Siku za karibuni mapigano yameanza tena DR Congo. Ni vita ambayo majeshi ya Nkunda yanapigana na majeshi ya Serikali.
Mawazo yangu mimi ni kwamba vita kama hizi zinazotokea Africa,kama kwa mfano vita hii,au vita ya Sudan,au matatizo ya LRA,Lords Resisatnce Army,au vita vya Darfur,au matatizo ya Somalia.
Hii ni hali ambayo waafrika wanakata tamaa kuhusu maendeleo ya Afrika. Wanadhani kwamba baada ya Wakoloni kuitawala Afirka kwa miaka 100,basi,Afrika imekwisha,haitainuka tena,siyo,leo,siyo kesho,siyo siku yoyote. Ndiyo maana watu wanapigana vita hizi.
Lakini kama Wakielimika,yanaweza kuwepo matumaini kuhusu Afirka. Mara nyingi huwa naisikiliza Wapo Radio,kuhusu matatizo ya Warenchoka na Wanchari,na watu wa Dar es Salaam kila wanaposikia kuhusu haya matatizo,huwa wanauliza,Hivi huko Tarime kuna matatizo gani kuhusu hao watu? Kila kukicha tunasikia kuna mtu amekatwa na panga? Lakini ukienda kule unaona mara moja matatizo ni nini. Watu hawajaelimika. Kuna matatizo,kwa mfano ya ushirikina,vifo vinavyosababishwa na ushirikina,na haya mambo utaona yanatokea katika majimbo ya nchi ambayo kiwango cha elimu kiko chini. Kwa hiyo tunahitaji kuwekeza zaidi katika elimu,rafiki zetu wa nchi za nje watusaide kuwekeza katika elimu. Kama watu wa Sumbawanga wataelimika kama watu wa Kilimanjaro,matatatizo ya ushirikina yatakwisha. Kwa sababu hatusikii mauaji haya yanatokea Kilimanjaro,au hata hapa Dar es Salaam.
Mara ya mwisho yalipotokea ni yule kijana Rama,nadhani anaitwa, alipokutwa anakula fuvu la mtoto aliyemuua. Lakini ile ilikuwa ni hali ambayo yule kijana kwanza alimtapeli Mama Gertrude Rwakatare,na akapata marafiki wengi,lakini baadaye,baada ya watu kusahau lile tukio,akatoka kufanya visa vingine,ili watu wamuone tena,wampe soda na maandazi.
Kwa hiyo nasema,tunahitaji waelimike Sumbawanga,siyo waelimike sawa na Amerika,ila waelimike kama Kilimanjaro,ili tuweze kuuondoa ushirikina.
Rais Kabila hawezi kusema kwamba hawezi kujadiliana na Nkunda. Lazima ajadiliane naye. Na,tusipeleke majeshi kule kwa sababu tu Rais Kabila hataki kujadiliana na Nkunda.
Isipokuwa kinachohitajika ni majadiano na mantiki. Kwamba lazima wajadilane na Nkunda kwa kutambua kwamba Nkunda analo Jeshi ambalo linaleta usumbufu kwa raia,lakini kwa mantiki,kwa kuelewa kwamba Nkunda ni muasi,fisadi,ambaye anafanya mambo ambayo ni kinyume cha sheria ,kwa kuanzisha vita.
Pia DR Congo,na Afirka yote,kuna matatizo makubwa ya afya,na vita kama hizi zinakwamisha juhudi ya kuyapiga vita magonjwa. Kwa Nkunda lazima aende kwenye majadiliano,lakini bila kuleta masharti mengi,kwa kuelewa kwamba yeye ni muasi.
Kwa maendeleo ya Afrika,hawa watu lazima waache vita,waelewe kwamba huu sio mwisho,Afrika itainuka tena kama tukifaulu kuziaacha hizi vita,kama tukiweza kuelewa ni kwa nini tunapaswa kuyaacha haya magomvi yetu. Kama hivi sasa Barak Obama amechaguliwa kuwa Rais wa Marekani,tuitumie fursa hii kuleta maendeleo Afrika,kwa kujaribu kupata wawekezaji na missaada zaidi kutoka nje. Tusichukulie kwamba Barak Obama amechaguliwa kwa bahati mbaya tu kuwa Rais wa Marekani,kwamba Waamerika walighafilika,isipokuwa tuitumie kwamba ndiyo nafasi yetu ya kuleta maendeleo Afrika.
Huu uwe wakati wa kuijenga African Union,siyo kwa haraka nyngi kama anavyopendekeza Gadafi,isipokuwa,baada ya miiaka 50,Afirka iwe na Rais mmoja. Tufanye mambo polepole,kama alivyopendekeza Thabo Mbeki. Tuijenge African Union polepole lakini tudhamirie kuijenga African Union yenye nguvu sana. Tuiejenge na kuikamilisha baada ya miaka 50. Yaani,sio watoto wetu,ila watoto wa watoto wetu. Sasa tuna matatizo mengi sana ya kutanzua ya afya na elimu. Kuna matatizo ya ufisadi. Tukiyatanzua haya matatizo,hata kwa kiasi,watu wataanza kufikiri,waafrika watanza kufikiri,na Afrika itaendelea,watu wataweza kujadili ni mabadiliko gani wanayotaka kuyaona katika mfumo wa Uchumi,ili kila mtu aweze kupata maendeleo.
Watu wa Sudan hata sijui kama tunaweza kuwaita Waafrika,kwa sababu hawasikilizi kitu chochote tunachowaambia.
Lakini ingekuwa bora kama International Criminal Court ingekaa kando,tupate nafasi ya kuyatanzua haya matatizo ya LRA,na Sudan,na matatizo ya Rwanda Genocide,kwa mfano,juzi Rose Kabuye,mkuu wa itfaki Rwanda, amekamatwa na polisi wa Ujerumani,siyo kwa vile wanawajali Waaafrika waliokufa kule,isipokuwa kwa ajili ya wale marubani Wafaransa waliokufa. Ni bora Waafrika waachiwe wayatanzue matatizo haya. Ingekuwa siyo matatizo ya ICC,Joseph Kone angekuwa tayari amesaini mkataba wa amani.
Kuna uhusiano mkubwa kati ya watu kukosa elimu na kufanya mabo mengi ya vituko. Matatizo ya Afrika siyo kama vile Adolf Hitler anawaamrisha Wajerumani kupigana vita. Wajerumani walikuwa ni watu wenye elimu. Hapa ni hali ambayo watu ambao hawana elimu wameamrishwa kufanya mauaji.
Jambo moja muhimu analopaswa kuambiwa Nkunda,ni kwamba kazi yake siyo kucjinja watu wasiokuwa na hatia ili kuilazimisha Serikali ya Kongo kuongea naye. Kamanda yeyote wa Jeshi,kama ameteka eneo lolote,lazima ahakikishe kwamba anadumisha usalama wa raia katika sehemu ambayo ipo katika milki yake.Ndivyo alivyokuwa anafanya Mao Zedong Jeshi Jekundu lilipokuwa linapigana na Guo Mitang au na Wajapani.