadi, wao Watachekelea na kusema wanajua wanachokifanya. Na waanchokifanya ni kuwa wao wameamka na hawajala! Huo ni Ushindi!
Wao watachekelea kabisa na kusema JF na vyobo vya habari hamna lolote..wataendelea kukwida vileo na vilevi kwa burudani zao..wakisema hamana kitu hayo yatapita...Huu ni ushindi tena wa kumshukuru Mungu! Ukweli ni kuwa SIKUZAO ZINAHESABIKA!

Mafisadi watakuwa hawana AKILI NA FIKRA SAFI kuona kuwa NGUVU YA UMMA WA TANZANIA IKO JUU SASA KULIKO WAKATI MWINGINE kudai UTU BORA na UTANZANIA STAHILI!

Hawataona!

Nani hapa JF alitaka waone?

Nani hapa JF alataka wachukulie haya matamshi kama ni serious?

Tumshukuru Mungu Kwa Upofu wao!

Naam tumshukuru Raisi wetu Kipenzi JMKIKWETE kwa kuwepo kwake!

Nani Alitaka tusimshukuru Mugu kwa hilo???
 
Sina uhakika kama wengi tumepata vizuri maana ya asemayo Rev. Kishoka. Anasema kwamba sasa inanonekana wale viongozi wa dini waliosema JK ni chaguo la Mungu hawakukusea. They spoke prophetically.

Nani alidhani JK angekuwa ndiye Rais atakayewatoa mkuku wale viongozi waliodhani kwamba mbinu zao za wizi wa mali ya uma ni kikomo?

JK ameanza na wale waliodhani kwamba wakati akitoka Mkapa, ni lazima aidha wachote mamilioni mengi sana wayafiche nje (eg Chenge, Mahalu, Balali, Mkono), au waweke mirija ya kinyonyaji sana watakayoitumia miaka itakayofuatia (eg Mkapa, Yona, Pesambili, Karimagi, Kingunge).

JK awakumbuke pia wale waliochota wakati akiondoka Mwalimu. Alishasema Mwinyi kwamba alikuta Hazina kweupe! Ilibidi akakope kwa Mugabe ili kukomboa mzigo wa mafuta uliokuwa bandarini! Mungu atamrudishia Mugabe wema wake!


Ziko habari kwamba walioandamana na Mwalimu wakati akizunguka Canada na Marekani kuaga,walibadilisha malundo ya travelers cheques kuwa cash (dola). Ripoti zinasema kwenye benki moja pekee, walibadilisha travelers cheques kiasi cha $90,000. Mjue walirudi na hayo madola Dar na kuyauza kwa njia za ulanguzi!

Nadhani JK alipokutana na Mrema waliteta kuhusu dhahabu aliyokuwa amekamata uwanja wa ndege. JK atawafikia wote hao. Dawa yao iko jikoi. Chaguo la Mungu hajawasahau, hatawasahau. Mungu mwenyewe atamkumbusha.

JK aanze kuchunguza tangu kuanzia kwa akina Amir Jamal, na amalizie na washirika wake wa karibu (eg Rostam Aziz).

Mambo bado kabisa! Bado tuko kwenye rasharasha, mvua zenyewe bado sana!
 
Sina uhakika kama wengi tumepata vizuri maana ya asemayo Rev. Kishoka. Anasema kwamba sasa inanonekana wale viongozi wa dini waliosema JK ni chaguo la Mungu hawakukusea. They spoke prophetically.

Mkuu Moshi,

Heshima mbele, Mchungaji hapa anamaanisha kuwa kuwepo kwa serikali ya sasa, ni zawadi kutoka kwa Mungu ambayo wananchi tukiitumia vizuri au ipasavyo, basi tutaweza kubadilisha mambo mengi muhimu kwa maendeleo ya taifa letu, na hasa tukiweza kukazania mabadiliko ya katiba, kwa sababu serikali ya sasa ni so weak kwamba haina hata muelekeo, lakini bado inaheshimu sana uhuru wa speech!

I hope nimempata mchungaji sawa sawa!
 
