The dark side of business

The dark side of business

Tanzanian Dream

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2024
Posts
274
Reaction score
1,771
Hakuna shule hakuna chuo utafundishwa kuhusu dark side of anything,Kuna njia mbili tu za kujua wasichokijua watu wengi,njia nyepesi zaidi ni kujua kupitia shuhuda za watu waliopita kwenye kivuli cha mauti na wakatoka salama na njia ngumu zaidi ndio Kama niliyopitia Mimi,i dip my feet into the ways of darkness.

Angalizo
Hiki ninachoandika ni experience ya miaka mingi nyuma, now mimi ni mtu safi,i believe in G-d na kwa kila nnachofanya i pray for his guidance.

Lengo la uzi
Nataka ujue upande wa pili wa shilingi,the dark side of business,uujue ulimwengu wa kiroho wa Biashara kwasababu huko ndio karata zinachezwa huko ndio kete zinasukumwa,sitaki upite dark side nataka upite light side(G-d side) kwasababu mafanikio bila giza yanawezekana.

This is my story
Nikiwa advance kwenye mkoa mmojawapo wa kanda ya ziwa,hapo shule nilipangwa room moja na machalii wawili kutoka A town na Kama unavyojua spirit ya wachaga wengi ni Biashara so ikawa story nyingi ni kuhusu biashara,chalii mmoja(tumwite fabi)ndio alikuwa moto sana na issue za biashara,kwasbb baba yake alikuwa mfanyabiashara mkubwa sana huko chuga,so jamaa alitamani kuvaa viatu vya baba yake.
Mzee wa fabi alikuwa ana hardware mbili kubwa town na nyumba za kutosha,alikuwa ni realestate guru,simply huyu mzee alikuwa tajiri,Kuna likizo tulienda chuga ili nipate mawili matatu kuhusu biashara.

Mzee fabi:ahaa wewe ndio rafiki yake fabi
Mm:ndio mzee,
Fabi:huyu ndio yule rafiki yangu niliyekuambia anapenda kufanya biashara
Mzee fabi:sawa,karibu sana kijana ila someni hizi Biashara mtazikuta tu,sisi hatukusoma lkn hesabu za Biashara tunazijua...(wote tukacheka)then mzee akaondoka akaenda kwenye mishe zake.
siku iliyofuata fabi alinizungusha kwenye miradi ya mzee,alikuwa na lodge 3,semi mbili na nyumba za wapangaji za kutosha,I was amazed!nikasema hakika business is a sure way onto riches,nilitamani nianze mishe za biashara hata kabla sijamaliza shule,kichwa iliwaka moto,baada ya likizo tulirudi shule nikiwa na vibe la kutosha.

Tukiwa shule
Tukawa tunaulizana tukimaliza shule tufanye issue gani!,fabi akawa anasema akimaliza anataka kuuza vocha za jumla(vocha za mitandao ya simu)mimi nikawa nasema nataka kuuza mafuta(dealer wa hizi cooking oil) so siku moja tukaenda town(shule yetu ilikuwa porini,ndani ndani) lengo la kwenda town ilikuwa ni kufanya utafiti wa hizo mishe tulizoplan kuzifanya,hapa nieleze ujanja flani aliotufundisha mzee wake fabi"ukitaka upate wazo zuri la Biashara angalia customer Queueing" akimaanisha angalia biashara inayotengeneza foleni ya wateja,isee huyu mzee hajasoma lkn alikuwa na nondo Kama za rich dady😃
Sasa huwezi kuamini tulizura pale town kucheki hizo mishe Kama zinatengeneza foleni ya wateja,kwanza tuliona maduka mengi yanayofanya mishe hizo ni ya wahindi(huko mbele nitakuja kueleza dark side ya hawa jamaa hapa bongo,Wana hadi kitabu maalumu cha namna ya kumpiga pin mtu mweusi awe Kama working machine)hawa jamaa kwa sehemu wametuzidi kete(kete za kiroho)....maduka mengi makubwa yalikuwa yao na kweli ile mishe ya vocha tuliona ina foleni si ya kitoto hadi na mm nikashawishika ku abort mishe ya mafuta!niingie kwny vocha.
*****************************

Wadau itabidi nigusie issue muhimu tu ili gazeti lisiwe refu,Sasa nini kitajiri baada ya kumaliza six na kuingia rasmi mtaani..........nitarudi
***************************

EPISODE 2
Inaendelea.................

Kuna uzi wangu niliutupia hapa unasema"experience ya miaka 15 ya kijiajiri(nadiriki kusema business is a sure way onto true riches)"kwenye huo uzi sikuelezea hiyo miaka 15 nilikuwa nafanya mishe gani, simply ilikuwa ni mishe ya vocha(wholesale)

Sasa baada ya kumaliza six,nilirudi mtaani na harakati za biashara zikaanza rasmi,kuna biashara ndogo nilianzisha lkn mawazo yangu yalikuwa ni mishe ya vocha za jumla, sema mtaji ulikuwa kipengele,so nikavutavuta siku mpk naingia chuo,ile biashara mdogo ilienda poa kimtindo,kuna dogo nilikuwa namwacha shop,mm naendelea na kitabu,nikapata boom(kwny intake yetu tulichelewa kupata,so tukapewa lumpsum ya mwaka mzima ilikuwa Kama 2.4M),chap nikaigeuza kuwa mtaji wa Biashara ya ndoto zangu,hii biashara ya vocha ni kama Biashara ya mafuta,faida yake ni ndogo sana lkn ukiuza mzigo mkubwa faida unaiona,kipindi hicho hii mishe ilikuwa 🔥 🔥 ila now days ni ya kawaida sana,kuuza mzigo wa milioni 5 kwa siku ilikuwa ni jambo la kawaida,nilichanganya shule na biashara kwasababu sikuwa na gutts tena za kusubiri mpk nimalize.
Chuo kilipoisha,
Kwa kweli sikuwa hata na chembe ya kutafuta ajira ijapokuwa matokeo yalikuwa mazuri,washkaji niliomaliza nao walikimbilia ajira,mimi nikaingia rasmi kwenye biashara ya vocha za jumla, wakati namaliza chuo mtaji ulikuwa kama 3M hv lkn ndani ya miezi sita mtaji ukafika 10M miezi sita mingine ikafika 20M,kwa waliofanya mishe hii backdays wanajua kama ukiuza mzigo wa milioni basi faida ni elfu 20,nilikuwa nauza mpk 8M kwa siku,kukunja laki hadi laki na nusu perday ilikuwa kawaida,dat time nikanunua kiwanja,nikajenga maflemu kama nane,then kwa nyuma niliplan kujenga apartments za kupangisha,nilinunua hiace(daladala)ili nitanue wigo,it was amazingl!coz I was just 23,nikazidi kusema "business is a quickest way onto riches" ila sikujua kuwa business is also a riskiest way onto riches,kwa ufupi ile side A ya biashara niliimaster ipasavyo,nilipiga kazi sana mpk watu wakahisi natumia ndumba,kwasababu ofisini watu walikuwa wanajaa,foleni kama nmb,hakika biashara na maisha kwa ujumla viliniendea poa,mtaani kila mtu alitamani afanye biashara kwakile alichokiona kinatokea kwangu,nilitengeneza jina kwa muda mfupi sana ghafla yakaanza mapicha picha,mara nikute damu kwny kiti ninachokalia pale ofisini,Mara hirizi,pesa zikawa zinapotea kimazingara,hua siamini uchawi lkn hiki kilichokuwa kinatokea ni uchawi bila chenga,nilifukuza wafanyakazi lkn haikusaidia(nilihisi wananipiga)nilipiga moyo konde lkn changamoto zilizidi to the extent nikaanza kuogopa biashara,kwa kweli nilibaki njia panda,ila Kuna wazo likanijia,juu ya nini cha kufanya......................
*****************************
Biashara zina ups and downs,niliona upande mmoja,sasa dunia inanionyesha upande wa pili,nini kitaendelea baada ya kupata wazo..........usikose

EPISODE 3
Tuendelee

Mawazo ya kuhisi nalogwa yalitawala kichwani mwangu na ni kawaida ya mbongo kuwaza hivyo,nilipata wazo la kumtafuta mzee wake fabi,nimwelezee hii changamoto ya pesa kupotea kimazingara,nasema kimazingara kwasababu nilifukuza wafanyakazi nikabaki mwenyewe lkn kila nikipiga hesabu mtaji unakata tu,hata ungekuwa wewe ungehisi kuna namna Kuna mchezo unachezewa,ikabidi nimtafute mzee fabi,yeye ni mzoefu kwny biashara na mambo kama hayo itakuwa amepitia.
Mm:habari mzee wangu za siku.
Mzee fabi:salama,nani mwenzangu
Mm:ni Mimi,rafiki yake na fabi(nikajieleza mzee akanikumbuka,nikamweleza changamoto ninayopitia)
Mzee fabi:kijana mambo hayo Ni kawaida sana kwenye biashara,kwani fedha zako hapo dukani hua unaziweka kwenye nini?
Mm:naziweka kwenye draw
Mzee fabi:usiweke fedha kwenye draw ya mbao,nenda mjini kanunue safe.
Mm:mzee ninapitia changamoto za fedha kupotea kimazingara,hiyo safe itanisaidia kweli?(niliuliza kwa mshangao)
Mzee fabi(huku akicheka):kijana nimefanya biashara zaidi ya miaka 30,ninajua mengi,fanya nilichokuambia..
Kwa kweli sikutaka kuuliza sana nikaonekana ni much know,nikashindwa kusaidika.

