Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ujamaa wa mwalimu ulitufumba macho,hakuna aliejua kama kuna epl wala la liga,radio ilikua moja na magazeti yake matatu ya chama na serikali,tulikaribia north korea ilivo sasa hiviHivi labda niulize kwanini hao mnaowataja hawakwenda kucheza soka la kulipwa? Au hakukuwa na soka la kulipwa? Binafsi mchezaji bora kuwahi kutokea ni
Mbwana samatta
Simon Msuva
Na
Shiza Kichuya
hajapata tu wakala kumtafutia team
Bwana mdogo lazima ujue nyakati zaenda zikibadilika kwa kasi kubwa. Fikiria Pelle wa Brazil na ustaa wake wote huo hakuwahi kucheza Barcelona ama Madrid timu ambazo ndo kipimo cha ustaa duniani kwa sasa. Kwa jumla hakuwahi kucheza hata timu ndogo ya ulaya kama West ham utd. Nyakati hizo Dunia haikuwa imefunguka kama sasa na after all kwanza mpira ulionekana kama kitu cha kuburudisha pekee hakuna aliyeupa value kihivyo. Halafu we unafanya mzaha na suala la kwenda ulaya, kwanza mtu angeenda vipi ulaya? Zama hizo ungeweza kung'ara kinoma ukiwa kwenu Karagwe na usithubutu tu hata kwenda Dar kutafuta team. Lakini pia hapo nyuma kigodo ubaguzi ulikuwa bado uko peak. Kiukweli kulikuwa na combination ya mambo kibao yaliyowafanya wasifike ulaya. Ni kweli kwa sasa Samatta ni best kwa Tz lakini sina uhakika sana kama anaweza kuwa yuko juu ya Mogella wa 1984 CCM Kirumba dhidi ya National Al Ahly akipiga bonge la bao la kusawazisha dk 37 akijibu goli la mapema la Mohamed Al Hatib huku baadaye Simba wakishinda kwa goli la pili la Mtemi Ramadhani second half. Alikuwa Mogella wa kuamua matokea, bahati mbaya alikuwa Mogella mmoja ndani ya kundi la wachezaji wa kawaida. Tusingeweza kufika popote kama ambavyo Liberia wakiwa na George Wear hawakuweza kufika popote.Hivi labda niulize kwanini hao mnaowataja hawakwenda kucheza soka la kulipwa? Au hakukuwa na soka la kulipwa? Binafsi mchezaji bora kuwahi kutokea ni
Mbwana samatta
Simon Msuva
Na
Shiza Kichuya
hajapata tu wakala kumtafutia team
R.I.P Said (Kizota)
Edibily Lunyamila
Kuna m1 wa zamani aliwekwa mpaka kwenye stamp. Nani sijui jona lake....
Funguka vizuri hapo mkuu.Ugolo wa mzee akili Mali ni kitu gani?