Field Marshal ES,

Heshima mbele Mkuu! Kwa nini unasema serikali ya JK ni weak? Serikali weak haingeweza kuwatetemesha vigogo kama inavyofanyika sasa. JK hana challenge yoyote. Hana challenge kwenye CCM, hana challenge toka upinzani. Jeshi, Polisi na Usalama Wa Taifa wako naye. Spika wa Bunge anamsikiliza JK. Jaji Mkuu anamsikiliza JK. Hao ndiyo nguvu yake. Mfumo wetu wa serikali hauwezi kuruhusu serikali kuyumbishwa na watu waliojiuzulu kutokana na shutuma za rushwa.

Unadhani hao fisadi koko wana kambi ya kweza kumtingisha mtu ambaye angeweza kuwa Rais hata kabla ya Mkapa?
 
Sina uhakika kama wengi tumepata vizuri maana ya asemayo Rev. Kishoka. Anasema kwamba sasa inanonekana wale viongozi wa dini waliosema JK ni chaguo la Mungu hawakukusea. They spoke prophetically.

Nani alidhani JK angekuwa ndiye Rais atakayewatoa mkuku wale viongozi waliodhani kwamba mbinu zao za wizi wa mali ya uma ni kikomo?

Augustine!

Nafikiri umenifanya nikafikiria mara ya pili and in that case ku_polish mtizamo wangu kidogo!

Honestly speaking Taifa under Kikwete linapitia kwenye mabadiliko ya msingi if you realy care to watch closely! Kufikiri he isnt doing His job properly sio sahihi sana....Nafikiri hata viongozi wa dini they will go along very well with this observation! Walimuoba Mungu yeye kama chaguo na ukiangalia vitu vya msingi tena vya kinabii vinatimia!

I can feel something big coming for the good of our nation! And this is God given gift as our President is following his intuition and insipiration from the good Lord. Amen!
 
Kama ingekuwa hiyo ni kazi ya mungu nafikiri priority yake mungu ilikuwa kuwashushia wale wa-Dafur, Zimbabwe au Iraq kwanza.
There are some issues which are very scientific here, sasa hata hapa mahali mie nilikuwa napaamini mnaanza kuleta metaphysics na supersition.

Sababu kubwa ya muungwana kuanza kuact sasa hivi ni nyingi, wabongo wamechoka na anything can happen anytime; na huyu jamaa anataka kuendelea na miaka mitano mingine. Dr Slaa factor plays a very big roll in these changes, aliumbua vitu ambazo mtu wa kawaida alikuwa hajui. Kashfa ziko nyingi mno, another big factor ni information technology -internet. Zama za mwinyi au nyerere habari zilikuwa hazitembei. Another was Zito factor!

The only issue maybe from the beginning, Muungwana ameaacha free speech ishamiri hajawasweka ndani watu kama mkapa! Ben was a dictator. You cannot cheat people all the time!!
 
Huyu anajuta na kumlilia Mungu kwa nini watu tumemchagua JK.

Mungu katupatia akili, tunazijaribu
 
Kama ingekuwa hiyo ni kazi ya mungu nafikiri priority yake mungu ilikuwa kuwashushia wale wa-Dafur, Zimbabwe au Iraq kwanza.
There are some issues which are very scientific here, sasa hata hapa mahali mie nilikuwa napaamini mnaanza kuleta metaphysics na supersition.

Sababu kubwa ya muungwana kuanza kuact sasa hivi ni nyingi, wabongo wamechoka na anything can happen anytime; na huyu jamaa anataka kuendelea na miaka mitano mingine. Dr Slaa factor plays a very big roll in these changes, aliumbua vitu ambazo mtu wa kawaida alikuwa hajui. Kashfa ziko nyingi mno, another big factor ni information technology -internet. Zama za mwinyi au nyerere habari zilikuwa hazitembei. Another was Zito factor!

The only issue maybe from the beginning, Muungwana ameaacha free speech ishamiri hajawasweka ndani watu kama mkapa! Ben was a dictator. You cannot cheat people all the time!!
And thanks God for Slaa, Thanks God for Zitto, thanks God for everybody who live and breath in Tanzania Uwepo wao wote ni katika mpango wa Mungu. JINA LA BWANA LIHIMIDIWE KWA KUWA YOTE MAZURI AMEYAFANYA YEYE, NA MABAYA NI YA SHETANI, NA MUNGU SIKU ZOTE AMEENDELEA KUWA MSHINDI, I SAY THIS THROUGH CHRIST OUR LORD, AMEN.
 