Nilienda town,nikanunua safe ya kilo 50 nikaanza kuweka fedha zangu humo na u can't believe,sikupoteza tena fedha baada ya kufanyahivyo.

Nilijaribu kutafuta uhusiano wa kupoteza fedha na kuziweka kwny safe then hazipotei,sikupata jibu,kumuuliza mzee nilishindwa,niliogopa kumkera kwa maswali,hii kitu mpk leo bado inanifikirisha,nilijaribu ku Google walau nitaambulia chochote,sikupata kitu,nikajua Kuna elimu nyingine zimefichwa ni wachache wanajua,wadau tupo hapa kujifunza sijui kila kitu so kama kuna mdau hapa jf anajua atumegee kuhusu hiyo elimu,inakuaje uchawi ushindwe kupenya kwny safe?hii ni sayansi ya namna gani?
In short hii changamoto iliisha kiihivyo,nikaendelae na business zangu Kama kawaida,lakini baadaye kidogo ikaibuka changamoto nyingine iliyonitikisa kibiashara..................
*****************************
Nilichojifunza kwa mzee fabi ni kwamba kupata changamoto kwny biashara ni kawaida ila tatizo ni namna unavyozitatua,hebu tuone changamoto ya safari hii nitatoka vp..........let's keep diving

EPISODE 4
Ilipoishia..........
Ile changamoto ya kupoteza fedha iliisha kiivyo nikaendelea na business zangu Kama kawaida,lkn baadaye kidogo iliibuka changamoto nyingine Tena,iliyonitikisa kibiashara........

Sasa tuendelee
Baaba ya mzee fabi kunipa ujanja wa kuweka hela kwenye safe,nilijiona mshindi,Kuna siku ambayo sitakuja kuisahau,siku hiyo nafika dukani simkuti mlinzi,mimi hua nawahi sana kufika ili nionane kwanza na mlinzi ndio mambo mengine yaendelee,sasa siku hiyo sijamkuta,piga simu hapatikani,nikaenda dukani nakuta geti imerudishiwa tu,kuingia ndani naona paa imevunjwa,nikajua jamaa wameingia,isee mapigo ya moyo yalienda mbio,akili ikanijia nicheki ile safe, nayo haipo😭jamaa wameibeba kabisa,dah!hapo ndio nikajua sijui,kwenye ile safe kulikuwa na zaidi ya 10M,hiyo ilikuwa my saddest day tangu nianze biashara,nilitetemeka all the day,nilitafuta yule mlinzi bila mafanikio,hiyo kazi nikawaachia polisi,mpaka leo hajaonekana,sitamsahau yule mzee alinifanyia umafia wa kiwango cha kasusura!wadau sijui nisemeje ila kuna wakati unaweza kujiona the luckiest guy in the world and within a minute ukajiona the most cursed person in the world,ile daladala nayo ilipata ajali(nilikuja kuiuza kwa hasara kama screpa)it was sad time,nilitafuta ushauri kwa watu sikupata msaada wa maana na wengi walinishauri niende kwa wataalamu nikasafishe nyota,niondoe mikosi,nikawapuuza,nilipata wazo la kumtafuta mzee wake fabi lkn nilijishtukia ikabidi nimtafute kwanza fabi(fabi baada ya kumaliza six,mzee wake alimpeleka kwenda kusoma nje,lkn kipindi hicho alikuwa ameshamaliza yupo chuga kusimamia buss za mzee wake)
Mm:habari fab,za kitambo hiyo,mishe vp?
Fabi:isee mambo safi chalii yangu,niko chuga,nasimamia biashara za mzee,vp ww,upo kwny ajira au umejiajiri?
Mm:nimejiajiri,ajira zinachelewesha kaka(tukacheka then mazungumzo yakaendelea)
Nilimweleza fabi changamoto ninazopitia,so akaniambia usijali,we njoo chuga tutayajenga.

Chuga town
niliingia chuga,mida ya saa mbili usiku,fabi akaniambia nimemweleza mzee wangu changamoto unazopitia,amehaidi atakusaidia,nilifurahi sana,siku hiyo mzee fabi hakuwepo(kila siku ya ijumaa halali nyumbani,analala ofisini) akaingia asubuhi

Mzee fabi:vp kijana mbona umepungua sana?
Mm:kawaida tu mzee wangu si unajua vijana ni kupambana
Nikaendelaea kusema"pole na kazi maana niliambiwa umelala ofisini.
Mzee fabi:yah,wakati mwingine kazi zinakuwa nyingi huna budi kulala ofisini,anyway kuhusu suala lako,tutakwenda baadaye kuzungumzia ofisini.

Huyu mzee kwny duka lake moja la hardware ni jengo la ghorofa moja kwa juu ndio ameweka ofisi yake.
Nikafika ofisini kwake,yeye akaelekea dukani,mm akanipa funguo nitangulie ofisini,nikaingia ndani,nikaona kuna shelfu kubwa imejaa vitabu,kwa ukutani Kuna picha kubwa ya triangle ndani ya kiooa,nikiwa nashangaa shangaa,mzee akaingia akaniambia hivyo vitabu vyote nimevisoma,najua vitu vingi kuliko ww ijapokuwa sikusoma kama ninyi akimaanisha(mm n fabi)akaendelea kusema"elimu ya maisha haifundishwi shuleni,ipo katika kusoma vitabu"narudia tena kusema,huyu mzee alikuwa na nondo sio za nchi hii,ameniachia hazina kubwa sana kwny akili yangu,mzee aliongea mengi lkn alinisisitiza niielewe biashara kiroho la sivyo nitakuwa napiga double march time,sikuwa nimemwelewa hasa alimaanisha nn kuhusu kusoma vitabu na hasa alimaanisha vitabu gani,maana Mimi pia ni msomaji mzuri wa vitabu,nilikuwa na maswali mengi ya kumuuliza sema sikutaka kumchimba sana,mzee akainuka kwenye kiti akaenda kwenye shelfu akachomoa kitabu kimoja,akasema nenda kasome hicho,akanipa nauli na 2M ya kuboost mtaji,kwa maana niliyumba vibaya,nikamshukuru sana mzee,then nikarudi zangu,kuendelea na haso.
*****************************

Hiko kitabu kimebeba Siri gani....tunaelekea patamu,hii si ya kukosa...............

EPISODE 5
Ilipoishia

Baada ya mzee fabi kunipa kitabu, nilirudi kuendelea na haso zangu Kama kawaida,hiko kitabu kimebeba Siri gani...........

Tuendelee Sasa
Nilisoma kile kitabu Kama nakunywa maji,kilielezea zaidi kuhusu ulimwengu wa kiroho kwenye masuala ya biashara na maendeleo ya sayansi na technolojia,kilieleza nguvu ya technologia dhidi ya uchawi,M-ngu alileta tech ili kuondoa uchawi,hii ni mada ndefu ningeweza hata kuiandikia uzi lakini itoshe kusema Kuna Siri kubwa sana nyuma ya tech,kitu ambacho kilinivutia zaidi kwny kile kitabu ni issue ya mitaji"yaani kutengeneza na kulinda mtaji"kwenye ulimwengu wa roho mtaji una matter zaidi kuliko faida,ndio maana maguru wanasema"the rule number one,don't lose money,'kupoteza hela ya mtaji kwa njia yoyote ile ni ishara ya kutokuwa na ulinzi rohoni,issue ya mitaji ni complex sana ndio maana huku mitaani,kilio cha sina mtaji ni kikubwa,mara mtaji umekata mara mtu amefilisika,hii issue ya mitaji kwa mbongo ni kipengele,kuna watu wana million dollar ideas ila tatizo ni mtaji.
Humo ndani wamegusia concept ya capital dimensions,yaani viwango vya mitaji na ulinzi wa kiroho,alitoa mfano wa bank,ni kwann?wachawi wasiende kuchota hela benki?zimeandikwa sababu kubwa tatu
1)bank zina ulinzi mkali kiroho,(ni dark au light wamiliki ndio wanajua),
2)bank zinatumia technology kupanga hesabu zao(technolojia ina nguvu kiliko uchawi)
3)bank wanahifadhi fedha zao kwenye strong room ya chuma(Kuna mdau aligusia hii issue,huu sio uchawi ni kanuni ya kiroho)

Hizo dimensions ni kama mstari umechorwa kwamba aina flani ya mfanyabiashara asiweze kuvuka kiwango flani cha mtaji,kwenye hicho kitabu waliongelea dimensions 3,ya kwanza ni milioni moja(kwa kifupi tuseme 1M)ya pili 10M na ya tatu ni 100M,yaani mtaji wako ukiwa chini ya milioni moja basi utapata shida sana kuivuka hiyo 1M na Kama ukivuka vita nyingine ni kwny 10M,hapo kuvuka ni kipengele na ukiona mfanyabiashara amevuka mtaji wa milioni 100,huyo rohoni sio mwenzako,kuna dimensions huwezi kuzivuka if you know nothing about spirituality,yaani ni lazima awe nondo sana either darkside au light side nje ya hapo utakuwa unapiga double march time.

Nilimaliza kusoma kile kitabu cha "The dark path"kilichoandikwa na mganda ambaye alikuwa tajiri baadaye alianguka vibaya but later on alirudi juu tena,ameandika mambo aliyopitia na namna alivyo rise to the top again,hicho kitabu kwa sehemu kilinisaidia kujua abc za upande wa pili,na nikajiona sina ulinzi wowote wa maana kiroho,na mfanyabiashara makini ni lazima ujikoki kisawasawa la sivyo wajanja watakuzidi kete.

Turudi nyuma kidogo
kuna mzee mmoja ambaye tulifahamiana siku za nyuma,huyu mzee alikuwa ni fundi wa seat cover za magari,yeye ndiye aliniwekea cover kwny ile hiace yangu,so tulifahamiana kwa njia hiyo.
yule mzee(tumwite mzee sudi) alijenga ukaribu flani na mimi,kwasababu aliniona bwn mdogo harafu namiliki gari ya biashara,so akawa ananifungukia mambo mengi ya gizani(alidhani na mm nitakuwa konki wa hizo kitu) mzee sudi aliwahi kufanya kazi kwenye kampuni za mabasi ya wahindi zaidi ya miaka 20,niliijua dark side ya hao jamaa pitia huyu mzee,akawa ananifungukia mambo mengi sana..
,"Pale kazini ilikuwa kila alhamisi wanachinja mbuzi 20 na damu inamwagwa kuzunguka eneo lote na kila mwaka lazima mfanyakazi afe(hii kwa mtu wa kawaida ni ngumu kujua mpk uwe na spiritual intelligence kama za mzee sudi)
Jamaa walikuwa wanatoa kafara,wafanyakazi,abiria mpaka watu baki ilimradi damu imwagike biashara zao ziende,mtu akifa tu huyo mmiliki wa mabasi anaongeza basi zingine,"nimewafanyia kazi zaidi ya miaka 20 Sina cha maana nilichopata na Kama ningekuwa sijajikoki wangenitoa kafara( aliongea mzee sudi kwa uchungu)
Huyu mzee ndio alinionyesha kitabu wanachokitumia kujitajirisha kupitia jasho,damu na nafsi ya mtu mweusi,wana kunyonya jasho lako,wanakuibia nyota yako then lastly wanakutoa kafara,they are building wealth upon our sweats&bloods.

Zile story za mzee sudi ziliniogopesha Sana kuhusu biashara na hasa hizi za vyombo vya usafiri,yaani bila kupuliza mambo hayaendi😜,huyu mzee alinipa namba za mtaalamu wake aliyemsaidia tangu kipindi yuko kwa mhindi,nilisave namba zake lkn sikuwa na mpango wa kumtafuta,kwasbb mpk muda huo sikuwa naamini Katika ushirikina.

Turudi sasa kwny kile kitabu
Kuna mahali ameandika "kuwa tajiri ni rahisi,kigumu ni kuulinda utajiri wako,matajiri wana siri kubwa sana namna wanalinda utajiri wao,hiki kitabu kilinifanya nijione niko naked kiroho,sasa baada ya kumaliza kusoma,sikutaka kumsumbua mzee fabi,kwasababu msaada alioutoa kwangu ni mkubwa,nikaona nijiongeze kivyangu.
Nikachukua simu nikamtafuta mtaalamu wa mzee sudi,nilichokuwa nakitafuta mimi ni ulinzi sio utajiri,njia za utajiri nilisha zi master ila kwny suala la protection ya kiroho nilikuwa empty.

Nilifika kwa mtalaamu,asubuhi na mapema,hapo kwake nilikuta nyomi ya watu,kila mtu na changamoto yake,nikakaa foleni Kama masaa mawili hv,ilipofika zamu yangu nikaitwa nikazama ndani.............

Kwa mara ya kwanza naanza kulisogelea giza...................

EPISODE 6
Inaendelea......

Nilizama ndani,nikamkuta mbaba wa makamo around 50s,huyu mtaalamu alijulikana kwa jina moja la "ngurumo"
"Karibu kijana,usiogope,umefika kwangu shida yako imekwisha"(aliongea mzee ngurumo kwa kujitapa)
Mm:nimeskia habari zako,nikasema nije nikuone,huenda ukanisaidia(nikamwelezea changamoto nilizopitia na nini nahitaji kutoka kwake)
Ngurumo:nimesaidia wafanyabiashara wengi sana,hiyo issue yako ni ndogo,akaniambia weka elfu 50 hapo kwenye kikapu,baada ya kuweka aliniambia nenda urudi usiku saa mbili,uje na njiwa.

Niliondoka,saa mbili juu ya alama nikawa nimefika
Ngurumo:kijana umekuja na yule njiwa
Mm:ndio huyu hapa
Ngurumo:sasa ngoja nimpigie dereva atupeleke lango la bahari
Ilifika saa tatu ndio dereva akaja,tukaondoka

Tukiwa njiani
Ngurumo akaniuliza yule njiwa yuko wapi?muda wote nilikuwa nimemshika lakini saa hiyo sikumwona
"Hebu simamisha gari"aliongea ngurumo kwa jazba!dereva akaweka gari pembeni,tukaanza kutafuta mule ndani ya gari hakuonekana!
Ngurumo:kijana inaonekana vita yako ni kubwa sana,nilikuwa nakuchukulia kawaida lkn naanza kuona mambo mazito(ngurumo alianza kuingiwa na wasiwasi)
Hali Kama hii haijawahi kunitokea,leo kuna nini?(mzee ngurumo alijiuliza mwenyewe,)tulipoteza Kama nusu saa pale,gafla tusikia Kama njiwa anapiga mabawa chini ya gari,kucheki kumbe yuko chini ya gari,tulijiuliza alitokaye hakuna aliyekuwa na majibu
Safari iliendelea.......
Huko lango la bahari ni mbali,tulitembea na gari kwa saa moja na nusu,hatimaye tukafika.
Hapo lango la bahari pana beach moja kubwa(sitaitaja) hapo beach Kuna harakati za kawaida zinaendelea,tukavuta siti takawa tunavuta pumzi ili tuingie baharini,mida Kama ya saa tano na nusu usiku,tukasogea baharini,nikabadili nguo nikavaa nguo za kazi,nikaanza kupiga hatua kuelekea baharini,wakati huo ngurumo yuko ufukweni,ananiambia kijana nenda,usigeuke nyuma,wewe nenda tu.. usiogope..dah usiku bahari inatisha,mkononi nilikuwa nimeshika coins,lengo la ngurumo kunileta huku bahari ni kuni connect na miungu ya pesa..
"Rusha hizo hela kwa nguvu huku ukisema,eeh miungu ya baharini nipeni utajiri,nipeni ulinzi"wakati natamka hayo maneno ghafla bahari ilifunuka mbele yangu,mzee ngurumo akasema usiogope,maombi yako yamepokelewa,rusha hizo hela haraka...nilizirusha fasta...akaniambia rudi kinyume nyume,kazi imekwisha,mapigo ya moyo yalinienda mbio sana,moyoni nikasema hakika njia ya utajiri ni ngumu ila kwa kuwa nimeshapiga one step ahead,ngoja nikomae nione mwisho utakuwaje!....tulirudi kwenye gari fasta,hatukuwa na muda wa kupoteza.....
Mzee ngurumo akaniambia bado issue moja tunaenda kuimalizia usiogope huu ndio uanaume...........
*******************"*********
Nilijua mambo yamekwisha kumbe picha ndio linaanza!hapo ilikuwa inakimbilia saa saba usiku,mzee ngurumo akamwambia dereva kimbiza gari tumebakiwa na nusu saa tu...........nini kitajiri...

EPISODE 7
Inaendelea

Ilipoishia..............
Baada ya kutoka lango la bahari,
tulirudi kwenye gari fasta,hatukuwa na muda wa kupoteza.....
Mzee ngurumo akaniambia bado issue moja tunaenda kuimalizia usiogope huu ndio uanaume......

...........ilikuwa inakimbilia saa saba usiku,mzee ngurumo akamwambia dereva kimbiza gari tumebakiwa na nusu saa tu...........

sasa tuendelee

Dereva alikimbiza gari na hatimaye tukafika eneo la tukio,baada ya kupark,tukashuka,hilo eneo lilikuwa na giza,hakuna nyumba wala hakuna mtu anapita.
Ngurumo:akiwa ameshika begi mkononi,akamwambia dereva wewe baki hapa,tusubiri...akanigeukia akaniambia kijana usiogope,akafungua begi akatoa nguo nyeusi,akaniambia chukua hiyo uvae,ile nguo ilikua kama kanzu nyeusi,nikaivaa juu ya nguo zangu na yeye pia akavaa kanzu yake,hizi nguo zina funika mpk kichwa na zilikuwa nzito Kama ovalori,kama ulishawahi kuiona ile movie ya kanumba''devil kingdom",Kuna scene jamaa wamevaa maguo flani hv meusi,basi ndio tulifanania hivyo.

Ndani ya msitu mnene
Baada kumaliza kuvaa nikambeba yule njiwa na safari ya kuingia ndani ya msitu ikaanza,hapo inakimbilia saa nane za usiku.
Ngurumo akaanza kuniongelesha
Ngurumo:suala lako limekuwa na uzito flani sijui kwanini?lakini kila kitu kitakaa sawa Mimi ndio ngurumo..
Hapo Mimi niko kimya tu namsikiliza.
Ngurumo:0ngeza kasi kijana,saa nane inatakiwa tuwe tumefika..
Mm:kwani tunaelekea wapi?
Hakunijibu chochote ila baada ya muda kidogo...tukawa tumeshafika
Tulitokea kwenye eneo la makaburi,mzee ngurumo alitafuta kaburi mojawapo akaniambia njoo hapa juu ya kaburi,hatuna muda wa kupoteza, akaniambia,kinachokwenda kutokea naomba chonde chonde usimwambie mtu na uwe makini kusikiliza maelekezo nitakayo kupa,ukifanya kosa hata dogo utakwenda na maji kijana,uwe makini(alisisitiza mzee ngurumo)
tukapiga magoti then akaniambia mshike vizuri huyo njiwa,nilimshikilia kwa mikono miwili nikiwa nimepiga magoti pale juu ya kaburi,nikaanza kusikia ndani ya tumbo la yule njiwa Kuna Kama kitu kinatembea...ghafla yule njiwa alianza kuongea Kama binadamu....(mzee ngurumo akaniambia usiogope)so nilijikaza lkn mwili ulitetemeka,mikono ilikufa ganzi.
Yule njiwa alianza kucheka huku akiniita jina langu kwa kurudia rudia...
Ngurumo:anavyokuita itika,sema naam nakusikia
Njiwa:akaniita tena.
Mm:naam nakusikia
Njiwa:wewe ni mtu mkubwa Sana ndio maana vita yako ni kubwa lakini usijali mimi nitakusaidia(akaendelea kucheka)
Ngurumo:mwambie akusaidie
Mm:naomba unisaidie
Njiwa:nitakusaidia,nitakupa utajiri mwingi sana na ulinzi mkubwa,hakuna mtu ataweza kukusogelea...
Mm:nahitaji ulinzi na sio utajiri
(Nikawa namnong'oneza mzee ngurumo)
utapewa utajiri na ulinzi ni lazima ukubali vyote(alijibu ngurumo kwa ukali)..
Basi nikaona isiwe ligi nikakubali yaishe.....

Kwanini nilikuwa nakataa utajiri
nilikuwa najua nina uwezo wa kupambana na kutoboa bila ndumba na lengo langu lilikuwa ni kutengeneza utajiri utakaodumu vizazi na vizazi,nilijua mali za giza hua hazidumu,ukifa zinapukutika,so nikawa na defend point yangu"sitaki utajiri nataka ulinzi"but a devil was smarter than me,alinibana niukubali na utajiri wake...

Turudi kwa yule njiwa
Njiwa aliendelea kuongea
"Nitakufanya kuwa mtu mkubwa sana hapa Tanzania na utajiri wako utakuwa Kama wa...akataja matajiri wawili wa hapa bongo,yule njiwa alimalizia kwa kunitaka nimpe ng'ombe wawili,ili shughuli ya kunisaidia ianze mara moja...

Ngurumo:unao uwezo wa kutoa ng'ombe wawili?
Mm:ndio
Ngurumo:utawatoa lini
Mm:naomba mnipe wiki mbili
Ngurumo:wiki mbili ni nyingi,tunakupa wiki moja

Tulipomaliza maongezi,tulimchinja yule njiwa na kumwacha hukohuko makubiri,then Mimi na mzee ngurumo tukaondoka.....

Baada siku mbili,mzee ngurumo alinipandia hewani
Baada ya salamu mazungumzo yaliendelea
Ngurumo:hivi kijana hao ng'ombe unajua unawatoa vp
Mm:si naenda kuwanunua then nawaletea Kama nilivyofanya kwa yule njiwa?
Ngurumo:hapana,hao ng'ombe tunaenda kuwanunua kisha unakodi gari ya kuwabeba,njiani itatokea ajali,gari itapinduka na wale ng'ombe wakufa,tutatuma viumbe sita,watatu wa kike(kwa ajili ya mvuto) na watatu wa kiume(kwa ajili ya ulinzi) hao ndio watasababisha ajali na wale ng'ombe watanyonywa damu na hao viumbe na baada ya tukio hilo wale viumbe watakuwa ni mali yako,watakufata kila mahali na utawatuma popote unapotaka.............
****************************
Je hao viumbe ni akina nani? na je nitafanikiwa kuwatoa hao ng'ombe wawili....

EPISODE 8
inaendelea


Ilipoishia......
Ngurumo alinipa maelekezo ya namna ya kuwatoa wale ng'ombe na jinsi wale viumbe watakavyo sababisha ajali na baada ya hapo watakuwa ni mali yangu,watanifata kila mahali na nitakuwa na uwezo wa kuwatuma popote unapotaka.............
Je hao viumbe ni akina nani? na je nitafanikiwa kuwatoa hao ng'ombe.......

Sasa tuendelee
Baada ya ngurumo kunipa maelekezo ya namna ya kuwatoa wale ng'ombe,ilinifikirisha sana,akili yangu ilienda mbali kidogo,ikabidi nimuulize,

"Hiyo ajali ikitokea huyo dereva atanusurika?
Ngurumo:Kama ana kinga anaweza kupona lkn kama hana kinga ni lazima atakufa
"Hii iliniogopesha sana"
Mm:kwani hakuna njia nyingine?maana naona Kama tunaenda kuua mtu asiye na hatia!
Ngurumo:kijana mbona una huruma sana,utajiri utauweza?....hao ng'ombe hawatolewi kwa kuchinjwa,wanatolewa kwa ajali hakuna njia nyingine(alisisitiza mzee ngurumo)
Baadaye kidogo akaniambia wewe hofu yako ni dereva kufa,basi usijali,nitaangalia namna ya kumkinga lkn hiyo ni gharama nyingine,itabidi ulipie...

Ajali nyingi ni za mchongo
Mara nyingi ajali ikitokea tunaishia kumlaumu dereva lkn nyuma ya pazia,ajali nyingi ni platform ya kutolea kafara,ukipanda chombo chochote cha moto,iwe ni basi,meli,treni,ndege hata iwe bodaboda usidharau,fanya sala na ukishuka ushukuru....

Ile siku ikafika
Mzee ngurumo alinipeleka kwa mtu wake ambaye alikuwa ni mfugaji,kwa kuwa alikuwa tayari ameshampanga,tulimkuta anatusubiri
Ngurumo:unaona jinsi ng'ombe wake walivyo wakubwa,ndio maana nikakuleta huku.

Nililipa 1.6M,kila ng'ombe alinicost laki nane,dereva akaja,tukawapakia.

Safari ikaanza
Mimi na mzee ngurumo tulipanda pikipiki,tukatangulia mbele,jamaa anatufata kwa nyuma,moyoni niliwaza kile kinachokwenda kutokea......tulitembea Kama dk 15 hv, ngurumo akatoa kifuko mfukoni kilichokua na unga,tulipofika njia panda akamwaga ule unga na Kuna maneno akayasema...,ilitokea Lori hz tipper za mchanga iko moto vibaya ikaigonga ile canter ubavuni kwa nyuma,kwasababu ya speed ile canter ilienda chini,lile lori likaingia kwny mtaro.
Wakati huo sisi tumepark pikipiki tunaangalia ile ajali,nikawa nawaza kwa mzinga ule sidhani Kama Kuna mtu atatoka salama,nilianza kujiskia vibaya.......
Ngurumo:twende tukacheki Kama wale ng'ombe wamekufa au la!
Watu walikuwa wameshajaa eneo la tukio,mzee ngurumo alienda moja kwa moja kutazama ng'ombe,Mimi nilienda kucheki wale madereva,yule wa Lori alikuwa mzima amekaa chini,yule aliyebeba ng'ombe walimtoa kwny gari wamemlaza chini,dah!nikasema kimoyo moyo"huyu atakuwa ameshavuta.....
Ghafla mzee ngurumo akanishika begani,akaniambia kijana" deal done"(huku akitabasamu)
Mm:mbona sasa yule dereva amekufa?(nilimuuliza kwa huzuni)
Ngurumo:yule hajafa amezimia tu.
Tulifanya mchakato wa kuwapeleka hospitali na kweli yule bwn alikuwa hajafa.

Baadaye kidogo tulikodi gari nyingine,tukabeba wale ng'ombe,tukaenda kuwazika.

Ngurumo:Sasa kila kitu kipo sawa..naomba urudi nyumbani ikajiandae maana usiku wa leo(ilikuwa alhamisi)wale viumbe watakuja,ila naomba uzingatie haya masharti matatu 1),usimwambie mtu yoyote mambo haya 2)usimguse mwanamke kwa miezi sita na baada ya hapo itakubidi uoe maana zinaa na utajiri havipatani na 3)kila siku ya alhamisi usiku,utakuwa unachoma udi,dukani na nyumbani kwako(mzee ngurumo alimaliza kutoa maelekezo)
Haya masharti sikuyaona Kama yana ugumu wowote ila lile sharti la pili kwa sehemu niliona ni kipengele 😀

Nikarudi home
Nimefika home nimechoka,nikaweka mazingira vizuri kwa ajili ya ugeni wa vile viumbe,nikaingia gheto(bed room)nikachoma udi za kutosha,kwasababu harufu ilikuwa kali ikabidi nitoke nikalale sitting room,nilipitiwa na usingizi mzito,niliamshwa na mlio wa simu,kucheki nani ananipigia,kumbe ni mtu wangu wa dukani,nilimpa maelekezo wakati wa kufunga achome udi za kutosha,baada ya Kama nusu saa aka nitext"boss nimeshachoma na duka tumeshafunga"
Nikacheki saa,ni saa mbili na nusu usiku,ghafla nikaskia mlango unagongwa..........mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio,nikajisemea ndio wale viumbe wamekuja...nikawa najiuliza hivi viumbe zipoje,sura zao zipoje?nilijiuliza bila majibu....mlango ulizidi kugongwa....nilisogea pale mlangoni huku

natetemeka..........................
***************************

EPISODE 9
Inaendelea


Ilipoishia(nikiwa home)
Nikacheki saa,ni saa mbili na nusu usiku,ghafla nikaskia
mlango unagongwa..........mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio,nikajisemea ndio wale viumbe wamekuja...nikawa najiuliza hivi viumbe zipoje,sura zao zipoje?nilijiuliza bila majibu....mlango ulizidi kugongwa....nilisogea pale mlangoni huku natetemeka...................

Sasa tuendelee

Nilifungua ule mlango then nikarudi nyuma ili nione kitakacho ingia,aliingia recho!

(Huyu recho alikuwa ni girl friend wangu tangu niko chuo)

Recho:we mwanaume vp,nagonga mlango muda wote huo hufungui?(alihoji recho kwa ukali)

Mm:"punguza jazba,nilikuwa nimelala sikukuskia ulipokuwa unagonga!vp mbona umekuja bila taarifa?

Recho:haah!,yaani ww leo ni wa kuniuliza mimi hivyo,ama kweli umenichoka,kwanza wiki nzima hupatikani uko bize,dukani haupo,nyumbani haupo unakuwa wapi?

Mm:mbona unanifatilia ww mwanamke!kwahiyo ulikuja ili unifumanie?mbona huniamini?

Recho:ehee bora umejitekenya mwenyewe,kwanza hii harufu ninayoisikia humu ndani ni ya nini?utakuwa umeingiza mwanamke!(aliacha kuongea akaanza kuelekea chumbani)
Recho:tena huku ndio harufu inatokea,ngoja nimkute huyo mwanamke,patachimbika!....(alizama ndani,akapiga dolia lkn hakuona kitu)
Recho:hebu niambie hii harufu ni ya nini?
Mm:ni marashi tu ya kawaida mambo ya Oriental hayo,
recho:akaguna then akapotezea.....,tukaendelea kupiga story za hapa na pale.
Story zikanoga nikasahau kwamba nina ugeni....ghafla kuna text ikaingia kwny simu"kijana umeshafanya maandalizi?"ilikuwa ni text ya mzee ngurumo (akili zilinirudia) nilijiuliza hawa viumbe wakija na kunikuta na mwanamke,walahi sitaomba maji kwasababu sharti moja wapo ni kukaa mbali na hawa viumbe wa kike!

Mm:sasa baby,nikusindikize maana leo siko poa kabisa
Recho:sikua na mpango wa kuja kulala leo nilitaka nije tu nione Kama Kuna usalama.

Basi nilimsindikiza kisha nikarudi,nikaingia chumbani,nikawa nimekaa kitandani natafakari namna ya kumpiga chenga recho kwa miezi sita,na Kama mnavyojua mtoto wa kike,ukimletea ring show,ma baharia wanapita naye,kwa kweli sikuwa tayari kumpoteza recho,niliwaza labda nisafiri kwa hiyo miezi sita sikupata jibu,nilijilaza pale kitandani ila sikuwa hata na chembe y usingizi,masaa yalizidi kukatika.

Ikafika saa nne usiku
Nilisubiri wale viumbe,lkn hawakutokea,nilitegemea kusikia mlango unagongwa lkn wapi,mpk nikaanza kupitiwa na usingizi.

Baada ya dk Kama 20 nikashtuka,taa ya chumbani ilikuwa on lkn nashangaa kuona imezima,then mlango ukafunguka wenyewe bila kuguswa....nikawa nimekodolea macho pale mlangoni....ulitokea Kama mwangaza,kisha viliingia viumbe sita,wakike watatu na wakiume watatu,ile harufu ya udi ikatoweka ikaja harufu moja nzuri sana,ile hofu niliyokuwa nayo mwanzo ikapotea,niliinuka pale kitandani kwa ujasiri na kusimama mbele ya wale viumbe,mwanzoni nilijua watakuwa ni viumbe wa ajabu wenye sura mbaya,nilishangaa kuona ni warembo wa maana.

