Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,362
- 1,133
Mwalimu Augustine,
Mimi nimempa Mungu tukuzo. Nimempa shukrani, soma magazeti ya tangu mwaka huu uanze, mpaka leo, soma mijadala ya watu kama sisi JF na wengine, ni ishara wazi kuwa mapenzi ya Mungu kulipa Taifa letu neema yanatimilika, ila si kwa utashi wetu au kwa umahiri wa kiongozi wetu.
Yanayotokea ni dhahiri kuwa hata kama kwa nafsi zetu tunamuona JK hafai na ni batili, lakini ni JK huyohuyo ambaye katupa nafasi (kwa kudhamiria au hata bila kudhamiria) kuyazungumza yale ambayo yalikuwa hayazungumziki.
Mchungaji!
Ni Negative Progress!
Pia mimi nitoe shukrani zangu kwa Muumba Mungu Baba!
Kama umepoteza kipande kimoja cha almasi ndani ya vichaka 100; Kila unapokikosa kwenye kichaka kimoja kati ya hivyo mia, huo ni ushindi maana unahakika hapo kwenye hicho kimoja haipo. Umeikosa lakini umeshinda maana katika kuitafuta hapo hutarudia tena. Ni maedeleo mema kwenye safari ndefu ya utafutaji wako.
Hata unapoikosa kwenye kichaka cha 98, bado hayo ni maendeleo na shukrani kwa Mungu, kwani kwa hivyo vichaka unahakika haipo, na hata kama kuna wafadhili wanataka kukusaidia....hawatagharamikia kupitia vichaka 98, Hayo ni Maendeleo ya kusifiwa!
Wengi wanaweza wasione kuwa haya tunayoogelea hapa ni maendeleo ya kishindo lakini ndio ukweli.
Unapokuwa na werevu wa kutosha unawea kuwaona Viogozi wengi wa sasa Katika taifa letu watakavyotupa ushindi wa Bure sisi watanzania tuliosahauliwa! Tumshukuru Mungu kwa werevu wetu na UUPUUZI NA USINGIZI WALIOLALA MAFISADI.
Mimi ninafuraha,na pia nimtanguliza Mungu kwani Huyu Mtu wao atakaopokwenda kueleza kuwa tumewaita nilivyowaita hawa Mafisadi, wao Watachekelea na kusema wanajua wanachokifanya. Na waanchokifanya ni kuwa wao wameamka na hawajala! Huo ni Ushindi!
Wao watachekelea kabisa na kusema JF na vyobo vya habari hamna lolote..wataendelea kukwida vileo na vilevi kwa burudani zao..wakisema hamana kitu hayo yatapita...Huu ni ushindi tena wa kumshukuru Mungu! Ukweli ni kuwa SIKUZAO ZINAHESABIKA!
Mafisadi watakuwa hawana AKILI NA FIKRA SAFI kuona kuwa NGUVU YA UMMA WA TANZANIA IKO JUU SASA KULIKO WAKATI MWINGINE kudai UTU BORA na UTANZANIA STAHILI!
Hawataona!
Nani hapa JF alitaka waone?
Nani hapa JF alataka wachukulie haya matamshi kama ni serious?
Tumshukuru Mungu Kwa Upofu wao!
Naam tumshukuru Raisi wetu Kipenzi JMKIKWETE kwa kuwepo kwake!
Nani Alitaka tusimshukuru Mugu kwa hilo???