sosoliso
JF-Expert Member
- May 6, 2009
- 8,540
- 9,473
Kwa TZ narudia tena wanaoweza kuendesha midaharo wanaweza kuwa ni Jenerali Ulimwengu na Tido Mhando,Prof.Shivji ana munkari anaweza kutia ndimu kwenye supu,kijana Pasco naye kaegemea sana Monduli.Dada Rose Mwakitwange yalimshinda.Kibonde ataleta mipasho ya Ikulu oyeee
Mkuu mfianchi hao wawili pamoja na mtangazaji mmoja wa zamani kutoka Radio Tanzania aitwae Edda Sanga ninaamini ndo wanaoweza kuendesha mdahalo.. Hawa wamiliki wa vyombo vya habari wafike wakati waone umuhimu wa kuwekeza ili wawapate waandishi na watangazaji wa televisheni wenye upeo wa kimataifa.. Wawasaidie kupata exposure katika fani yao kwa faida ya nchi.. Tulionao wamekosa sifa na weledi kwa kuwa wengi wao wameingia kwenye tasnia ya habari kimakosa..
Last edited by a moderator: