Hongera saana Sizinga,kumbuka kuwa kazi ni tamu na yenye kupewa thaman kabla mtu hajaipata lkn ukisa ipata na kuanza kupata mshahara basi inakuwa ni mitihani mikubwa,zingatia wajibu wako,ipende,shirikiana na wenzako,tumia elimu yako na ujuzi ulionao kuellimisha wengne,saidia jamii kwa kipato chako,saidia ndugu na watu wasiojiweza....
Zaidi ya hapo nakupa hongera zaidi, usitusahau humu sisi ambao bado hatujapata kazi,share na sisi vyote vinavyopaswa share nasi,ilinde kazi yako kwakuwa ndio itakuwa inakupa mkate wako wa kila siku,fanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi,kwakuwa umeingia ktk moja kwa moja kama mlipa kodi na mjenga Taifa hili changa,onyesha ufanisi na ubunifu,Sizinga daima usijihusishe na mambo mabaya amabayo yanaweza iharibu kazi yako kama rushwa,ulevi(tofauti na unywaji pombe),anasa ,kutojenga maelewano na ofisi yako.....na mengne mengi tuu!
Sizinga kila la kheri ktk kazi yako mpya,imenipa hamasa na mwongozo kuwa kila jambo linawezekana na kwa muda husika!
Nikutakie maisha mema kwakuwa now ndio unaanza maisha,maisha bila mkate wa kila siku sio maisha!!!!!