Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Ngoja tucheki tuhuma za Dr. Slaa kuhusu Karamagi zilihusu nini hasa...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwafrika wa kike hapa naweza kupingana kidogo na wewe. Tanzania wanaopokea rushwa na wanaonunulika kirahisi ni mahakimu na sio majaji. Majaji waliowengi ni watu wenye msimamo wanajua wanachofanya. Lakini pia wakienda kinyume na serikali wanawekwa kando maamuzi yao huwa hayatekelezwi. Serikali yetu huwa inatunga sheria yenyewe kupitia wabunge wa CCM, na kuzitekeleza kupitia wabunge wa CCM na kuzivunja kupitia mawaziri wake. Kama utakumbuka hoja ya mgombea binafsi, pamoja na kuwa mahamaka kuu iliruhusu S. sitta wakati huo akiwa waziri wa sheria aliitolea nje.
tatizo ni kuwa mahakama Tanzania isipotendewa haki haina pa kwenda kushitaki, ndio maana serikali inafanya inavyotaka. Kama tungekuwa kwenye Privy coincil labda mahakama ingeheshimiwa kidogo.
Lakini hata hivyo still, naweza kusema sijui JK ameteua majaji wangapi na kama ni majaji wa mambo ya sheria au ni majaji wa siasa. Inawezekana kuwa wameshapiga mahesabau yao na sasa wanaanza utekelezaji wa kumsilence Slaa na upinzani.
.... i hope and pray that you are right on this one
Katika hili wewe uko right na wala sitapingana nawe hata kidogo..
the past experience ya maamuzi ya mahakama inanifanya niwe kinda of worried.... but yangu macho.... i hope and pray that you are right on this one
haya ni maneno ya Mzee Mkapa
"Napenda tujikumbushe maana upo uwezekano wa wana-CCM kubweteka. Kwa vile tunajua chama chetu kina nguvu na mvuto, hatuweki mkazo mkubwa kwenye kujinoa binafsi. Badala yake tunapigana vikumbo kutafuta kuteuliwa, kwa kuamini ukishateuliwa ndio umeula. Na tukishaelekea huko, hakutakuwa na kingine kinachotusukuma ila ubinafsiubinafsi wa kusema mimi lazima niendelee, na anayenisogelea ni adui; au ubinafsi wa kusema wewe sasa imetosha, sasa ni zamu yangu."
hawa ndio wasaniii mabao mzee mkapa alikwishawaona nadhani utabiri umetimia,mambo ya Buzwagi ni matokeo ya "ukishateuliwa ndio umeula.
karamagi nenda ,ila Mzee Mkapa alitabiri mtakuwapo watu kama nyie,unasubiri nini Kusijiuzuru Uwaziri?
source:HOTUBA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM MKAPA, KWENYE MKUTANO WA HALMASHAURI KUU YA CCM, DODOMA, 25 AGOSTI 2004
Link:http://www.ccmtz.org/hotuba/040825nec.htm
Hivi hao jamaa apo kwenye picha-nadhani 'wasaidizi' wa waziri...ndo wamemshauri aitishe mkutano na waandishi? Maana mi naona kama hili linaweza kuwa na athari mbaya zaidi kwake kuliko ilivokuwa kabla?