Nitatoa ufafanuzi kidogo kwenye hii story ya mleta mada kulingana na elimu yangu ya dunia/ ulimwengu niliyonayo
Wana JF siri kubwa na ufafanuzi ipo kwenye kile kitabu cha " chuo Kikuu cha wachawi" kina story kama hii na sababu ya vitu kutendeka.
Nilikisoma muda mrefu sana jina la mwandishi silikumbuki kwa anaelijua au mwenye picha ya kitabu hicho atume humu JF
Point yako kubwa hapa kwenye maelezo yako ni " the power of autosuggestion ". Kila kitu huyo mzee anacho suggest kwenye akili yako, akili yako inachakata hiyo jambo nakulidhiirisha.
Atakuambia anaogopa lakini akiwa hana ela utasikia mimi hata mwizi safari hii ntakuwa..
Tusiwe na maarifa tukayashindwa yatumia. Sawa na kuwa na bunduki porini unaona nyati akajuka nakuondoka wewe unaangalia tuu, kisha baadae wakuja simulia ya huko porini
We ni kumahkibuyu kama kumah wengine. [emoji706]Sjawai ona janaume lenye gubu kama jike kama wewe..janaume.linasutana kutwa nzima kwenye mitandao..[emoji706][emoji867] niggah ur dead.
Atakuambia anaogopa lakini akiwa hana ela utasikia mimi hata mwizi safari hii ntakuwa..
Tusiwe na maarifa tukayashindwa yatumia. Sawa na kuwa na bunduki porini unaona nyati akajuka nakuondoka wewe unaangalia tuu, kisha baadae wakuja simulia ya huko porini
Point yako kubwa hapa kwenye maelezo yako ni " the power of autosuggestion ". Kila kitu huyo mzee anacho suggest kwenye akili yako, akili yako inachakata hiyo jambo nakulidhiirisha.
NJIA YA KUFANIKIWA IN LIGHT SIDE
Nimeulizwa hili swali. Ni ipi njia ya kufanikiwa kiroho in Light side?
Kwa Experince na mtazamo wangu njia ni hii
Kwa wanao muamini Mungu
Njia pekee ya kufanikiwa kibiashara ni light side.
Unachohitaji ni [ A ]
Mtaji. , ubunifu, watu sahiihi, kujituma kutokukukata tamaa, kipaji ...n.k
Sasa Mungu anakujaje kwenye biashara.
Kwenye huu ulimwenhu kuna siri nyingi ambazo huwezi kuziona kwa macho ya kawaida au siku yakikukuta ndo utajua, vinginevyo endelea kusikia kwenye story za watu , siku ya kikukuta ndo uanze kuamini
Ili ufanikiwe Kwenye biashara kiroho kwa kupitia kwa Mungu kwa kinachohitajika Ni
Ulinzi wa kiroho = kwani kuna watu hawatapenda wewe uendelee au uwazidi ndipo chuki, majungu na kuendeaana kwa waganga panapo anziaga ni hapo ilimradi ufeli
Ukishatekeleza hayo nilioandika kwenye [ A] hapo juu. Maswala ya mvuto wa kibiashara na mafanikio yanatoka kwa Mungu
Cha muhumu ni wewe kuwa na uhusiano na conection na Mungu.
Unaipataje Hio connection na uhusiano?
Kwa
1 Toba na utakaso wa dhambi kwa kutubu.
Ili ukubali kuwa umeacha yale yote ya kale uliokuwa unayafacha dhambi ..nk yaani vitu visivyompendeza Mungu na umeamua kuwa mcha Mungu
2 Kusoma Biblia maana ndio maandiko yatakayo kuimarisha kiroho ili uwe mcha Mungu
3 maombi na sara. Ndo njia pekee ya kuongea na Mungu. Hakikisha unasali walau mara 3-5 kwa siku
( interval utakayo amua wewe kama kira baada ya masaa 8 au 6) ni sawa
4 Kufunga na kusali; namaanisha kukaa bila kula chakula waweza kunywa maji. Unaweza kuamua kufunga kuanzia asubuhi na ukala saa 12 jioni na saa 6 usiku.
5 usiwe mtenda dhambi kupindukia
Ukishafanya vyote hvyo ndani ya mwezi 1 hadi 3 utakua tayari una ulinzi wa kiroho wa Mungu pamoja na connection na Uhusiano wake.
