THBUB: Tanzania nchi inayopaswa kuzingatia Utawala wa Sheria

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB ), Mathew Mwaimu amesema kuwa Tanzania Nchi inayopaswa kuzingatia Utawala wa Sheria na kwamba Mtu anapoona hatari anatakiwa kutoa taarifa kwenye mamlaka stahiki.

"Tunazungumzia Tanzania Nchi inayopaswa kufuata Utawala wa Sheria, hivyo kwa lolote linalotokea mtu ni wazi kila mmoja anapaswa kuhakikisha kwamba anapoona jambo la hatari anapaswa kutoa taarifa katika vyombo stahiki na vyombo hivyo vitaweza kuchukua hatua zinazostahili," amesema Mathew.

Anaongeza "Ni wazi kuwa Watanzania tunakoelekea siko kwa sababu nchi ya Tanzania ni Nchi ya kistarabu na ustarabu huu ndio unaotutaka kufanya kila jambo kuzingatia sheria."


Amesema wazi kuwa sio jambo jema kuondoa uhai wa mtu bila kuzingatia utaratibu wa kisheria, ambapo amesisitiza uzingatiaji wa Sheria.

Ameyasema hayo September 13, 2024 wakati wakifanya uzinduzi gari ambayo watakuwa wakiitumia kama sehemu ya kutekeleza majukumu yao katika maeneo mbalimbali nchini.

"Gari hili linakwenda kusaidia katika utendaji kazi hasa pale tutakapokuwa tunasafiri mikoani kwasababu moja ya shughuli za Tume nikutoka nje ya ofisi kwaajili ya kufanya uchunguzi, kutoa elimu kwa umma, na kwenda kufanya tafiti hivyo gari hili linakwenda kusaidia kazi nyingine nyingi zinazotekelezwa na Tume, " amesema Mathew
 
Sasa ukinyofolewa kwenye usafiri unafanyeje mkuu!?
 
Hii ndio ile tasisi iko pale mlangoni mwa Magogoni kabisa? Na inateuliwa na mwenye Nchi?

Tazama tu hili tamko😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…