Bado nakumbuka alichosema Kikwete baada ya list ya mafisadi kutajwa. ...... nimetunza hayo maneno na yanasaidia kuwaangalia mara mbili mbili wanaosema kuwa Kikwete anapambana kusafisha nchi toka kwenye ufisadi.

The same Kikwete ndiye ameshikilia report ya EPA, the same Kikwete ndiye amekataa kutaja majina ya wanaodaiwa kuiba bank kuu. The same Kikwete ndiye amefanya nothing kwenye ile kashfa nyingine ya Meremeta na wenzake. The same kikwete ndiye amekaa kimya wakati Tanzania ikiendelea kumlipa rafiki yake mamilioni ya dola kila mwezi.

The same kikwete ndiye ametuletea buzwagi na ......... kama MUNGU anashukuriwa kwa Kikwete, basi kuna sababu ya kufuatilia tena uelewa wangu kwa huyu MUNGU.
 
We are too cheap to believe that Muungwana is God given to us! It reminds me that we have easy minds! Please kishoka refrain and retrieve your words; this forum becomes too cheap! You are the best contributor to this forum; but this is a mess!
 
Interested Observer Na Mwafrika wa Kike,

Wanasiasa wanauma na kupuliza. Mara nyingine inabidi wafanye hivyo. La sivyo wanaanguka.

Ni vijana wa JK ndiyo waliowapa Slaa na Zitto data. Baadhi ya data walizipata kwa CAG (baada ya baraka ya JK) na nyingine wakafanya utafiti kwa msaada wa vijana wa JK. Kwa upande mmoja, JK aliwatumia.

Kusema sababu ya huu uwazi wa sasa ni kuweko internet si sahihi. Hiki kifaa kilikuweko hata kabla ya JK. Tulikuwa na bcstimes.com, na ilikuwa imepamba moto kweli kweli. Lakini mahasimu kwenye serikali wakaifungia mbali.

Juzi juzi walijaribu watu kuangamiza JF. Naamini JK ndiye aliwakanya akina Mwema waache uhuni wao.

JK si malaika. Mungu anachagua hata wale wasio perfect wakati mwingine. JK ana makosa mengi, hasa kwenye Uchumi. Mimi nilipiga kelele kumpinga mara tu moshi mweupe ulipoonekana kule Dodoma.

JK alisema tumpe muda kabla ya kumhukumu. Tumefanya hivyo. Sasa tumegundua kumbe alikuwa na program ya kuwashukia wezi wakuu wa mali za uma.

Tunasema ni imani yetu kwamba kuna mkono wa Mungu hapa. Ama huu ukombozi unadhani unatoka wapi?

Imani sio ushirikina. Imani ni kipaji toka kwa Mungu. Kama hunacho basi omba tu, atakusikia, na kukujalia. Ni umasikini ulioje kikosa kabisa Imani?
 
We are too cheap to believe that Muungwana is God given to us! It reminds me that we have easy minds! Please kishoka refrain and retrieve your words; this forum becomes too cheap! You are the best contributor to this forum; but this is a mess!
NO I THINK U DONT GET WHAT REV WAS TRYING TO SAY, JUS READ BETWEEN THE LINES, MIE NISHAMUELEWA, AMETUMIA LUGHA YA KITABU SANA KAMA MTU SI WA KITABU INAKUWA VIGUMU KUMPATA LAKINI HIVYO HIVYO KIDOGO KIDOGO TUNAENDELEA KUELEWESHANA.
 
Hii serikali imewekwa na M/mungu makusudi ili kuwasaidi watanzania kurekebisha na kuziba panapovuja ili maisha ya watanzania yaweze kuwa bora, ndo maana tunaweza kupata data tunazolingia leo na kuwanyanyasa mafisadi, ndo maana tunapata majukwaa ya kuongelea kama hapa JF. Mungu mkubwa.
 
But Hapana, On The 2nd Thought, You People Dont Try To Make Kikwete Look Like An Angel Sent Down By Almighty Kupambana Na Mafisadi, Plz Read Careful And Understand What Rev Was Try To Emphasize.
 
But Hapana, On The 2nd Thought, You People Dont Try To Make Kikwete Look Like An Angel Sent Down By Almighty Kupambana Na Mafisadi, Plz Read Careful And Understand What Rev Was Try To Emphasize.

Sijui hapa hakieleweki nini, looks obvious though!

JK wasn't sent to eliminate FISADI'S!.... he was sent to be used as a tool to reveal fisadis!! Him siting where he is, he doesn't even know how these things happen.... they happen too fast for him. Thats why he is just busy with so many things outside the country and every time he tries to settle down he finds a resignation letter on his table....duh!!!

Thanks to God otherwise Chunusi wangetumaliza..... we didn't know they were there!!!!! Fungeni mikanda ....kumbe??!😡
 
Naomba nijinukuu mwenyewe na angalieni mkazo ulipo kwa wale ambao bado mnaona utata wa hoja hii.

Katika hiki Kitab Alf Layla wa Layla, napenda kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Subhana Wataala kwa kutupa Jakaya Mirisho Kikwete kuwa Raisi wetu.

We need to thank God for so much blessings to have Kikwete as man in charge.

Yes I have been critical of his leadership, I have mocked him, I have challenged him for his in-activeness and forgot that it was blessings in disguise from our Lord God!

Mungu ni wa ajabu sana, na nafikiri ni mapenzi yake tumepewa Kikwete awe kiongozi wetu. Ni mapenzi ya Mungu leo hii tupo hapa tukipiga kelele na baragumu tukitumia vinubi, zumari na tarumbeta kufukuta hasira zetu, vilio vyetu, aibu yetu na umoja wetu.

Si kwa mapenzi yake Jakaya Kikwete, bali ni mapenzi ya Mungu, kuwa yanayotokea sasa hivi, yalipangwa mapema na Mola.

Nasi tumkubali Jakaya Mrisho Kikwete kwa mapungufu yake yote, ukimya, uzembe, uvivu, uzubaaji, kutokuchangamka, kutokuwajibika na dhana kuwa analinda wale wahujumu. Mapungufu yake, ndiyo ngao na silaha yetu tuliyopewa na Mungu dhidi ya wale wenye kutaka kutufanyia dhuluma na kutuumiza.

Kuporomoka kwa Mawaziri wakubwa na mashuhuri wanne si mapenzi yake Kikwete, maana alitoa machozi. Lakini ni mapenzi ya Mungu leo hii nchi nzima si vilio kuhusu ufisadi tuu, bali mazungumzo ya kutaka uwajibikaji, mazungumzo ya kuimarisha ufanisi, na kulitakia Taifa letu maisha mema na Baraka za Mungu ndiyo yaliyotawala.

Tunataka mshikamano, tunataka uongozi madhubuti, tunataka tufaidi matunda ya utajiri wetu wa asili, uhuru wetu na matunda ya jasho letu bila kunyonywa, kudhulumiwa, kuonewa au kudhihakiwa.

Haya yote yasingetokea kama Kikwete wetu, mtalii, Vasco Da Gama, Sinbad, Chekacheka, Kisura asingekuwa madarakani.

Najiuliza je tungekuwa na mwamko mkubwa namna hii wa kutetea haki zetu kama tungekuwa chini ya Nyerere? Labda ungekuwako, lakini tungekuwa na woga.

Najiuliza je tungekuwa na ukali namna hii wakati wa Mwinyi, yawezekana, lakini bado tungekuwa na woga.

Najiuliza tena tungekuwa na uwezo wa kuchambua mambo muhimu kwa Taifa letu, kuishupalia Serikali, kutafuta ushahidi na hata kuimbua Serikali yetu wakati wa Mkapa? tungeweza, lakini angetupuuza na angetumia ujeuri na dharau zake kutokutusikiliza.

Sidhani kama Kikwete ni msikilizaji mzuri, ila ni baraka za Mungu kuwa kujivuta vuta kwake ambao wengine wamekuita Uyakhe yakhe, Ukwerekwere na Usaigon, ndio umetusaidia sana.

Yeye mwenyewe sijui kama analijua hili, lakini tafadhali sana wewe uliye mwakilishi wa Mheshimiwa Kikwete unayepita kuchungulia JF wamesema nini, mnapoamka Ijumaa hii na kujiandaa na Gwaride la Muungano, mwambie Mheshimiwa Raisi, tunamshukuru Mungu kwa kuwa yeye ni Raisi wetu.

