Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,650
- 6,084
The – book – I – Read, 2024
Ni wakati mwingine tena wa mwisho wa mwaka, tunapoelekea kuhitimisha mwaka 2024, na kuimba ule wimbo maarufu wa “Auld Lang Syne, tukimaanisha ‘For the Sake of Old (good) Days,’ ikiwa ni ishara ya kuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mwingine (au kusheherekea kukamilisha jambo).
Mwaka huu, katika ‘The-Book-I-Read’, inayohusisha kusoma machapisho mbalimbali, lakini hasa vitabu, majarida/makala za kimataifa, nilikuwa na hamu na kufanya jitihada za kumalizia ‘viporo’ kwa kuendelea na vitabu ambavyo hadi mwaka wa jana unamalizika, sikuwa nimemaliza kuvisoma.
Hamu na jitihada hizo zikanisukuma pia kusoma vitabu vipya kadhaa, pamoja na kurejea kusoma vingine ambavyo nimewahi kuvisoma huko nyuma zamani.
Katika ‘mradi’ huu wa kila mwaka, jambo mojawapo muhimu naendelea kujivunia ni kupambana na kupata muda wa kusoma, katikati ya mbiombio za ratiba ngumu za maisha ya kila siku.
Kama ambavyo imekuwa ada kwa awamu zilizopita, mwaka huu 2024 pia jumla ya ‘readings’ ambazo nimefanikiwa kusoma, zinatokana na kusukumwa na mambo anuai, ikiwa ni pamoja na mapito/mapitio mbalimbali ya maisha ya kila siku; kutafuta maarifa na taarifa zaidi katika maisha na kujaribu kuongeza utaalamu au ujuzi zaidi wa kitaaluma na kikazi. Muhimu zaidi ni KUJIFUNZA.
Hivyo ‘readings’ zote nilizofanikiwa kusoma, zinatokana na kusukumwa kutaka kuelewa zaidi muktadha wa mambo yanayotuzunguka au kutukabili ili kuongeza mwanga wa ufahamu, kubadili mtazamo wa namna ya kuyakabili, pia kuongeza wigo wa fikra ili kuvielewa vitu/ kuwaelewa watu na mazingira yetu wanadamu. Hivyo katikati ya ratiba mbiombio na mikikimikiki ya mwaka huu, nimefanikiwa kurejea;
Ugumu na urahisi wa kupata muda unahusisha kuupangilia na kuugawanya au kuutumia muda vizuri, wote wa kazi, familia (kama unayo), masuala ya kijamii na ule wa masuala binafsi.
Inahitaji kushinda majaribu yanayoletwa na teknolojia, ambayo yanawalazimisha binadamu kuwa rafiki wakubwa wa simu zao za mkononi, kuliko wanavyoweza kuzingatia ‘table manners’ wakati wa kula na familia au wenzi wao au kuliko wanavyoweza kutenga muda wa kusikiliza wenzao wakati wa mazungumzo au kuliko kutega sikio kwa watoto wao baada ya mihangaiko ya siku nzima.
Ili kuweza kumudu changamoto hizo, binafsi, kama nilivyoonesha huko juu, nimeamua kuyaheshimu sana masuala yanayonisukuma kusoma. Nimeshayataja huko juu. Jambo jingine kubwa ninaloweza kuongeza, ni namna ambavyo napambana kutumia ‘geopolitics trending’ kusoma. Kwamba matukio mbalimbali yanapotokea, yananisukuma kutafuta vitabu au reports zinazohusu masuala hayo. Nakuwa nimejilazimisha kuchukua na kusoma vitu kadhaa kwa wakati mmoja ili kuvielewa.
Lakini katikati ya masuala hayo yanayoweka msukumo wa kusoma, bado lengo kuu linakuwa ni KUJIFUNZA zaidi na zaidi.
Mwaka huu tena sijafanikiwa kuanza kusoma kitabu cha “My Life My Purpose” ambacho ni autobiography ya Hayati Benjamin Mkapa, kama nilivyodhamiria. Panapo majaaliwa nitakianza pia na bila shaka nitafanikiwa kukimaliza, sambamba na Tawasif (biography) ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, iliyoandikwa na Profesa Issa G. Shivji, Profesa Saida Yahya-Othman na na Dkt. Ng'wanza Kamata.
