The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

The Buzwagi Saga: Karamagi aenda kusaini Mkataba wa ULAJI London

Mmekwisha ona mfa maji?kwake yeye hata akipita kenge mbele yake atataka amdadie mgongoni akidhani huo ndio wokovu wake.Ndivyo ilivyo sasa kwa CCM,chama ambacho kwa muda mrefu kimejigamba kuwa ni makini na chenye viongozi bora,nini sasa wanafanya?mfa maji! Kama wanaweza kuwatumia kuwasafishia watu kama Akwilombe na Tambwe basi kwisha kazi! maana hayo si ni makapi ya vyama vile wanavyoviita vya 'ovyo ovyo?' ukiona hivyo,mfa maji!
 
Unajua kuna hali ya mtu kuwa mwehu lakini asiweze kujijua .Maneno ya akina Hizza an Akwilombe yananikumbusha miaka ile Mrema anagombea Temeke .Mgombea wa CCM Sisco alisimama pale kurasini kwa kukosa neno ama sera akaanza kuhubiri kujuana na ukabila na akasema haya , Naombe mnichague mimi ni msela mwenzenu na muda mtoto wa Temeke, pia nilikuwa mwizi wa minazi hii hapa wakati niko mtoto . Watu wakashangaa .

Tambwe kwa uongo , uhuni ni sehemu ya maisha . Maana kama anaweza kughushi vyeti vya shule kitendo ambacho hata Lamwai anamjua kilipelekea kuenguliwa toka kugombea kiti cha Ubunge akiwa NCCR akaja kusaidiwa na nguvu ya vijana .Sasa Tambwe si mtu wa kumwamini maana ni mtu wa mission town .Kakutana na Makamba sasa wanafunga watu kamba.Akwilombe ni mtupu siwezi kumsemea .

Wote 2 hawakubaliki kwa watu wenye akili timamu na ndiyo maana wameenda CCM wamekubalika sasa leo sitashangaa kuona na kusikia haya . Ni maajabu kwamba Tambwe kagombea Temeke ambako aliamini kwamba angalishida hata nafasi ile kwa kuwa kaenda huko bado kamwagwa . wacha agange njaa na ila mwisho wa Makamba unakaribia na Hizza na Akwilombe wataishia hapo pia .

Lakini pia wasameheni uwezo wa kuchambia na hata kusoma alama za nyakati ni mdogo maana hawana shule ya kuwatisha pia hili msije lisahau.
 
Kuna habari ifuatayo inatia wasiwasi, soma hapa:
Mh. Zitto hatarini

2007-09-27 16:14:17
Na Usu-Emma Sindila, Jijini


Kuna habari kuwa Mbunge machachari wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe yuko katika hatari kubwa baada ya kutishiwa kuuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wapinzani wake kisiasa.

Habari toka kwa watu walio karibu na Zitto, zinadai kuwa vitisho anavyodaiwa kuvipata mbunge huyo toka kwa wapinzani wake, vinadaiwa kutumwa kwa njia ya meseji za simu.

Watu hao wa karibu ambao hawakupenda kuandikwa majina yao, wamesema watishaji wa maisha ya Zitto wanadaiwa kumueleza kuwa asipokuwa makini na kuendelea `kuchonga` juu ya suala la mikataba ya madini ambalo ni kubwa kuliko uwezo wake, basi ajiandae kwenda kuzimu.

Imedaiwa kuwa mbunge huyo amesisitizwa kuwa awe mpole kuhusiana na mambo hayo kwa kuwa yeye hajui chochote kuhusiana na nchi inakoelekea.

Alipoulizwa juu ya madai hayo katika mkutano na waandihi wa habari jana pale kwenye Makao Makuu ya chama chake cha CHADEMA, Mhe. Zitto alisema hilo ni suala la kipolisi na hivyo yeye hawezi kulizungumza.

Aidha, aliwataka waandishi wa habari waliokuwa wakitaka kujua undani wa madai hayo ya vitisho, kuwawasiliana na Mkurugenzi wa Kamati ya Ulinzi ya CHADEMA, akidai kuwa yeye ndiye anayefahamu zaidi kuhusiana na suala hilo.

