Kwa nini tusiendelee kushukuru? Maana hata katika udhaifu wake kama mtendaji na kiongozi, mengi yanafunuka hata kuhusu sisi kama Taifa na wananchi! Tujiulize kwa nini tulimpa dhamana tena 2010? Je tulikuwa tumelewa au ni upofu uliokomaa?
Yote haya yanayotokea, ni lazima yatokee na ni kutokana na namna ya uongozi wake, tunaweza kujipima kama Taifa na jamii kuona kama tuko kwenye mstari sahihi au tuanze upya.
Ni Fasihi dada yangu na ukweli ni kuwa jamii ni lazima ijitazame hata kutumia fasihi na kujitambua ala, kumbe nasi twachangia na si Kikwete pekee.
Nilipoandika Screw Muungwana, ilikuwa miezi michache baada ya yeye kuchaguliwa, na hata kabla hajaapishwa niliandika mada nyingine "Hercules..." nayo ikionyesha wazi maoni yangu kuhusu uwezo wake wa kufanya kazi na kuwa kiongozi.
Sasa ukirudi kuvisoma, utafikiri ulikuwa ni unajimu!
So bado namshukuru, maana si Kikwete pekee, bali hata wengine twaanza kuwatambua na tunaanza kujitambua kama jamii!