Mwita Maranya, mie Fundi Mchundo bado hahahaa, kwa hiyo hilo mie halinihusu.
Ila kweli watu wa Ufundi huwa tunachemsha sana mara nyingi maana nasikia kuna jamaa alienda Ukraine kusoma na wakati akiingia jikoni, dada wa Kinigeria akawa kamaliza kupika na akataka kuzima jiko basi kaka wa Kizaramo akaona awahi kabla jiko halijazimwa "........... no no no, Don't put off, I'm Cooking on him......" hihihiiiiiii.
Kimbunga, tukiacha utani, sijui field nyingine ila kwenye Ujenzi, inabidi sana kufahamu Managements, Uchumi, fine Art nk maana kila Structure ya Wajenzi wanasema ni lazima iwe: Bei nafuu, Ipendeze kwa Sura, Itimize kazi inayotakiwa kufanya na Idumu.
Sasa basi hapo una mambo ya Uchumi na Sanaa. Ukiongeza kuwa jengo kabla halijajengwa, inabidi utengeneze Organisation ya Nguvu kazi (watu), Vifaa vya kutumia na Materials yake. Hapo kama wewe hujui uongozi, kazi itakushida. Ndiyo maana utaona leo Crane fulani inaletwa sehemu ya jenzi, kesho haipo au kifaa fulani kinakuja kwa muda fulani tu. Inabidi uchunge MUDA maara ukichelewa kukabidhi jengo, faini yake kwa siku si njema sana kwa faida yako.
Kuna sehemu USA walikuwa wamwage Zege na ghafla kukawa na maandamano. Ilibidi wafanye Booking haraka sana ya zile helcopiters za Zima moto na zikatumika kubeba Mitungi ya Zege ili waweze tu ku-keep Timetatble.
OGOPA MHANDISI WA UJENZI, NI KIONGOZI MZURI SANA.
Hahaha naona wewe unatafuta ugomvi na wahandisi.
Sikonge akikusikia tusilaumiane!