The 1889-90 Brussels Anti-slavery Conference

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
The 1889-90 Brussels Anti-slavery Conference: Mkutano Uliozalisha Haya Yanayoendelea Afrika Ya Leo

Wajuvi wa mambo wana msemo kwamba “Historia ni mwalimu mzuri wa muda”. Lakini wengi wetu tumekuwa tukiichukulia misemo kama ni “Vitu vya kupita” bila kuipa uzito. Kwa wenzetu whites huwa wanatunza historia zao vizuri na kuzitumia kama mwalimu wao wa kipindi kijacho, kama ni historia nzuri basi watahakikisha in future watafanya vizuri zaidi ya hapo, kama ni historia mbaya basi watahakikisha haijirudii mbeleni.

Leo tujikumbushe kidogo kuhusiana na huu mkataba uliozalisha kile kinachojulikana kama Brussels Conference Act of 1890.

Moja ya sababu kubwa iliyowaleta wakoloni Afrika ni malighafi za asili zinazopatikana kwenye bara hili. Lakini kufuata malighafi tuu ilionekana sio sababu yenye mashiko sana ambayo ingewapa good justification ya wao kutawala hili bara. Ilihitajika strong ideological justification ambayo ingemake sense mbele ya masikio ya ulimwengu. Hivyo waliamua kuja na sababu ya “ubinaadamu na kukomesha ubaguzi wa rangi” (Humanitarianism and Racism). Kuanzia karne ya kumi na sita mpaka karne ya kumi na tisa takribani Waafrika milioni kumi na mbili walikuwa wametumika kama watumwa.

Hivyo basi kwa sababu uvamizi wa Afrika ulihitaji ideological justification, ndipo mataifa yenye nguvu kwa kipindi hiko yalifanya mkutano kwa takribani miezi 8 kuanzia Novemba 18, 1889 hadi Julai 2, 1890. Ndipo katika huu mkutano wakatengeneza mkataba wa pamoja wa kutokomeza utumwa na biashara ya utumwa (Brussels Conference Act of 1890). Ni huu huu mkataba/sheria ndio uliotumika kama sababu ya kuivamia Afrika kwa kivuli cha kutokomeza utumwa (Abolition of slavery and slave trade).

Kufikia mwishoni mwa karne ya 19 biashara ya utumwa ilionekana kama isiyo ya kibinaadam kulingana na maadili ya Kikristo na hata kulingana na sheria za nchi kama Ufaransa. Hivyo kulingana na mkataba huu, mataifa ya bara ulaya yalijiweka katika nafasi ya wakombozi wa Bara la Afrika, na huu msemo umeendelea kutumika mpaka sasa na mataifa makubwa pale wanapotaka kuleta mageuzi yoyote katika bara hili.

Mfano Waingereza walitumia sababu kuu 3 katika makoloni yao ambazo ni kuleta Ustaarabu, Biashara na Dini (Civilisation, Commerce and Christianity). Wafaransa wao kama taifa la kidunia (secular state) wakaja na civilising mission ambapo waliona kama ni wajibu wao kuleta amani kwa Waafrika, kuwaelimisha Waafrika kwa sababu itawafanya wakae mbali na maovu ya vita, magonjwa na njaa.

Kulingana na nadharia za kibaguzi zilizotengenezwa Ulaya kufikia mwishoni mwa karne ya 19, Waafrika waliwekwa kwenye kundi la chini kabisa/duni (inferior race) ambalo lilitakiwa kuelimishwa/kustaarabishwa na Wazungu. Hii racist justification ya ukoloni ilipewa kinga/uzito na nadharia bandia ambazo ziliwaweka Waafrika chini kabisa mwa racial hierarchy. Kwa hiyo huu mkataba ulimalizia kwa kusema kwamba “it is the ‘white man’s burden’ to educate an inferior race”.

Mpaka leo hii ninapoyaandika haya sijawahi kusikia kama hawa ma-giants walirudi tena kukaa na kuufuta huu mkataba. Na ndio maana kwenye mageuzi mbalimbali wayaletayo huwa wako kitu kimoja, akisema huyu wote wanaungana kukipa sapoti. Ni huu mkataba ndio ulioleta mabadiliko ya tamaduni (acculturation) barani mwetu na mpaka leo hii tunakaribia kuzisahau tamaduni zetu kabisa. Ni huu mkataba ndio ulitupa uhuru wa nadharia lakini kiuhalisia bado hatuko huru kujiamulia mambo nyeti mfano ushoga.

Hata ile historia tuliyofundishwa mashuleni imewekwa katika sura ya kuwaweka waafrika kama watu ambao tulikuwa kundi duni, tunaaminishwa kwamba ni kweli ilikuwa lazima waje wazungu ndipo tujikomboe. Lakini hamna vitu vya msingi vinavyofundishwa kuonesha jinsi maisha halisi ya Mwafrika yalivyokuwa. Hivyo kama Waafrika tunapoamua kuchukua maamuzi tuangalie nyuma ili tuone wapi tumekosea ili kupiga hatua za uhakika zaidi mbeleni.
 
Asante kwa thread naingia chimbo na mm nikiwapisha wajuvi wa mambo uwanjani...!
 
Satirical
IMG_20181121_231736.jpeg
 
Back
Top Bottom