
Inaendelea................
Kuna uzi wangu niliutupia hapa unasema"experience ya miaka 15 ya kijiajiri(nadiriki kusema business is a sure way onto true riches)"kwenye huo uzi sikuelezea hiyo miaka 15 nilikuwa nafanya mishe gani, simply ilikuwa ni mishe ya vocha(wholesale)
Sasa baada ya kumaliza six,nilirudi mtaani na harakati za biashara zikaanza rasmi,kuna biashara ndogo nilianzisha lkn mawazo yangu yalikuwa ni mishe ya vocha za jumla, sema mtaji ulikuwa kipengele,so nikavutavuta siku mpk naingia chuo,ile biashara mdogo ilienda poa kimtindo,kuna dogo nilikuwa namwacha shop,mm naendelea na kitabu,nikapata boom(kwny intake yetu tulichelewa kupata,so tukapewa lumpsum ya mwaka mzima ilikuwa Kama 2.4M),chap nikaigeuza kuwa mtaji wa Biashara ya ndoto zangu,hii biashara ya vocha ni kama Biashara ya mafuta,faida yake ni ndogo sana lkn ukiuza mzigo mkubwa faida unaiona,kipindi hicho hii mishe ilikuwa 🔥 🔥 ila now days ni ya kawaida sana,kuuza mzigo wa milioni 5 kwa siku ilikuwa ni jambo la kawaida,nilichanganya shule na biashara kwasababu sikuwa na gutts tena za kusubiri mpk nimalize.
Chuo kilipoisha,
Kwa kweli sikuwa hata na chembe ya kutafuta ajira ijapokuwa matokeo yalikuwa mazuri,washkaji niliomaliza nao walikimbilia ajira,mimi nikaingia rasmi kwenye biashara ya vocha za jumla, wakati namaliza chuo mtaji ulikuwa kama 3M hv lkn ndani ya miezi sita mtaji ukafika 10M miezi sita mingine ikafika 20M,kwa waliofanya mishe hii backdays wanajua kama ukiuza mzigo wa milioni basi faida ni elfu 20,nilikuwa nauza mpk 8M kwa siku,kukunja laki hadi laki na nusu perday ilikuwa kawaida,dat time nikanunua kiwanja,nikajenga maflemu kama nane,then kwa nyuma niliplan kujenga apartments za kupangisha,nilinunua hiace(daladala)ili nitanue wigo,it was amazingl!coz I was just 23,nikazidi kusema "business is a quickest way onto riches" ila sikujua kuwa business is also a riskiest way onto riches,kwa ufupi ile side A ya biashara niliimaster ipasavyo,nilipiga kazi sana mpk watu wakahisi natumia ndumba,kwasababu ofisini watu walikuwa wanajaa,foleni kama nmb,hakika biashara na maisha kwa ujumla viliniendea poa,mtaani kila mtu alitamani afanye biashara kwakile alichokiona kinatokea kwangu,nilitengeneza jina kwa muda mfupi sana ghafla yakaanza mapicha picha,mara nikute damu kwny kiti ninachokalia pale ofisini,Mara hirizi,pesa zikawa zinapotea kimazingara,hua siamini uchawi lkn hiki kilichokuwa kinatokea ni uchawi bila chenga,nilifukuza wafanyakazi lkn haikusaidia(nilihisi wananipiga)nilipiga moyo konde lkn changamoto zilizidi to the extent nikaanza kuogopa biashara,kwa kweli nilibaki njia panda,ila Kuna wazo likanijia,juu ya nini cha kufanya......................
*****************************
Biashara zina ups and downs,niliona upande mmoja,sasa dunia inanionyesha upande wa pili,nini kitaendelea baada ya kupata wazo.............usikose