Tariq f
JF-Expert Member
- Dec 11, 2021
- 233
- 347
Habari wakuu!
Kuelekea Robo Fainali Tarehe 30 pale kwa mkapa hebu tuchukue hii kwanza...
Wakati macho ya wengi wakipiga hesabu za Themba Zwane, Teboho Mokoena, Peter Shalulile, Marcel Arende, Bongani Zungu nk.
Kwa bahati mbaya inakuwa kama ni danganya toto fulani hivi inayotumiwa mara nyingi na kocha Rulani Makwena, ambaye mara nyingi hutumia silaha moja hatari sana isiyozungumzwa nae ni Maseko ( silent killer).
Jina kamili anaitwa Thapelo Maseko aka Ndlovu , ni moja kati ya wanajeshi waliopeperusha bendera ya Bafana Bafana pale Ivory Coast na kukiwasha hasa. Alisajiliwa kutokea SuperSport na kuhamia kwa wababe wa Masandawana ( Mamelodi Sundowns) mapema mwaka jana. Ilichukua mechi 6 tu kwa kijana huyu wa 2002 kuitwa kikosi cha Taifa akitokea klabuni hapo.
Thapelo Maseko amekuwa miongoni mwa wachezaji tishio sana kwa Mamelodi Sundowns kutokana na style yake ya uchezaji inayotegemea Speed, akili, uwezo wa kutengeneza penalty na mashuti makali yanayowanyima usingizi wapinzani kila kukicha.
ONYO
Angalizo sana kwa backline ya Wapinzani wao Young Africans ikiongozwa na Captain Bakari Nondo juu ya mshambuliaji huyu.
MSISEME HATUKUWAAMBIA.
Kila la kheri