Thanx God....17 yrs...Still getting stronger

Thanx God....17 yrs...Still getting stronger

Fukuzia mwanawane ikiwezekana hama hata mtaa msichana ataanza kukumiss kama kweli umemuingia moyoni, kuna wakati mwingine huw a tunajidanganya kwamba hatuwapendi watu kumbe deep inside kabisa mahaba yamejaa tele

huwezi ukajua wakati mwingine bahati ya mwenzio pia yaweza kuwa ya kwako........it is implausible but you never know how the Almighty God works in people....................................aendelee kukaza buti mpaka kieleweke..............Let his gentleness be be known to all for the Lord is at hand...................
 
Kwa kweli nimefurahi umenipa moyo , na Mungu najua ndiye aliyenifikisha hapa nilipo, pia nina shuhuda nyingi tu za kushuhudia, ahsante sana

Ubarikiwe sana.................
 
Daaa umenifanya nifurahi sana, umenipa maneno matamu sana nashukuru sana rafiki yangu

Hahahaha kwa kweli mautundu niliyaanza mdogo sana, loooo ila hayakuniadhiri yamelipa eeee au sio, cha muhimu namshukuru mpenzi mume wangu kwa kugundua udogo wangu na kuwa mkali wakati mwingine ili niwe kwenye mstari, raha nyingine ya kuolewa mdogo ni muda wote unaonekana wewe ni mtoto tu mpaka wakati mwingine unakuwa mkali ili akuchukulie kama mtu mzima, aaaich kwa kweli raha sana
Usijali Gaga unastahili yote haya, pongezi ni haki yako kabisa
 
Hongereni sana sana,
mungu azidi kuibariki ndoa yenu pamoja na familia yenu kwa ujumla.
 
Daaa umenifanya nifurahi sana, umenipa maneno matamu sana nashukuru sana rafiki yangu

Hahahaha kwa kweli mautundu niliyaanza mdogo sana, loooo ila hayakuniadhiri yamelipa eeee au sio, cha muhimu namshukuru mpenzi mume wangu kwa kugundua udogo wangu na kuwa mkali wakati mwingine ili niwe kwenye mstari, raha nyingine ya kuolewa mdogo ni muda wote unaonekana wewe ni mtoto tu mpaka wakati mwingine unakuwa mkali ili akuchukulie kama mtu mzima, aaaich kwa kweli raha sana
Hahahahaaaaaaa, kwa kweli utundu wako ulilipa, ila inaonekana ulianzamambo ukiwa mdogo sana, jamaa huyo ni hatari sana
 
Hi marafiki, wanajamii wenzangu, siwezi amini miaka inavokatika, nikiangalia naona kama ni juzijuzi tu, sijui wakati umeenda wapi, all in all namshukuru Mwenyezi Mungu sana sana kwani leo ni anniversary yetu na my hubby, namshukuru Mume wangu pia kwa kunichagua mimi kuwa mke wake, nawashukuru pia watoto wangu kwa kunipa sababu nyingine ya kuishi, nawapenda sana hawa watu walio katika maisha yangu. Our anniversary is a time to look back at the good times and to look ahead to live our dream...below is my story..

Nikirudi nyuma kabisa nakumbuka nikiwa msichana mdogo na kabegi kangu ka shule nakutana na huyu mkaka aliyehamia mtaani kwetu, na kupanga chumba nyumba ya jirani baada ya kumaliza masomo ya chuo, utani uleeee wa kizamani ukaanza, oooh mchumba, oooh hakuna shule hapo, oooh sijui nini badae nikaja kugundua huyu jamaa ananizimia, mwisho wa siku akaniambia ukweli wake, niliogopa sana...ukizingatia alikuwa mkubwa kuliko mimi.

Moyoni nilikuwa na mawazo sana hasa wasichana wengi wanajua kipindi ambapo wanafanya maamuzi ya kuwa na BF wa kwanza kabisa, nikammwaga,nilihisi bado wakati na siwezi kuwa na uhusiano na mkaka mkubwa,miezi ikaendelea, mara tunakutana dukani, mara kwenye chips mtaani.....miezi inaendelea...hatimae mwaka....jamaa kawa stable kidogo kazini anataka kuhamia chumba kingine eneo lingine kabisa, hapo ndio kimbembe kilianza

Jioni moja kaniita kanambia anahama keshapata chumba mahala pengine, na alipohama ndipo nilianza ku mmiss mpaka nikaumwa kabisa, kumbuka kipindi cha miaka ya tisini na hivi simu ilikuwa ni ishu, mawasiliano ni mpaka umtafute mtu, na wakunitafuta ni yeye coz mie alipohama nilijifanya sitaki kujua anahamia wapi,muda ukapita ila jamaa hakukata tamaa, akarudi siku moja mtaani nilipomwona mpaka machozi yalinitoka....... hapa ndio ule msemo wa "huwezi jua thamani ya kitu mpaka ukipoteze ndipo ulifika mahala pake"........kiss ya kwanza bonde la mchicha loooooooooo.....jamaa hakuamini... baada ya muda mfupi uhusiano ukaanza...

"Love for me is to trust yourself that your in love....thats what happened to me, pamoja nilikuwa mdogo ila nilijua kabisa huyu mwanaume nimempenda kwa dhati,love is trusting your partner enough to tell them everything about yourself,ukijumlisha na yale yooote you might be ashamed of, Love is feeling comfortable and safe with someone........thats what i felt when im around him Basi rafiki zangu, maisha yakaenda nikamaliza shule yaaani O level nikaolewa mwenzenu loooo.... yaliyofata kutokea hapo ni rahaaaaaaaaaa, uchungu ......rahaaaaaaaaaaaaa uchungu....... na sasa ndio raha kamili kila mahali....ndoa zina changamoto nyingi sana ni namna unavoichukulia wewe ndio itakuwa hivohivo, ndoa ni tamu asikwambie mtu, hata kama ni ndoano, ila ndoano yake ni ya aina ya pekee...

Nampenda sana Mume wangu mpenzi, Naendelea kuomba Mungu atupe afya mie na familia yangu, kwa maisha yetu yote, atulinde na mabaya yote, azidi kutupa nguvu na amani ndani ya ndoa yetu.......Ndoa yetu na iheshimiwe na watu wote,,,,AMIN
Hongera sana Gaga, tumejifunza mengi sana kutoka kwako, yaani kwa miaka mingi uliyokaa kwenye ndoa nahisi hakuna la kukubabaisha, nakuonea raha pamoja na kuolewa siku nyingi bado umri wako unadai kabisa, hongela sana bibie Mungu akuzidishie baraka tele
 
huwezi ukajua wakati mwingine bahati ya mwenzio pia yaweza kuwa ya kwako........it is implausible but you never know how the Almighty God works in people....................................aendelee kukaza buti mpaka kieleweke..............Let his gentleness be be known to all for the Lord is at hand...................
kwa kweli, bahati ya mwenzako usiilalie mlango wazi
 
Hahahahaaaaaaa, kwa kweli utundu wako ulilipa, ila inaonekana ulianzamambo ukiwa mdogo sana, jamaa huyo ni hatari sana
Wewe mtoto embu acha chokochoko
 
Hongera sana Gaga, tumejifunza mengi sana kutoka kwako, yaani kwa miaka mingi uliyokaa kwenye ndoa nahisi hakuna la kukubabaisha, nakuonea raha pamoja na kuolewa siku nyingi bado umri wako unadai kabisa, hongela sana bibie Mungu akuzidishie baraka tele
Nashukuru sana kama kuna kitu umejifunza kwangu dinnah, Mungu ni mkubwa sana na kwake yanawezekana yote
 
Hahahahahaaahaha, EMT thanx for the furniture, yaani naisubiria kwahamu, kwa kweli miaka imekatika bila hata kujua, machungu yapo tu ila nashukuru Mungu unakuwa unajua namna ya kuya handle..... hakuna ndoa inayoenda tu smooothly, mara nyingi lazima yanatokea kutokubaliana na mabishano ya hapa na pale, ila yakiisha mnasahau na kuendelea na maisha..ahsante sana EMT naisubiria zawadi yangu

Usiwe na wasiwasi tunaileta. Si unajua tena hizi foleni? Na umeme huku kwetu hakuna masaa 21 sasa.
 
Aisee Hongera Mdada kwa mafanikio uliyofikia, Mungu azidi kuibariki Ndoa yenu iwe na mafanikio zaidi na zaidi...
Angalau nimepata funzo kwenye hii story yako...
 
Be blessed guys 17yrs si jambo la kukaa kimya,tumeshuhudia ndoa za wiki 1,2 miezi.Najua maisha sio rahisi hivyo but you know how to face the challenges togethor.Nawatakia maisha mema jamani
 
Be blessed guys 17yrs si jambo la kukaa kimya,tumeshuhudia ndoa za wiki 1,2 miezi.Najua maisha sio rahisi hivyo but you know how to face the challenges togethor.Nawatakia maisha mema jamani
u
Charger nashukuru mkuu sanasana t
 
Aisee Hongera Mdada kwa mafanikio uliyofikia, Mungu azidi kuibariki Ndoa yenu iwe na mafanikio zaidi na zaidi...
Angalau nimepata funzo kwenye hii story yako...
nashukuru kama umepata funzo kupitia mimi
 
nashukuru kama umepata funzo kupitia mimi
Sweety za toka jana,siulizi sarakasi za jana usiku za anniversary, sasa unaonaje huyu jamaa ukampa notice kwamba utakuwa nae miaka mingine mitatu yaani jumla ishirini na kuna mtu huku uraiani nae anahitaji furaha ya miaka 5 hivi ?
 
hahhhahahahaaaa uporoto, kwa hiyo nimwambie baada ya miaka mitatu akae pembeni? duh haya kwa kuwa wewe ni swt wangu nitafikiria hilo , na sasa ukizingatia bado nina muda wa kufikiria
 
hahhhahahahaaaa uporoto, kwa hiyo nimwambie baada ya miaka mitatu akae pembeni? duh haya kwa kuwa wewe ni swt wangu nitafikiria hilo , na sasa ukizingatia bado nina muda wa kufikiria
Mwambie asiwe mchoyo bana miaka 20 imemtosha.
 
Back
Top Bottom