Mapambano yetu bado hayajaisha. Tuendelee kutumia kudra, rehema na baraka hizi za Mwenyezi Mungu, kuendeleza Libeneke la kutaka uwajibikaji, ufanisi, umahiri kupiga vita Uhujumu, Uzembe, Dhuluma, Umasikini, Ujinga na Maradhi.

Kila jamii ina njia yake ambayo Mungu kawatengenezea. Njia yetu ya Ukombozi ni wakati huu wa ndugu yetu Muungwana akiwa Raisi!

Tutumie fursa hii kupigana na wale mahasidi wasiotutakia mema, tuendeleze shinikizo letu kwa viongozi wetu wawe watii wa sheria, walinzi wa katiba, wafuata haki na wanaothamini utu.

Through Jesus Christ our Lord, Amen, Amen, Amen
Through Muhamed our Lord, Amen, Amen Amen
By the Grace of Allmighty Lord, Amen, Amen, Amen

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Tubariki watoto wa Tanzania.
 
Sijui hapa hakieleweki nini, looks obvious though!

JK wasn't sent to eliminate FISADI'S!.... he was sent to be used as a tool to reveal fisadis!! Him siting where he is, he doesn't even know how these things happen.... they happen too fast for him. Thats why he is just busy with so many things outside the country and every time he tries to settle down he finds a resignation letter on his table....duh!!!

Thanks to God otherwise Chunusi wangetumaliza..... we didn't know they were there!!!!! Fungeni mikanda ....kumbe??!😡



Message nzito hii .JK nadhani wampeleke asome aelewe mawazo yako .Mungu asante kwa kutupatia JK ? Well sina comments zozote hapa .
 
Tusianze kupeana maelezo ya kubabaishana, maana ni very open! Maybe our understanding is different, but in the bottomline: A chronicle of issues:

1. The three ministers including the PM left their positions after Mr. Mwakyembe Richmond report. That was obvious!
2. Chenge - a scandal, which is open,
3. Ballali - a sacrifice
Kikwete alitetea Richmond, alitetea Bank Kuu, na hakuna any public statement kuhusu hayo yote. Kaficha EPA report. He is mumb on the Tangold and other stolen money through meremeta! A major culprit, who used that money to win the presidency! No I cannot budge; he has to come out clean.

In politics people play games, the game of survival; JK is just telling these guys who are dropping; hey guys step aside I will protect you from behind but not within. That is why in this CCM era, we will never see Lowasa, Chenge, Karamagi, and all with scandals prosecuted; only because these scandals engulf all CCM survival; without these culprits CCM will never exist and JK would never be a president!

Please do not blassphem; JK was born like you was raised like and he played his cards well to become a president! These chances are equally given by the almighty; we should spin our brains, and not put god in our reasoning weaknesses!
 
Interested Observer

Do you think what has happened today would have happened during Nyerere, Mwinyi or Mkapa' time? That people will be bold enough to talk and raise their voices unopposed by the government regardless of the degree of allegations of ufisadi, uhujumu or kukosa kuwajibika?
 
Last edited by a moderator:
Simply nothing could happen, a big reason is, how information spread, and mostly important is how evidence is backing such allegations. Ile report ya silaha ilikuwa ni revelation ya madudu yaliyokuwa yakifanywa tangu enzi hizo.

Lakini most of the time kulikuwa hakuna evidence. Hata kama kukiwa na weak evidence ilikuwa inapotea tu kwa sababu ya strong propaganda, na jua kuwa wakati ule majority ya sisi wabongo tulikuwa tunategemea information from Dailynews/Uhuru au RTD; hizo news zote zilikuwa authorised news; no free media.

Unajua watu wakichoka utawajua, nyerere aliondoka kwa kuwa kila mtu alichoka, na yeye alijua watu walimchoka, mwinyi made grave mistakes but at that time we had a very controlled media. Mkapa alishaanza kulemewa, na yote hayo kamwachia JK. JK knows very well everybody in this country is tired; and is just a time bomb. You can't slave people of all generations.

This president should do more, to clean himself, and i wonder why there is a feeling in this discussion that a president should be praised if he does his duties?
 
Back
Top Bottom