Lakini utunzi wako unagusa watu walio katika janga. Mtu anafungua anaanza kusoma akiamini atapata taarifa ya kumsaidia nyakati hizi za hofu. Sasa anachokikuta akijumlisha na hisia zake, ungekuwa karibu angekuzaba kofi. Hadidhi nyingine zinaweza kuamsha hisia hasi dhidi yako kuendana na hali ya mtu.
Fikiria fundi ujenzi ambaye hana akiba ya fedha wala chakula. Amaanka asubuhi anakutana na habari zinazoashiria kuwa hataweza kufanya kazi angalau mwezi mmoja. Mke na watoto wanamwangalia. Mara anapata taarifa kuwa wanafunzi wamerudishwa nyumbani kwa mwezi mmoja.
Halafu anakutana na uzi huu akiamini una msaada. Anakuta stori. Vumilia tu mkuu. Watu wana mengi vichwani mwao.