Hata hivyo, alipofuatwa baadaye na mwandishi wa Alasiri, Zitto akasisitiza kuwa yeye hawezi kulisema.

`Jamani si kila kitu cha kuweka hadharani hukawii kusema ni kweli, halafu kesho ukakuta liko front page (kurasa za mbele) ya magazeti yote nchini,` akasema.

Hata polisi walipoulizwa leo asubuhi na gazeti hili iwapo wamepokea taarifa zozote kutoka kwa Bw. Zitto kuhusiana na vitisho hivyo, walisema hawajapokea taarifa hizo.


SOURCE: Alasiri

Source link: Ipp Media.

SteveD.
 
Mzee mwanakiji,ziafanyie jitihada za haraka tupate mkataba wa buzwagi in Pdf fomat,wanakijiji wengi mamcho yamewatoka wanataka kuusoma kwa undani
 
mzee mwana kijiji, naunga mkono hoja ya mkomboziufisadi ya happo juu. vyema pia ukipata na nakala ya original ya kimombo kwa wale wanaouelewa.

macinkus
 
Huyu Akwilombe mzigo wa kulea wake wanne unamuelemea ana ganga njaa huyu ni wa kusamehewa tu...
 
Gazeti la Majira!

Good,
Ndo maana makala yenyewe iko hivi!
Poor jounalist! Inatia huruma sana pale mtu inapo bidi 'ucompromise' taaluma yako, kwa kuambiwa uandike kile ambacho una ambiwa uandike si kile unacho kiona ama unacho tafiti na kugundua!
 
hamna mtu wa kuweza kumuua Zitto,hao vitisho vyao ni mbuzi tu,na endapo hilo litatokea basi moto wake hautazimwa.
 
Huo mkataba mbona umekuwa elussive kiasi hichi? utafikiri tunasubiri gazeti la Mfanyakazi Jumamosi? yaani pamoja na kuwepo kwa Internet lakini huu mkataba umekua elusive vipi kikosi cha upelelzi cha JF mbona mnatuangusha?


Vile vile tunaomba mtupatie format ambayo itakuwa rahisi kuisambaza hii mikataba na ile listi ya wala RUSHWA kirahisi online


waslaam
 
Chakaza,
Jamaa yangu umenivunja mbavu.Maana nimejaribu kuangalia size ya kenge na binadamu, nimechoka mwenyewe.
 
Hapo ndipo watakapoona kanga anavyonyolewa mzima mzima.
 
Leop Polisi wanakataa kwamba hawajapata taarifa ila nina uhakika IGP na Manumba wana habari tangia mwanzo Zitto anatoka Bungeni.Hali ya Usalama wa Zitto inahofiwa mno kwa kuwa Nchi hii utawala bora ni ndoto.Lakini huko majuu ma scandals zinatokea na watu wanasema kwa uwazi .Nasema Zitto utaishi maisha marefu sana maisha yako mwamuzi ni Mungu na ulinzi uko kwa kila Mtanzania na hao wapambe wa hao mafisadi hawatajaribu kuipa Serikali ya CCM wakati mgumu tena baada ya kuipeleka pabaya kule Dodoma na Mikataba. Serikali iko macho na inajua nguvu ya Zitto sasa .
 
Kuna gharama ya kulipa katika ukombozi. Zitto anaelewa hilo na wale wote ambao tumekuwa tukiikosoa serikali na kuipinga tunajua gharama hiyo. Wakati mwingine gharama hiyo ni lazima ilipwe. Hata hivyo haiwezi kulipwa kirahisi hivyo. Hivyo ni jukumu la serikali ya CCM na viongozi wake kuchukua hatua zote zilizo ndani ya mikono yao kuhakikisha kuwa Zitto hajikwai, na Dr. Slaa haumwi na mbu!!
 
zitto kuuliwa ni ndoto ya alinacha kwa sababu wanajuwa kuwa hawawezi kuweka kibiriti kwenye petroli
 
PRESS RELEASE – Issued by Barrick Tanzania
Barrick Gold Named to Dow Jones Sustainability Index

September, 2007
TORONTO, ON – Barrick Gold Corporation has been added to the annual Dow Jones Sustainability Index (DJSI) - North America for the first time, ranking the company as best-in-class for its ongoing commitment to sustainability.



