pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
@5,199 Metres, Mlima Kenya(Kirinyaga) ndio mlima wa pili kwa urefu barani Africa. Ml. Kenya na Mbuga la Wanyama la Ml. Kenya, viungani mwake, ni UNESCO 'World Heritage Site' na 'World Biosphere Reserve' pia.
Ml. Kenya una theluji kileleni na upo kilomita chache sana kutoka kwenye ikweta. Ambayo inapita Nanyuki, mji ambao upo chini ya 'slopes' za mlima huo.
Jambo ambalo watu wengi huwa hawalifahamu ni kwamba juu ya mlima huo kuna maziwa zaidi ya 25, yenye 'size' tofauti na ambayo yapo kwenye 'altitude' tofauti.
Maziwa yanayofahamika zaidi kati ya hayo 25 ni yale maarufu kama 'Top 4', kwa watalii. Yakiwa ni pamoja na Lake Rutundu(25 Acres) @3100Mtrs, Lake Ellis(28 Acres) @3,470Mtrs, Lake Alice(48 Acres) @3,500Mtrs, na Lake Michaelson(30 Acres) @3,950Metres. Pamoja na maziwa mengine kama Enchanted Lakes, Teleki Tarn, Nanyuki Tarn, Kami Tarn n.k, n.k.
Lake Michaelson.
Lake Rutundu.
Lake Alice
Lake Ellis
Enchanted Lake