Wale viumbe waliongea kwa lugha ambayo sikuijua lkn nilikuwa nawaelewa na Mimi nikiongea kiswahili changu wananielewa...niliwauliza wametokea wapi? Kuna mmoja alikuwa kama ndio
Kiongozi wao,anaitwa bijan"tafasiri ya hili jina ni "shujaa"

Bijan:sisi ni wa Persian(aliongea bijan kwa kilugha Chao)...bijan aliendelea..
Tumetoka ulimwengu wa mbali,tumetoka kwenye ufalme wa kiajemi na tupo hapa kwa ajili yako.....bijani aliendea kuongea na baada ya muda kidogo aliita"yasamin" akaitika kiumbe mmoja wa kike(huyu yasamin ndio sisi kibongo tunamwita jasmine na maana yake ni zawadi kutoka kwa mungu,haya majina yao yalikuwa yana husiana na mishe iliyowaleta..kule mwanzo nilisema watatu walikuwa ni kwa ajili ya mvuto na watatu kwa ajili ya ulinzi)
Baada ya bijan kumwita yasamin,aliendelea kuongea,

Bijan:lete zawadi kutoka kwa mungu...(wadau hapa naandika mungu kwa herufi ndogo tena bila codes kwasababu huyo wanayemwita mungu sio huyu unayemjua wewe,huyo mungu wao anaitwa mkuu wa ufalme wa uajemi)

Jasmine alileta kijisanduku kidogo na akakifungua mbele yangu,kwa ndani kilikuwa na pete ya dhahabu..bijan akasema mvalishe hiyo Pete
Basi nikanyoosha kidole na Jasmin akanivalisha ile Pete....ghafla wale viumbe waliinama na kunisujudia na wote kwa pamoja wakisema sisi ni mali yako,wakawa wanarudia rudia kusema khuda...khuda...khuda,hili neno ni sawa na kusema bwana au Lord na tafasiri yake ni"mmiliki au owner"hili ni neno zito sana kwenye lugha ya kiajemi.

Vile viumbe kunisujudia nilijiona somebody in the realm of spirit,nikajiona mfalme.

Assignment
Usiku uleule nikaanza kutoa assignment kwa wale viumbe

Mm:bijan nahitaji upeleke walinzi pale dukani kwangu na wewe utakuwa unanilinda mimi....baada ya kusema hivyo wale viumbe wawili wa kiume walipotea kama upepo,within a second...bijani akaniambia wameshafika...
Na wale akina jasmine niliwaambia waende wasimame mbele ya duka langu ili kuvuta wateja,nao walipotea kama upepo kwa speed ya light....nikabaki na bijan
Mm:wewe kazi yako ni kunilinda Mimi,uta hakikisha hakuna nguvu ya giza inanipata na hakuna senti yangu hata moja inapotea..bijani aliitikia kwa kusema "khuda"kisha akendelea kusema..
Bijan:Kuna zawadi nyingine mkuu wa ufalme wa uajemi ataituma kwako,akiituma niite nikupe maelekezo.....

Baada ya maongezi ya muda mrefu.....
Niliachana na bijan,nikaenda zangu kulala na bijan akawa around ila haonekani(hawa viumbe pakikucha huwa siwezi kuwaona ila naweza kuongea nao)

Kesho yake
Nilienda dukani mapema sana,nikafungua geti nikazama ndani,nikaweka mazingira sawa,then nikafungua safe(baada ya ile safe ya kwanza kubebwa,nilinunua safe nyingine kubwa zaidi) ndani ya safe nikakuta hela zangu na mzigo wa vocha kama kawaida lakini niliona kuna hela zingine sio za kitanzania,nilishtuka kidogo lkn nikajiongeza itakuwa ndio ile zawadi aliyoniambia bijan kwamba mkuu wa ufalme wa uajemi atanitumia,nilizihesabu nikakuta zipo dinari 25,000,kipindi hicho ilikuwa 1KWD ni sawa na TSH 4500,zile dinari 25,000 ni sawa na milioni mia za kibongo na chenji zake..nilifurahi kama mwalimu aliyeongezewa mshahara😀😀
nilichukua zile hela,nikaenda nazo home niongee na bijan,kwasababu aliniambia nikipokea hiyo zawadi,nimuite anipe maelekezo.

Nikiwa njiani nilianza kuipigia hesabu hiyo hela,nikawaza nivute bmw 320i harafu kiasi kinachobaki nikamalizie kujenga apartments zangu.

nimefika home moja kwa moja nikaenda chumbani,nikaita bijan,bijan..

Bijan:ndio mkuu nakusikia(hapo bijan anaongea kwa kilugha chao,naskia sauti yeye haonekani,hawa viumbe hawapatani kabisa na mwanga sijui kwann)
Mim:isee ile zawadi uliyoniambia tayari imeshatumwa(huku namwonyesha bijan vibunda vya hela)
Bijan:hizo hela usifanyie chochote zaidi ya kuiwekeza kwenye biashara(bijan alisisitiza)
Ile ndoto yangu ya bmw ikayeyuka😭😭
Baada ya bijan kunipa maelekezo sikutaka kulaza damu,nikaenda kuongea na mmiliki wa zile fremu pale ninapofanyia biashara anipe go ahead ya kulipanua lile duka na kujenga store moja kubwa,yule mmiliki aliniewa akanipa go ahead..

Shughuli ya kupanua jengo la Biashara ikaanza

Mafundi walipiga kazi mchana na usiku kwasababu wakati upanuzi unaendelea tuliacha kutoa huduma,
Nilijenga duka na store moja kubwa ili nijitanue kibiashara,nililenga nifungue duka kubwa la jumla ambalo nitauza karibu kila kitu nilitaka nifanye kama Walmart.

Baada ya ile kazi kuisha,
Kesho yake,nilikuja na cater mbili zimejaa mzigo,canter ya kwanza tukapakua mzigo tukaujaza store na canter ya pili tukaweka mzigo dukani....hiki nilichokuwa nakifanya watu walikuwa hawaamini kinachotokea,kila mtu aliongea yake mara jamaa amerithi mara anatumia ndumba...nilipuuza maneno yao nikaendelea kufanya maajabu.

Nilipiga hesabu ule mchakato mzima mpaka unakamilika,nilitumia 87M,ukipiga hesabu bado hela ndefu imebaki.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa na kituo chake cha kuuza tofari,huyu jamaa alikuwa anapiga Sana kazi kipindi cha nyuma mpk yalipoanza mapicha picha,mara mashine haziwaki,Mara mota imeungua,wateja nao wakakata,so jamaa akatangaza kuuza kila kitu,nilimpa jamaa gharama zake zote lkn kabla sijaanza kazi team yangu ilienda kukagua kile kituo na kuweka mambo sawa,jamaa alikuwa anarogwa na mshindani wake ambaye yuko kwenye game kitambo,so team yangu ikiongozwa na bijan walifanikiwa kutegua uchawi wote then mwanaume nikaingia.

Nilishusha mende za mchanga,leta semi ya cement,vijana walipiga kazi asubuhi,mchana,usiku ilikuwa ni shift,hawa wakichoka wanaingia wengine.

Kule dukani walibaki viumbe watatu,wawili niliwapeleka kwenye kituo cha tofari,mmoja wa mvuto na mwingine wa ulinzi,
mambo yakawa juu ya mstari.

Baada ya miezi 3
Ngurumo alinitafuta
"Vipi kijana mambo yanaendeleaje?"
Mm:isee mambo ni 🔥🔥kuna zawadi nitakupa mzee wangu!
Ngurumo:sawa ila wewe endelea kufata masharti utafika mbali Sana....una nyota kali sana ya biashara lakini ni muhimu kujua wale ng'ombe wawili wanamaanisha nini?kisha akakata simu..
Niliitafakari hii kauli ya mzee ngurumo sikupata jibu.........
****************"************
nini kitajiri baada ya hii kauli tata ya mzee ngurumo!wale ng'ombe wanamaanisha nini?........Bar mighardam(kiajemi) yaani nitarudi

EPISODE 10
Ilipoishia...

Baada ya miezi 3
Ngurumo alinitafuta
"Vipi kijana mambo yanaendeleaje?"
Mm:isee mambo ni 🔥🔥kuna zawadi nitakupa mzee wangu!
Ngurumo:sawa ila wewe endelea kufata masharti utafika mbali Sana....una nyota kali sana ya biashara lakini ni muhimu kujua wale ng'ombe wawili wanamaanisha nini?kisha akakata simu..
Niliitafakari hii kauli ya mzee ngurumo sikupata jibu..........

Sasa tuendelee
Ile kauli ya ngurumo ilinipa kutafakari kwasababu huyu mzee akiongea kitu huwa anamaanisha(nilijiuliza mwenyewe,wale ng'ombe Wanamaanisha nini? Sikupata jibu.

Niliendelea na biashara kama kawaida,mtaji ulikua kwa kasi,kwasababu 70%ya faida niliirudishia kwenye mtaji,ofisi zote mbili zilikuwa na nyomi ya wateja,tulipiga kazi mpaka mwaka unaisha working capital inasoma 250M,mwaka wa pili wembe ulikuwa ulele ila mwishoni mwa mwaka wa pili mambo yakaanza kuslow down!

Nikakumbuka ile kauli ya ngurumo kuhusu wale ng'ombe,nikahisi itakuwa Kuna uhusiano na hiki kinachonitokea,ikabidi nitafute namna ya kufungua hiyo code!

Niliwaza huenda bijan atanifungulia hii code,maana wale viumbe wana IQ kubwa Mara kumi ya mwanadamu.

Nikafika home,nikazama chumbani kama kawaida,niliita bijan....kimya,nikaita tena bijan...ukimya ulitawala,nililikaa mule chumbani najiuliza nini kinatokea mbona sio kawaida, baadaye kidogo bijan alitokea,nilimuuliza"kulikoni"lakini hakunijibu,alikaa kimya na baadaye kidogo alitoweka,nilipoona bijan hasomeki,nilipata wazo la kumtafuta mzee fabi,maana nilikosa kabisa utulivu wa kiakili....

Mm:habari,shikamoo mzee wangu

Mzee fabi:marahaba kijana, unaendeleaje?vp changamoto zako zimeisha?

Mm:aha wapi!mzee wangu,biashara hazihishiwi changamoto,linatoka hili linakuja hili(nilimuuliza mzee fabi kuhusu ng'ombe kiroho wana maanisha nn?)
Mz fabi:kwanini umeniuliza swali Kama hilo?
Mm:mzee nimeota ndoto,kwenye ndoto nikaona ng'ombe wawili,baada ya hapo biashara zikaanza kusua sua(ilibidi nimdanganye mzee fabi,asije akanishtukia Kama nimejiingiza kwenye dark side)

Mz fabi:mmh,kijana suala la ng'ombe kwny ulimwengu wa roho ni fumbo gumu...nakumbuka uliwahi kuniambia wazazi wako waote,walishafariki?(uliuliza mzee fabi)
Mm:ndio,walifariki tangu niko sekondari.
Mz fabi:na kwenu mlizaliwa wangapi?

Mm:tumezaliwa watatu,Mimi ndio firstborn na nina wadogo zangu wawili,mmoja wa kike na mwingine wa kiume.

Mz fabi:kijana sijui imani yako,lakini ng'ombe kwenye ulimwengu wa roho wana maana mbili,
1)ng'ombe humaanisha mwaka yaani kipindi cha miezi 12,kwahiyo Kama uliona ng'ombe wawili.maana yake ni miaka miwili....
"Nilikuwa makini sana kumsikiliza mzee fabi,huku nikilinganisha na situation yangu"

..kabla mzee fapi hajamalizia...alitokea bijan akasimama mbele yangu,alionekana ni mwenye hasira.
Bijan:huyo mzee ni mtu mbaya sana,achana naye,rafiki zako wa ukweli ni sisi na ngurumo.

Wakati namsikiliza bijan,mzee fabi aliendelea kuita halo...haloo,ilibidi nimwambie,samahani mzee wangu nitakutafuta baadaye.

Wakati naendelea kuongea na bijan,simu yangu iliita,kucheki ni mzee ngurumo.

Ngurumo:kijana naona umeanza kuvunja masharti,?

Mm:mbona sijavunja sharti lolote!
Ngurumo:huyo mzee ulikuwa unaongea naye nini?
Mm:ni mambo ya kawaida tu
Ngurumo:sawa,sasa naomba wewe na bijan mje kwangu leo saa mbili usiku kuna mambo tuyaweke sawa.

Baada ya kuachana na bijan, niliwaza kuhusu ile tafasiri ya mzee fabi kwamba wale ng'ombe wawili ni miaka miwili,niliona tafasiri yake ina ukweli,kwasababu miaka miwili imeisha tu mapichapicha yanaanza tena.

Nyumbani kwa ngurumo
Ilipofika saa mbili kimili,Mimi na bijan tulikuwa tumeshafika nyumbani kwa ngurumo.

Ngurumo: nimewaita ili tuimarishe agano, miaka miwili imeshakwisha na mafanikio tumeyaona,sasa ni wakati wa kukuinua uwe mfanyabiashara mkubwa Tanzania yote wakujue..

Mm:nakuamini sana mzee wangu,kila unachosema kinatimia,ni ndoto yangu niwe mfanyabiashara mkubwa sana hapa tanzania.

Ngurumo:usijali,hicho ni kitu kidogo sana kwangu(ngurumo aliingea huku akijipiga kufua)

Aliendelea kuongea...........
Ngurumo:sasa inabidi utoe ng'ombe wawili tena
Mm:haina shida,niko tayari hata kesho...
Ngurumo:kesho na kesho kutwa kuna mambo inabidi tuyaweke sawa,siku ya tatu ndio tutawatoa hao ng'ombe(ngurumo alimaliza kuongea)

Kesho yake
Nilipoamka asubuhi, kucheki simu yangu nakuta text ya mdogo wangu wa kike,ananiambia kuna ndoto ameota kuhusu mimi!nilishtuka sana, kwasababu huyu mdogo wangu akiota kitu basi 100% ni kweli.
"Bro nimeota usiku wa kuamkia leo,mimi na mdogo wetu wa mwisho umetutoa kafara"(hiyo text ilisomeka hivyo)

Wadau,kwenye ulimwengu wa roho,kuna kitu kinaitwa "binah"hii ni kama spiritual intelligence ambayo inamsaidia mtu kujua hatari iliyopo mbele hata kabla haijatokea,binah wanayo sana wasichana bikra na wanawake wanao mcha M-ngu(mwanamke akizini anapoteza vitu viwili "binah na loyalty" hii ndio sababu gadafi alikuwa na mabodigadi wa kike ambao ni bikra,alilenga binah na loyalty)

Tuendelee na ile sms
Baada ya kusoma ile meseji,nikamjibu
"Hiyo ni ndoto tu mdogo wangu,ipuuze,siwezi kufanya hivyo"
akanitumia text tena
" Mimi nikiotaga huwa inakuwa kweli,kama una mambo yako naomba uachane nayo"
nikamjibu
"Mimi ni mtu poa sana sina baya na nyie wadogo zangu ninawapenda,siwezi fanya lolote baya"
akamalizia kwa kunijibu"mh haya"
hii siku nzima nilishindwa kufanya chochote,nilikaa tu kitandani nawaza hiki alichoniambia mdogo wangu,nilivuta picha kwamba hao ng'ombe wawili ndio hao wadogo zangu,ndio maana hata mzee fabi aliniuliza nina wadogo wangapi?..nilijilaza pale kitandani,mpk nikapitiwa na usingizi....
kesho yake
Ikawa imebaki siku moja ya kuwatoa wale ng'ombe,akili yangu ilibadilika,niliwaza mbona ng'ombe wa kwanza niliwatoa na hakukuwa na baya,nikawa najitia moyo kuwa hawa watakuwa ni ng'ombe tu wa kawaida kama wale wa mwanzo..wakati naendelea kutafakari nilikumbuka mzee wangu(baba mzazi) akiwa amalazwa anakaribia kukata moto,aliniambia"wewe ndio mkubwa,unajukumu la kuwaangalia wadogo zako"haya maneno ya mzee wangu yalinifanya niwe njia panda,sijui niwatoe hao ng'ombe au niachane? Nikiacha lazima mambo yangu yaharibike na nitapatwa na mabaya lakini pia nikiwatoa harafu ndio iwe kweli ni wadogo zangu,nitapata laana ya mzee kumwaga damu isiyo na hatia....
*****************************
Siwezi kukaa njia panda daima lazima mwisho wa siku nifanye maamuzi,bado siku moja...je nitachukuwa maamuzi gani?............khodahafez

EPISODE 11 & EPISODE 12
fungua page 33 na page 39, respectively.
 
Hakuna shule hakuna chuo utafundishwa kuhusu dark side of anything,Kuna njia mbili tu za kujua wasichokijua watu wengi,njia nyepesi zaidi ni kujua kupitia shuhuda za watu waliopita kwenye kivuli cha mauti na wakatoka salama na njia ngumu zaidi ndio Kama niliyopitia Mimi,i dip my feet into the ways of darkness.

Angalizo
Hiki ninachoandika ni experience ya miaka mingi nyuma, now mimi ni mtu safi,i believe in G-d na kwa kila nnachofanya i pray for his guidance.

Lengo la uzi
Nataka ujue upande wa pili wa shilingi,the dark side of business,uujue ulimwengu wa kiroho wa Biashara kwasababu huko ndio karata zinachezwa huko ndio kete zinasukumwa,sitaki upite dark side nataka upite light side(G-d side) kwasababu mafanikio bila giza yanawezekana.

This is my story
Nikiwa advance kwenye mkoa mmojawapo wa kanda ya ziwa,hapo shule nilipangwa room moja na machalii wawili kutoka A town na Kama unavyojua spirit ya wachaga wengi ni Biashara so ikawa story nyingi ni kuhusu biashara,chalii mmoja(tumwite fabi)ndio alikuwa moto sana na issue za biashara,kwasbb baba yake alikuwa mfanyabiashara mkubwa sana huko chuga,so jamaa alitamani kuvaa viatu vya baba yake.
Mzee wa fabi alikuwa ana hardware mbili kubwa town na nyumba za kutosha,alikuwa ni realestate guru,simply huyu mzee alikuwa tajiri,Kuna likizo tulienda chuga ili nipate mawili matatu kuhusu biashara.

Mzee fabi:ahaa wewe ndio rafiki yake fabi
Mm:ndio mzee,
Fabi:huyu ndio yule rafiki yangu niliyekuambia anapenda kufanya biashara
Mzee fabi:sawa,karibu sana kijana ila someni hizi Biashara mtazikuta tu,sisi hatukusoma lkn hesabu za Biashara tunazijua...(wote tukacheka)then mzee akaondoka akaenda kwenye mishe zake.
siku iliyofuata fabi alinizungusha kwenye miradi ya mzee,alikuwa na lodge 3,semi mbili na nyumba za wapangaji za kutosha,I was amazed!nikasema hakika business is a sure way onto riches,nilitamani nianze mishe za biashara hata kabla sijamaliza shule,kichwa iliwaka moto,baada ya likizo tulirudi shule nikiwa na vibe la kutosha.

Tukiwa shule
Tukawa tunaulizana tukimaliza shule tufanye issue gani!,fabi akawa anasema akimaliza anataka kuuza vocha za jumla(vocha za mitandao ya simu)mimi nikawa nasema nataka kuuza mafuta(dealer wa hizi cooking oil) so siku moja tukaenda town(shule yetu ilikuwa porini,ndani ndani) lengo la kwenda town ilikuwa ni kufanya utafiti wa hizo mishe tulizoplan kuzifanya,hapa nieleze ujanja flani aliotufundisha mzee wake fabi"ukitaka upate wazo zuri la Biashara angalia customer Queueing" akimaanisha angalia biashara inayotengeneza foleni ya wateja,isee huyu mzee hajasoma lkn alikuwa na nondo Kama za rich dady😃
Sasa huwezi kuamini tulizura pale town kucheki hizo mishe Kama zinatengeneza foleni ya wateja,kwanza tuliona maduka mengi yanayofanya mishe hizo ni ya wahindi(huko mbele nitakuja kueleza dark side ya hawa jamaa hapa bongo,Wana hadi kitabu maalumu cha namna ya kumpiga pin mtu mweusi awe Kama working machine)hawa jamaa kwa sehemu wametuzidi kete(kete za kiroho)....maduka mengi makubwa yalikuwa yao na kweli ile mishe ya vocha tuliona ina foleni si ya kitoto hadi na mm nikashawishika ku abort mishe ya mafuta!niingie kwny vocha.
*****************************

Wadau itabidi nigusie issue muhimu tu ili gazeti lisiwe refu,Sasa nini kitajiri baada ya kumaliza six na kuingia rasmi mtaani..........nitarudi
Hapa ni JF shusha TU gazeti haina shida maana hata ukiongea ukwl lazima utapondwa so shusha nondo iwe muhimu au isiwe muhimu
 
Hakuna shule hakuna chuo utafundishwa kuhusu dark side of anything,Kuna njia mbili tu za kujua wasichokijua watu wengi,njia nyepesi zaidi ni kujua kupitia shuhuda za watu waliopita kwenye kivuli cha mauti na wakatoka salama na njia ngumu zaidi ndio Kama niliyopitia Mimi,i dip my feet into the ways of darkness.

Angalizo
Hiki ninachoandika ni experience ya miaka mingi nyuma, now mimi ni mtu safi,i believe in G-d na kwa kila nnachofanya i pray for his guidance.

Lengo la uzi
Nataka ujue upande wa pili wa shilingi,the dark side of business,uujue ulimwengu wa kiroho wa Biashara kwasababu huko ndio karata zinachezwa huko ndio kete zinasukumwa,sitaki upite dark side nataka upite light side(G-d side) kwasababu mafanikio bila giza yanawezekana.

This is my story
Nikiwa advance kwenye mkoa mmojawapo wa kanda ya ziwa,hapo shule nilipangwa room moja na machalii wawili kutoka A town na Kama unavyojua spirit ya wachaga wengi ni Biashara so ikawa story nyingi ni kuhusu biashara,chalii mmoja(tumwite fabi)ndio alikuwa moto sana na issue za biashara,kwasbb baba yake alikuwa mfanyabiashara mkubwa sana huko chuga,so jamaa alitamani kuvaa viatu vya baba yake.
Mzee wa fabi alikuwa ana hardware mbili kubwa town na nyumba za kutosha,alikuwa ni realestate guru,simply huyu mzee alikuwa tajiri,Kuna likizo tulienda chuga ili nipate mawili matatu kuhusu biashara.

Mzee fabi:ahaa wewe ndio rafiki yake fabi
Mm:ndio mzee,
Fabi:huyu ndio yule rafiki yangu niliyekuambia anapenda kufanya biashara
Mzee fabi:sawa,karibu sana kijana ila someni hizi Biashara mtazikuta tu,sisi hatukusoma lkn hesabu za Biashara tunazijua...(wote tukacheka)then mzee akaondoka akaenda kwenye mishe zake.
siku iliyofuata fabi alinizungusha kwenye miradi ya mzee,alikuwa na lodge 3,semi mbili na nyumba za wapangaji za kutosha,I was amazed!nikasema hakika business is a sure way onto riches,nilitamani nianze mishe za biashara hata kabla sijamaliza shule,kichwa iliwaka moto,baada ya likizo tulirudi shule nikiwa na vibe la kutosha.

Tukiwa shule
Tukawa tunaulizana tukimaliza shule tufanye issue gani!,fabi akawa anasema akimaliza anataka kuuza vocha za jumla(vocha za mitandao ya simu)mimi nikawa nasema nataka kuuza mafuta(dealer wa hizi cooking oil) so siku moja tukaenda town(shule yetu ilikuwa porini,ndani ndani) lengo la kwenda town ilikuwa ni kufanya utafiti wa hizo mishe tulizoplan kuzifanya,hapa nieleze ujanja flani aliotufundisha mzee wake fabi"ukitaka upate wazo zuri la Biashara angalia customer Queueing" akimaanisha angalia biashara inayotengeneza foleni ya wateja,isee huyu mzee hajasoma lkn alikuwa na nondo Kama za rich dady😃
Sasa huwezi kuamini tulizura pale town kucheki hizo mishe Kama zinatengeneza foleni ya wateja,kwanza tuliona maduka mengi yanayofanya mishe hizo ni ya wahindi(huko mbele nitakuja kueleza dark side ya hawa jamaa hapa bongo,Wana hadi kitabu maalumu cha namna ya kumpiga pin mtu mweusi awe Kama working machine)hawa jamaa kwa sehemu wametuzidi kete(kete za kiroho)....maduka mengi makubwa yalikuwa yao na kweli ile mishe ya vocha tuliona ina foleni si ya kitoto hadi na mm nikashawishika ku abort mishe ya mafuta!niingie kwny vocha.
*****************************

Wadau itabidi nigusie issue muhimu tu ili gazeti lisiwe refu,Sasa nini kitajiri baada ya kumaliza six na kuingia rasmi mtaani..........nitarudi
Endelea mkuu utupe nondo za biashara
 
Back
Top Bottom