Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
TRAILER YA THE CHURCH OF THE UNBORN!
Ndani ya jumba la Cinema lililoko Mlimani City. Ukumbi umejaa. Watu wanashauku ya uzinduzi wa filamu mpya ya The Church of the Unborn" ambayo inatokana na Riwaya yenye jina hilohilo, The Church of the Unborn, Mtunzi akiwa Robert Heriel na ndiye muongozaji wa filamu hiyo.
Ni saa tatu kamili usiku.
Jukwaa amesimama Mtunzi Robert Heriel na pembeni yake akiwepo Waziri wa Sanaa, utamaduni na michezo. MC anatangaza uzinduzi wa filamu. Pazia la damu ya Mzee linafunguka polepole, na skrini kubwa iliyopo ukutani inaonekana.
Watu wote wanapiga Makofi na kushangilia, kisha filamu inaanza kuonyesha utangulizi wa filamu. Kama ifuatavyo;
Ndani ya wodi ya uzazi – usiku wa manane.
ZARA, uso wake umechoka lakini macho yake yamejaa wasiwasi. Amekumbatia blanketi lililomfunika mtoto aliyeletwa kwake. Anaangalia uso wa mtoto… anasisimka. Anaangalia tena. Halafu kwa sauti ya hofu, anasema:
ZARA:
“Huyu si mtoto wangu… huyu si mtoto wangu!”
Wauguzi wawili wanatazamana. Mmoja wao, Jenny, anajaribu kumbembeleza kwa sauti laini:
JENNY:
“Mama... umepitia uchungu mwingi. Acha upumzike kidogo, akili yako bado haijakaa sawa.”
ZARA:
“La hasha! Huyu mtoto si wangu! Mtoto wangu nilimwona... nilimshika! Alilia! Alikuwa na alama ndogo hapa—” (anaonyesha begani mwake mwenyewe)
Muuguzi mwingine, SISTER Susy, anamshika begani kwa nguvu za pole:
SISTER SUSY:
“Mama, pole. Tulijitahidi lakini moyo wa mtoto ulisimama ghafla. Tafadhali tulia.”
Zara analia, haamini. Macho yake yanazunguka, anatafuta msaada. Hakuna mtu anayemsikiliza.
SEHEMU INAKATIKA – Kamera inafuata mtoto mchanga asiye na fahamu, akiwa amefungwa kwa taulo jeupe, akiwekwa kwenye sanduku la plastiki la wagonjwa. Anabebwa kwa haraka na mwanaume aliyevaa koti la madaktari. Huyo mwanaume anatoka kupitia mlango wa nyuma wa hospitali.
Nje ni usiku wa giza totoro. Gari jeupe lisilo na namba linafunguliwa haraka. Sanduku linaingizwa. Mlango unagonga kwa nguvu — gari linaondoka kwa kasi.
MUDA HUO HUO – SAUTI YA NARRATOR (MTAYARISHAJI):
"Katika kivuli cha imani, siri kubwa inafichwa. Siri ambayo ikifichuliwa, inaweza kuyumbisha misingi ya dunia nzima ya kiroho..."
MZIKI WA KUTISHA UNAINGIA — SCREEN INAGEUKA KUONYESHA:
KANISA LA LIGHT OF THE CHOSEN – lenye maelfu ya waumini, taa, vicheko, mapambio, na… damu.
KISHA SKRINI INAKUWA GIZA, ghafla inawaka na maneno THE CHURCH OF THE UNBORN yanatokea, rangingeyake ya dhahabu.
---
Ni nini kinachoendelea nyuma ya pazia la "muujiza"? Nyuma ya Kanisa la Light of the Chosen?
Usikose chuma hiki....
Tutaanza Chungu cha 01, Muda sio mrefu.
Nitahitaji uvumilivu wenu, pia maoni yenu.
Karibuni....!