The Bold Interview: Maisha, Intelijensia na mengi usiyoyajua

The Bold Interview: Maisha, Intelijensia na mengi usiyoyajua

Status
Not open for further replies.
Hahaha

Mkuu namshukuru Mungu vile ameniumba... Sidhani kama kuna kosa lolote jinsi ameniumba


Mi naona Bongo safi tu! Kuna mambo kibao yanatia hasira but futafanyaje?? Tanzania ndio mama yetu, tutaenda kila sehemu lakini lazima turudi Bongo


Nadhani wanaonizunguka ndio wana nafasi nzuri zaidi ya kujua udhaifu wangu kuliko mimi mwenyewe
Hahahaha
Aisee hivi ulishawahi kuibiwa au kutapeliwa?
Unaweza kushea nasi Ilikuwaje?

-Hivi kuna njia zozote au rules ambazo umeamua kuzifuata ili kukuepusha usiibiwe wala kutapeliwa?
 
Kabla hatujahama hebu Tueleze
-Kwamfano ukiambiwa ukadirie thamani ya ID yako ya JF, unahisi itafika kama tsh ngapi hivi?
Je, endapo mtu atafika dau la kiasi fulani, unaweza kuiuza?
 
Nipo kaka,naanzaje kubanduka hapa sasa? Narefresh huu uzi kila sekunde kama mwendawazimu [emoji85]

Yeah,kanifurahisha sana kwakweli. Hadi nimevunja ukimya.

Mwandalie vinywaji na sambusa ili nishat iende sawia.
 
Sawa, ila usisahau tu..
Sasa hebu tujuze
Je kitu ulichokisomea ndicho kinachokusaidia kusumuka maisha? Why??
Yes and No...

Yes kwa kuwa nimeanza kulitumikia Taifa tangu niko chuo... So kwa namba fulani labda nilipata hiyo deal kwa sababu ya Elimu...

No kwa sababu nilichokisoma sikitumii sana katika utumishi wangu...

But again Yes kwa kuwa nilichosoma kinanisaidia kuwa na good reasoning na kuelewa mambo kwa mapana.
 
Shahada ya kwanza...

Uchumi, Mzumbe University
Enhee umejileta mwenyewe...
Sasa nijibu haya maswali yafuatayo-
Tunafahamu kwasasa uchumi kidogo umeyumba hasahasa kwenye mifuko ya watu wengi, na vilevile fursa zimekuwa ngumu zaidi, je
unaweza kushea au kutoa sadaka idea yoyote ile ya kibiashara au fursa uliyonayo(uliyoiona)?
 
Yaani haya maneno mawili yamenifanya jioni yangu iende vzr aisee..
Mchapio murua huu kutoka kwa stunter..
Kipajo==Kipato
Kusumuka==Kusukuma..

Na hili
Photoshop ==Picha Duka
 
Hahahaha
Aisee hivi ulishawahi kuibiwa au kutapeliwa?
Unaweza kushea nasi Ilikuwaje?

-Hivi kuna njia zozote au rules ambazo umeamua kuzifuata ili kukuepusha usiibiwe wala kutapeliwa?
Nishawahi kutapeliwa... Yes

Ila ni kwa sababu ya uaminifu tu... Tena mshkaji ndio alinitapeli

2014 nilikuwa nataka assist kutoka bank kama milioni 15 au 20 kuna project fulani nilikuwa naifanya so nataka kuipanua zaidi...

Jamaa huyo mtoto wa mjini wale Loan Officers ni watu wake wa karibu... Sasa si unajua bank zetu magumashi mengi... Unataka loan japo ufailipa ila lazima utoe rushwa ndio upewe...

Basi jamaa ndio akawa kiunganishi kati ya mimi na wale loan officers... Kila siku lete laki wanataka, sijui kuna nini lete laki mbili... Mara kesho kutwa laki nyingine... Mpaka zikafika laki 7

Kumbe wajamaa wanajenga heshima baa tu

Hiyo 15M/20M sijaipataga mpaka leo...

Ila nilimsamehe tu mwana... Now tuko fresh tu! Mototo wa mjini so namtumia kwenye mambo mengi...

Now sijui iweje mpaka mtu anitapeli
 
The bold
Kipi ni sahihi kwako kati ya serikali kumiliki fedha nyingi kisha wananchi hawana kitu, au wananchi kuwa na fedha nyingi alafu serikali haina kitu? Why?
(Ningependa ujibu hili swali kitaalamu hasahasa katika kubalance hali ya maisha)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom