Wakubwa,
Si raha kuona yule ambaye unategemea kumpa kura yako akijieleza na kueleza mikakati yake namna hii. Inapendeza kweli, yaani hawa jamaa Mungu akiwasaidia uchaguzi wao ukaenda kwa amani, basi wametuacha. Hatuwapati tena, hii ndio demokrasia tunayoihitaji. Raia kupata habari bila ya vificho vificho, nataka kumpa kura mgombea ajieleze nimuelewe nipendezwe naye.
Tuna kila sababu ya kuwapongeza, tena kuchukua hatua ili nasi turudie utaratibu huu mzuri. Hii ilitakiwa iwe ni sheria, sio chama fulani kinaweza kuwaambia wagombea wake hapana.