NI KWANINI WANAMTUKANA NA KUMSIFIA NYERERE HAPO HAPO?
Mkuu
Rev. Kishoka
Katika mjadala huu naomba nizungumzie mada yako kwa namna nyingine ambayo kwa kiasi fulani inafedhehesha
Siku hizi imekuwa ni kawaida kusikia watu wakiongelea '' Awamu' hii imejenga vituo vingi vya afya kuliko Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete kwa pamoja.
Ni hoja inayoonekana kuwa ''zungumzo' na imepangwa izungumzwe hivyo.
Wanozungumza hoja hii ni watu wenye ufahamu na weledi na hilo linaacha mwaswali kama wanafanya kwa kutojua au kwa kujua hasa tukizingatia weledi wa wengi wa wananchi wetu.
Ni upotoshaji uliokithiri usiozingatia takwimu wala mantiki unaolenga hadaa na si ukweli.
Rais mstaafu Mwinyi aliwahi kusema '' yeye hawezi kuvaa viatu vya Mwl Nyerere'' na akasema pia ''Kila zama na kitabu chake'' Maneno haya yana maana sana na sijui wanaoeneza uvumi wa vituo vya afya wanayakumbuka au kuyajua.
Niongelee zama za Nyerere ambaye kwa mtazamo wangu kauli za vituo vya afya ni kumtusi hadharani
Mwl akichukua madaraka ilikuwa zama yake na kitabu chake.
Mwl hakuwa katika nafasi yoyote ile inayolingana na waliomfuata, alianza kujenga msingi si kuezeka paa.
1. Idadi ya watu wakati wa Uhuru ilikuwa milioni 9. Alikuwa na Daktari wa tiba mwenye sifa hiyo mmoja.
Sijui kama alikuwa na Engineer zaidi ya wawil. Hakuwa na mwanasheria hadi kuazima mwanasheria mkuu kutoka nje.
Mwl hakuwa na watalaamu wa kada za kati na chini. Nchi ilikuwa haina vyanzo vya nishati kama mabwawa ya umeme.
Hatukuwa na mfumo wa kusambaza maji. Mwalimu hakuwa na viwanda zaidi ya mashine ndogo ndogo.
Hakuwa na chuo kikuu hata kimoja. Barabara hazipitiki wakati wa masika. Reli iliyokuwepo ni ya kati na kaskazini
Orodha ni ndefu na inaweza kujaza kurasa na kurasa ikionyesha changamoto alizoanza nazo Nyerere akiwa na watu milioni 9, Taifa changa lililopata uhuru.
Taifa lilihotaji kuwekwa pamoja ili kuwa na utangamano kuelekea maendeleo.
Watu hawajui kwamba Mwl aliteua hata madereva kuwa wakuu wa Wilaya achilia mbali taasisi nyingi.
Katika changamoto hizo Mw alikuwa aanze na ipi?Mwl aliyachukua mambo yote kwa pamoja hatua kwa hatua
2. Nyerere alikuta chanzo cha umeme cha Pangani, akajenga Nyumba ya Mungu na Kidatu ili tupate nishati ya uhakika
3. Mwalimu akaanzisha vyuo vya elimu ili kupata walimu wa kuliemisha taifa. Mtakumbuka Ngumbaru ili at least watu waweze hata kuandika majina yao.
4. Mwalimu akajenga vyuo vya chini vya afya (RMA), Medical assistant, Assistant medical office (AMO)
5. Mwl akajenga vyuo vya chini na kati vya kilimo na ufundi
6. Mwl akajenga chuo kikuu cha kwanza nchini kilichotoa viongozi wengi sana wakiwemo wa Tanzania ya leo
7. Akajenga barabara kuu za lami kama Segera-Chalinze ili kurahisha usafiri
8. Ni Nyerere peke yake aliyejenga reli hadi leo(TAZARA). Hizi zinzokarabatiwa hazijengwi upya
9. Alijenga reli ya Mruazi-Ruvu kurahisha mawasiliano ya reli nchini
10 Akajenga viwanda watu walikwenda ''shift' kama nchi zilizoendelea si kukaa Bar ikifika saa 10 Jioni kama leo
11.Mwalimu akajenga Hospitali ya rufaa na kutafuta watalaam
12. Akajenga vyuo vya ulinzi na usalama kama Monduli n.k.
13. Mwalimu alitoa elimu bure hadi kulipia wanafunzi nauli. Hiyo ndiyo elimu bure aliyotoa Mwl
14. Mipango ya usambazaji maji ilikuwa inaendelea kote nchini( Someni mipango ya maendeleo 1963, 1967 n.k.)
Orodha inaendelea na hayo hapo juu ni kwa ujumla wake tu. Tukianza kuchambua kwa undani orodha itapanuka sana
Yote haya Mwl aliyafanya katika mazingira magumu sana, akiwa na watu milioni 9, watalaam 0
Laiti Mwl asingejenga reli ya Tanga au Tazara akaelekeza nguvu katika vituo vya afya basi tungekuwa na vituo vya afya kila nyumba 10.
Lakini Mwl alikuwa anawaza, je, ajenge vituo vya afya bila watalaamu na vifaa ?
Zama zake vituo vya afya vilikuwa na magari kwa ajili ya referal ikibidi. Je, ndiyo hali iliyopo leo?
Lakini pia lazima tuangalie mambo kwa kutumia akili.
Hivi wakati wa population ya milioni 9 kulikuwa na sababu ya kuwa na vituo vya afya 300 kama leo tukiwa na 55 milioni? Rationale ya kwamba alijenga vituo vya afya vichache inatoka wapi?
Vituo vya afya havijengwi tu kwasababu ya ku score political point, vinajengwa kutokana na mahitaji.
Hitaji la vituo mwaka 1961 ni tofauti na 1970 au 1980 au 2000 au 2019 kutokana na ongezeko la watu.
Hoja kwamba Nyerere hakujenga vituo kama leo ni tusi. Watanzania wanaomuenzi Mwl kwa dhati wakemee tusi hili.
Kazi ya Mwl Nyerere ilikuwa ngumu na nzuri bila kupepesa. Kumlinganisha Mwl na kiongozi mwingine ni kumtukana
Tena Mwl akawa ''Bold and Daring'' kwa kutaifisha Hospitali za watu na shule ili kujenga Taifa la pamoja na kuondoa matabaka. Leo hatuoni kazi hiyo. Mwl hakuwa na resource za kutosha akachukua maamuzi magumu kabisa.
Nyerere alikuwa bold and daring kwa kila kigezo. Nchi hii ilipotoka na ilipo leo si vitu vya kulinganisha hata kidogo.
Kinachosikitisha wanaomtukana Mwl Nyerere kwa vituo vy fya kama ilivyo leo bila mantiki ni hao hao wanaomsifia pale wanapotaka kuungwa mkono.
Tuache kumtukana Mwl Nyerere kwa hoja laini zisizo na mashiko za vituo vya afya.
Kazi ya Mwl ilikuwa kubwa, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Acheni kabisa kulinganisha kazi za Mwl, mnamtusi
Tukianza kuweka kazi za viongozi katika mizani. tutaishia kudhalilishana bila sababu.
Anayedhani kuwa ni wakati wa kumweka Mwl katika mizani na kiongozi mwingie tafadhali aje hapa tuongee!!!