Dalili utaziona kwenye ndoto utakazo anza kuziota
Ukisha anza kufanikiwa anza kutoa msaada kwa watu wasiojiweza mayatima, wagonjwa nk ndo njia ya kuongeza baraka
Ukisha vipata hivyo 3 yaani Ulinzi wa kiroho wa Mungu, uhusiano mzuri na Mungu pamoja na connection nakuhakikishia hakuna wa kugusa kiiimanini , kichawi, kishirikina nk
NB. Ata ukachukue mafuta, mchangaa, kitambaa, udongo kwa nabii wako bila kufanya nilio andika hapo juu hutoboi kibiashara maana Mungu akikubariki ni Life time au milele. Yaan watoto na kizazi chako chote kitabarikiwa kupitia wewe ata kwenye kuendeleza miradi yako.
Wale wa dark side hua sio milele kila baada ya muda fulani huwa wanaambiwa watoe sadaka/ wa mwage damu au dawa imeishiwa nguvu inabidi kutumia dawa nyingine
Ukisha pata uwepo wa Mungu ndani yako , maombi yako yote ya direct ufanikiwe ki biashara zako.
Kumbuka huko mwanzo ulikua unaomba uwepo wa Mungu uje ndani yake na katika maisha yako.
Sija taja dini au kanisa kwani kwangu mimi dini au kanisa ni njia anayotumia binadamu kukaa karibu na Mungu au kukkutana na wacha Mungu wenzio yaani kwa lugha nyingine Religion and chuch is pathway to Godliness. Sio gurantee kwamba ukiwa dini fulani au kanisa fulani ndo unakua mcha Mungu. Kinachohitajika ni JITIHADA ZAKo BINAFSI kumtafta Munvu kwa kufanya niliyo yaandika hapo juu.
Mambo ya niende kwa Nabii sijui mchungaji aniombee hayasaidii na hayatakupeleka popote . Ni JuHudi binafsi ya kumtafta Mungu kwa kufanya nilioyoyaandika hapo mwenyewe sio na wanakanisa au na nabii wako
Hivyo vitu vi 3 utavipoteza kwa kuwa mtenda dhambi au kufanya dhambi kupindukia. hasa ya KUZINI
Kwa nini kuzini?
Kwa sababu kuna wanaume/wanawake wanabeba roho/ spirit chafu, maagano ya ukoo, laana ..nk sasa utakapo sex nae ndo nawewe unabeba hizo roho kwani kwenye sex ndo portal ya wewe kutoa au kutokwa na baraka/ ulinzi wa kiroho n.k.
wale wa dark side ndo maana mtalaam akikupa dawa moja ya sharti ya dawa fulani uwa usifanye Sex kwani unaweza kupoteza nguvu ya dawa kwenye tendo hilo.
Watalaam mambo ya kidunia huwa wanasema mwanamke akiwa kwenye siku zake hua ni hatari sana kwani anaweza kupokea au kukupa spirit/ roho/ laana / magano kupitia sex ( hii story ya siku nyingine)
Ukiwa ushapata vitu hivyo wi 3 ya ulinzi wa kiroho wa Mungu, connction pamoja na uhusiano na ukafanya zinaa na mtu hasiye mke wako wa ndoa BAAS hivyo ndo Mungu atakapo uondoa uwepo wake nda yako.. Utajihisi MWEUPE yaan huna kinga /ulinzi wowote ule wa kiroho. Na kati ya vitu vigumu duniani ni kuuludisha huusiano wako na Mungu baada ya wewe kuuvunja. (Mffano ni petro alivyo mkana Yesu ma 3 kafatilie ako ka kipande ka hio stori ana kwambia alijihisi mweupe, manung'uniko ya kutosha au kwa samson na delilah baada ya uwepo wa Mungu kumtoka samson haikua Easy hivihivi kuurudisha)
Ulinzi wa kiroho kwa binadamu unatoka kwa Mungu, mizimu, uchawi, ushirikina, majini n.k
Ndo maana ukienda kwa waganga cha kwanza ni kuk scan au kwa lugha nyingine kukuchunguza kwenye chungu iliwaone kama una kinga/ulinzi wwte wa kiroho wa kukulinda . Kama huna ndo utaskia anasema wewe ni MWEUPE. Yaan huna kinga au ulinzi au kama unao basi hauna nguvu unaweza kudhulika muda wowote
Mfano
Ndo maana una skiaga story za fulani kanyeshwa sumu ili afe ila bado yupo hospitalini anapigania maisha yake .
HAPO unajifunza kwenye hii dunia sio kila kitu anapanga Mungu kitendeke vingine anapanga mwanadamu.
Turud kwenye mfano wetu wa sumu.
Sasa hapo kama alienyeshwa Sumu ni Mcha Mungu na Mungu hajapenda yeye afe atamuokoa arudi kwenye hali yake. AU
Kama huyo mtu alikua gwiji kwenye kuabudu mizimu na anatekeleza yte aavizwayo itampambania yeye aurudi kweye hali yake hivyohivyo kwa wachawi, majini n.k
Sasa wewe kama huna kinga / ulinzi utakua una ona una mabalaa na mikosi maana huna kinga/ ulinzi wa kujlinda mambo mengine ya kuache/ kupitie kushoto. Ndo mtu anakua na malalamiko ya kwanini mm hiki kinanikuta wengine hamn ( Mungu hajapanga vingine wamepanga binadamu kukukwamisha)
Ndo maana kwenye story ya " dark side of bussiness mzee ngurumo anasema dereva aliebeba ng'ombe kama hana ulinzi atakufa kwenye ajari. ( pia unajifunz mzee ngurumo na binadamu wengine wana ka technique ka kutambua fulani hana kinga au hana, usitukane au kumfanyia mtu mabaya huwezi kujua ulinzi wa kiroho alio nao una nguvu kiasi gani) ndo maana unaona wanasema ngoma nzito au kuingia choo cha kike watu wengine ni balaa unaweza kumtendea mabaya uu kumtumia kitu ila hakim kuti vinakurudia wewe alafu yakikurudia hua ni hatari sana kama sio kigo basi ni stroke au ulemavu
Na pale "kwenye ajari ya gari lilo beba ng'ombe" ndo maana kuna ajari nyingine zinatokea ila ukiangalia eneo au sehemu ajari ilipo tokea huoni damu ata barabarn. Damu huwa zinachukuliwa kimazingara na wachawi. Kuna mtu atabisha eti labda wamepata internal bleeding yaani damu imevujia kwa ndani/ ndani ya mwili.
( Tanzanian dream vipi hio ajari kwenye baranara kuna damu yyte ilichuruzika?)
Uki kaa na madereva wa mabasi na malori watakuelezea vizuri hio topic ya ulinzi / kinga kiroho kwani wanayo kutana nayo/ kuyaona barabarani ndo maana utaskia wana kimbilia kinga/ ulinzi wa kiroho
Wale wakina Tomaso wazee wa kubisha na kutoamini mpaka waone. Siwalazimishi muamini.
Na wapa assignemt.
Kila kipindi cha uchaguzi MCC utoa fedha nono kwa waganga wa Tz nzima ili wasitoe dawa yoyote kwa mwanachama yoyote wa upinzani itakayo msaidia ashinde chaguzi. Ka waulize waganga wa mkoa unaokaa walikutania wapi na MCC na wakapewa dau gani
Au
Ushasikia duka la muhindi au mwarabu limeibiwa kiujambazi? Basi kafatilie/ kawaulize waliowahi kuwaibia uwa kinawakuta nini? Sehemu zao za bishara huwa wana ulinzi wa kiroho wa kutosha usione kwa nje kaweka vitu vyke tu easy unakuta electronics kama Tv au pesa kaziachia wazi tu chukua kijambazi huone kitakachokukuta.
Au
kama umefatilia stroru ya mwana JF humu inasema kua walienda kwa mtalaam akawapa dawa na hirizi kabla hawajaenda kwenye tukio kufanya tukio lao la ujambazi. Kama ni ishu ya silaha na ngumi kwanini wasitumie kwenye kuiba mpka wakatafte kinga/ ulinzi utakao walinda pale watakapo pata shambulio la kiroho kwenye jambo lao.ni iweke hivi kua Kuna mali nyingine zimelinda kiroho. ( nyumba, benki, ikulu ila hii ni stori ya siku nyingine)
Usipo kaa na wakubwa wa nchii hii na dunia siri nyingine za ulimwengu unaweza ukafa hujazijua au kuzisikia masikion mwako
Hii njia ina Apply kwa mafanikio yoyote unayoyataka duniani iwe kibiashara, kimasomo, kilimo, siasa ...nk
Kwa kumalizia
Kwa experience yangu haya maisha tunayoishi ni ya kiroho. Unaweza ukakataa ila siku yakikukuta ndo utayajua kwa sahivi wewe kula shule ya dunia changanya na story za watu. Siku yakikukuta utaona vina make sense.
#SIKULAZIMISHI UAMINI MANENO YANGU. UNACHOTAKIWA KUFANYA NI WEWE KULA SHULE YA DUNIA/ ULIMWENGU NA CHAGUA NJIA YAKO KUISHI.
Kwa sasa tuachie hapo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.