Thawabu niliyoipata kwa kuepuka kuzini na wanafunzi

StudentTeacher

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2019
Posts
4,153
Reaction score
4,301
Salaam wana JF,

Mimi ni mwanaume ambaye ninawiwa kutoka moyoni kujishughulisha na "Lishe ya ubongo" yaani Elimu. Ndoto zangu za maisha zimeegemea kwenye Elimu zaidi.

Sasa katika harakati za kuwafundisha wanafunzi huko mashuleni na mtaani pia nimekuwa nikikutana na mitego ya hatari kutoka kwa wanafunzi wangu wa kike. Ni visa vingi sana kwa kweli. Lakini hakuna hata kimoja nilichonasa. Nimeruka mitego yote kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

Kubwa kuliko ni pale binti mmoja(kidato cha pili wakati huo) akiwa amekaa dawati la mwisho kabisa aliwahi kuivuta sketi yake nusu ya mapaja yake, halafu akaichanua miguu yake kwa wastani wa nyuzi zaidi ya tisini(Obtuse angle) tena kimkakati kabisa na akahakikisha namuona na hakuonesha kushtuka kabisa zaidi zaidi alilegeza macho yake kwa matamanio ya kingono. Mazingira aliyokuwepo yalimpa ujasiri wa kufanya hayo yote bila wenzake kumshtukia. Lakini mimi niliendelea kufundisha hadi namaliza kisha nika-sign out.

Nilikuwa napangua visa vyao kwa kutumia akili ya ziada sana maana na wao walikuwa wananitega kijanja mno(ingawa kuna ambao walikuwa wanatumwa kwa makusudi mahususi). Kiukweli kwa mwanaume asiye na uwezo wa kuudhibiti "uanaume wake" kuingia mkenge kwenye ile mitego ilikuwa ni kugusa tu.

Ndugu mwana JF, usidhani kwamba nilikuwa mjinga kuikwepa mitego ile katikati ya kizazi hiki cha zinaa. La hasha! nilikuwa najua manufaa ya nikifanyacho ambayo hadi leo nayafurahia kwa furaha ambayo sina maneno ya kuielezea nikaeleweka kwa namna ninavyotamani nieleweke.

Baadhi ya manufaa hayo ni;

1. Mungu alizidi kuniamini na kuwekeza zaidi talanta zake ndani yangu ambazo si kwa ajili yangu tu bali kwa ajili ya watu wengine pia wake kwa waume.

(Hili alikuwa ananiambia na kunithibitishia kwa kinywa chake mwenyewe). Alikuwa ananivika furaha ya ajabu moyoni mwangu yenye kuashiria kwamba anapendezwa na maamuzi yangu hayo(Ni kawaida Mungu kunipongeza kwa style hii)

2. Kuepuka kutembea na mwanafunzi mmoja nyumbani kwao(baada ya yeye kuvizia tupo mimi na yeye tu akaniwekea bonge ya mtego wa kingono ngono), kumenitengenezea connection ya kupata zaidi ya shilingi milioni 9 (Baba yake ndiye kawa connector). Naamini ningejifanya chizi na kudiriki kuanza kutembea na binti yake kuna siku angeshtukia mchezo na kwa vyovyote tungekuwa maadui na ningeukosa msaada wake huu muhimu.

3. Wanajamii wanaonizunguka wananiheshimu kipekee sana hasa baada ya kujiridhisha kwamba mwanafunzi mikononi mwangu anakuwa salama kiroho, kiakili na kimwili pia. Hata wahuni hapa mtaani wananiheshimu sana na huwa wananitania wakisema "yaani ningekuwa ndio wewe vitoto vikijilengelesha ningekuwa navifyatua sana, unakwama wapi
ticha?". Mimi huwa nawajibu " Ni kwa sababu mmechagua kuishi maisha ya kujikinai".

4. Imeniongezea kujiamini zaidi.

NB: Namshukuru sana Mungu kwa kutupa sisi wanadamu uhuru wa kuchagua either "raha ya muda mfupi" au "raha ya milele" ili mwisho wa yote kila mtu awajibike kwa maamuzi yake.

Mbarikiwe sana!
 
Hongera saana

Lakini tegemea matusi ya kukunyanyapaa kisa mwalimu kutoka kwa vipanga wa jf
Yesu alivyokuja duniani miongoni mwa somo nililojifunza kwake ni "kuwa na ngozi ngumu" pindi ninaposimamia jambo la haki. Hivyo usijali mkuu. Nilishapangwa nikapangika kukabiliana na lolote wakati wowote.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Mtoto wa kike mwanafunzi anapata wapi ujasiri wa kujirahisisha kwa mwalimu wake?!?..
Sitaki kuhukumu ila nina mashaka na unajipresent kwao..


Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Labda haiba yangu mkuu. Ni mtu niliyefunzwa kujali sana utu wa mtu bila kujali jinsia wala upendeleo wa aina yoyote ile. Kuna mmoja nilijaribu kuwa harsh kwake ili aache sarakasi zake,ndio kwanza akawa anabuni "vitimbi" vipya. Mbona balaaa.Lakini pia wanaamini kwamba walimu vijana ni 'maharage ya mbeya'. Hili nilikuja kulibaini baada ya kufanya utafiti wangu mmoja maridadi kabisa.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…