One of the world’s foremost indices of corporate social responsibility, DJSI is based on a comprehensive review of corporate sustainability practices by companies.

Independent research conducted for DJSI focuses on a broad range of economic, social and environmental performance criteria, using both general and industry-specific measures.



“We are very pleased that Dow Jones has recognized Barrick as a leader in corporate social responsibility,” said Greg Wilkins, Barrick CEO and President.

“We are convinced that our global commitment to responsible mining is making us a stronger and more successful business. I know that our employees are committed to responsible mining practices every day and have made this significant recognition possible.”



In commenting on the ranking, CEO Wilkins renewed the company’s pledge to continuously improve Barrick’s corporate social responsibility performance.

Established in 1999, DJSI is used by investors and asset managers as a benchmark and is considered influential in investment decision-making, particularly
for socially responsible investors.



For further details, a copy of the news release issued by the Dow Jones Sustainability Indexes is available at www.sustainability-indexes.com. Barrick’s 2006 Responsibility Report can be downloaded at www.barrick.com/corporateresponsibility.



The Report is independently reviewed by Environmental Resources Management, a global provider of environmental, health, safety and social consulting services. It is developed in accordance with the Global Reporting Initiative and documents key areas of progress during the year as well as areas where the company can improve in the future.
###



Barrick Yaingizwa katika Orodha ya Kampuni zenye sifa ya miradi endelevu

Septemba 17, 2007

TORONTO, ONTARIO – Kwa mara ya kwanza kampuni ya Uchimbaji Dhababu ya Barrick imeingizwa katika orodha ya mwaka ya Dow Jones ya Waendelevu (DJSI – Dow Jones Sustainability Index) kwa eneo la Amerika Kaskazini na kutajwa kuwa kampuni bora zaidi katika daraja lake kwa kujitolea kwake kwa miradi endelevu.



Ikiwa ni moja ya orodha mashuhuri zaidi ya kupima uwajibikaji wa mashirika kwa jamii, orodha ya DJSI hutegemea mapitio ya kina ya utendaji endelevu wa makampuni. Utafiti huru unaofanywa kwa niaba ya DJSI hupima utendaji wa kiuchumi, kijamii na kimazingira kwa kutumia vigezo vya jumla na vya ndani ya taslia.



“Tunafurahi kwamba Dow Jones imeitambua Barrick kama kinara katika uwajibikaji wa mashirika kwa jamii,” alisema Greg Wilkins, Afisa Mtendaji Mkuu na Rais wa Barrick. “Tunaamini kwamba kujitoa kwetu kuwa na uchimbaji duniani wenye kujali, kunatuimarisha na kuwa na mafanikio zaidi katika shughuli yetu. Ninafahamu kwamba wafanyakazi wetu wamejitoa kuwa na uchimbaji wenye kuwajibika kila siku na ndiwo wamewezesha kutambuliwa kwetu.”



Akizungumzia kuorodheshwa huko, AMM Wilkins alirudia tena ahadi ya kampuni ya kuendelea kuboresha uwajibikaji wa Barrick kwa jamii. DJSI, ambayo ilianzishwa kwaka 1999 hutumiwa na wawekezaji na wasimamizi wa raslimali kama kiwango na huonekana kuwa na ushawishi kwa maamuzi yanayohusu uwekezaji, hasa kwa wawekezaji wenye kujali uwajibikaji kwa jamii.



Kwa habari zaidi, nakala ya taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Orodha ya Dow Jones ya Waendelevu inapatikana www.sustainability-indexes.com. Ripoti ya Barrick ya Uwajibikaji mwaka 2006 inaweza kupatikana www.barrick.com/corporateresponsibility.



Ripoti hiyo hupitiwa na Kampuni ya Environmental Resources Management, ambayo ni huduma huru ya ushauri katika masuala ya mazingira, afya, usalama na uwajibikaji kwa jamii. Huandaliwa kulingana na vigezo vya Global Reporting Initiative na huelezea mwenendo muhimu wa mwaka na maeneo ambayo yanaweza kuboreshwa katika siku zijazo.
 

Attachments

Back
Top Bottom