Tupo wanafunzi wa MBA hapa schoo of busness tukitafakari nani anafaa kupewa dhamana ya urais sasa katika tuliopo hamsini 89% wamependekeza Kimea achukue fomu maana waliojitokeza hawaridhishi.Kimei amekuwa mtawala mzuri katika taasisi ya kibiashara na kampuni inaongoza kwa utawala wa raslimali watu, technolojia, ubunifu v tija na mahusiano na jamii
Hapo ni wapi mkuu, maana inawezekana mna mtizamo na dhamira njema; Je mnapendekeza kugombea kupitia Chama gani?
1. Kama ni CCM, hilo sahau maana si mwenzao na je ataweza kulinda maslahi ya Majizi ya CCM.
2. Kama ni Upinzani sidhani kuwa atapata nafasi kwa maana, ubavu wake wa kushindana na Sisimu ni Mwembamba.
Labda tu Mtueleze kama mnamshauri agombee kupitia CCM, maana huko wagombea waliojitokeza ni zaidi ya 12 kwa sasa, hii ni kwa sababu wameona urais ni kazi rahisi sana baada ya madudu mengi kufanywa na serikali ya chama chao.
My Take: Hapa tulipo kwa sasa kama nchi,basi tunahitaji
Mtawala na sio Kiongozi.....tunamtaka mtu mwenye Kuchukia Ufisadi si tu kwa Maneno bali kwa Vitendo (Kukamata na kufilisi mali zote zilizopatikana kwa njia ya hila).
Tunamhitaji Mtawala na wala si Mchumi au Kiongozi, kwa hali yetu tuliyonayo ya wizi wa mali ya Umma, Tunataka mtawala aweze kuisafisha nchi na baadae watatafutwa wachumi wazuri hata kutoka ugaibuni waje wamshauri kuhusu maswala ya Kiuchumi, wakati nchi ikiwa safi.
Ndani ya siku 100 za kushika dola awe amekamata Majizi yote ndani ya Utawala utakaokuwa umeanguka wa ma CCM.