Wakati huo huo nikiendeleza ‘ndoto’ zangu, siku moja kuweza kuandika kitabu chenye jina la “Die or Survive, Make or Break, Crash or Win; A Year That Was, ambalo kwa uhakika lilitokana na ushawishi wa mwanazuoni nguli, Noam Chomsky, kwenye kitabu chake “Hegemony or Survival; America’s Quest for Global Dominance”.
Makene, Tumaini
“Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; mshike, maana yeye ni uzima wako.”
“Tafuta elimu hata kama ni Uchina…”
“Watu walio hatari sana ni wale ambao wanafikiri kuwa wanajua kila kitu, wala hawana haja ya kujifunza zaidi. Hii ni tabia mbaya ambayo huzuia kabisa maendeleo.”
“Reading is essential for those who seek to rise above the ordinary.”

- Biblia
- Intellectuals At The Hill: Essays and Talks 1969 – 1993, Issa G. Shivji
- Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; Chemchemi ya Fikra za Kimapinduzi, Makala, Hotuba, Mashairi na Tenzi Teule, kilichohaririwa na Dkt. Bashiru Ally Kakurwa
- Seize The Day with Dietrich Bonhoeffer, by Charles Ringma
- Ujamaa ni Imani, Azimio la Arusha, by Julius K. Nyerere
- Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, by Julius K. Nyerere
- Kufa na Kupona, A. E. Musiba
- Mirathi ya Hatari, by Mung’ong’o C.G
- Misingi ya Falsafa, Itikadi, na Sera za Chama Cha Mapinduzi, kimehaririwa na Dkt. Bashiru Ally Kakurwa
- Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu, cha Mzee Ali Hassan Mwinyi
- Why and How The CPC Works in China: A look at what’s behind the achievements of the Communist Party of China, Revised edition, edited by Xie Chuntao
- Kickback: Exposing The Global Corporate Bribery Network, by David Montero
- TUMAINI: A Journey of Hope In The Heart of Africa, Katie ST. Germain
- Flashes of Thought: Inspired by a dialogue at the Government Summit 2023, by Mohammed bin Rashid Al Maktoum
- The Prime Ministers: Reflections on Leadership: From Wilson to Johnson, by Steve Richards (revised and updated)
- Myths and Legends of the Swahili, by Jan Knappert
- Utatanishi na Ukimya Katika Rasimu ya Katiba Mpya: Mhadhara wa Kuaga Kigoda cha Mwalimu, by Issa Shivji
- Tukumbuke Tulikotoka, 1954 – 1964, by Yahaya Suleman Ngoma (Katibu Veterani wa UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam).
- The First Political Order, How Sex Shapes Governance
- and National Security Worldwide, by Valerie M. Hudson,
- Donna Lee Bowen and Perpetual Lynne Nielsen
- How China Escaped The Poverty Trap, by Yuen Yuen Ang
- Rootless: There are two sides to every love story, by Krystle Zara Appiah
- Welcome to 2030: GLOBAL TRENDS TO 2030: CHALLENGES AND CHOICES FOR EUROPE, by Florence Gaub, European Union Institute for Security Studies (EUISS) (2019).
- With energy at play in the Ukraine war, everybody pays, by Izabela Surwillo and Veronika Slakaityte, Danish Institute for International Studies (2022).
- The Ukraine War: Preparing for the Longer-term Outcome, by Anthony H. Cordesman, Center for Strategic and International Studies (CSIS) (2022).
- Root Causes of Unrest and the Continued Increase in Global Uprisings, the Age of Mass Protests, Understanding an Escalating Global Trend, by Samuel J. Brannen, Christian S. Haig and Katherine Schmidt (Center for Strategic and International Studies (CSIS) (2020).
- Ukraine CONFLICT UPDATE, by Institute for the Study of War (2022).
- Nayakumbuka Yote, Hoyce Temu (kwa sababu nakusudia kuendelea kujifunza kwa wengine, wakati nikiendelea kufanyia kazi ‘project’ yangu pia)
- 38 Reflections on Mwalimu Nyerere, by Mark Mwandosya and Juma V. Mwapachu (editors and contributors).