Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
INSIDER MAN huyu jamaa story yake ndo the best tangu nimejiunga na JFhuysi yule jamaa mwenye story za waganga kongo na ubber driver ni wasimulizi wazuri sana
Stability ni ngumu kutenganisha mvuto na utajiri,ukilifata giza,kafara haziepukiki na mwisho zina madhara makubwa...fatilia huu uzi mpk mwisho,utapata kitu.Mkuu
je kama mtu atataka tu aende kupata mvuto wa wateja bila kufanya hizo kafala kwa ajili ya mali kubwa.
Je inawezekana? Pia ina madhara/gharama kwake katika ulimwengu wa kiroho hata kwa baadae?
jay-millions Episode ya 11 tayari........Tuendelee ndugu, umefika patamu
Stability ni ngumu kutenganisha mvuto na utajiri,ukilifata giza,kafara haziepukiki na mwisho zina madhara makubwa...fatilia huu uzi mpk mwisho,utapata kitu.
DuuuuuuhEPISODE 11
Ilipoishia...
nilikuwa njia panda,sijui niwatoe hao ng'ombe au niache? Nikiacha lazima mambo yangu yataharibika na nitapatwa na majanga lakini pia nikiwatoa harafu ndio iwe kweli ni wadogo zangu,nitapata laana ya mzee kwa kumwaga damu isiyo na hatia......
Sasa tuendelee
Baada ya kuwaza sana,mwisho wa siku nilifanya maamuzi magumu,niliamua nisiwatoe wale ng'ombe lakini sikutaka kumwambia ngurumo wala bijan,nilifanya maamuzi kimya kimya.
Nilijua haya maamuzi mwisho wa siku yatanigharimu,lazima yataibua vita kubwa sana, ukizingatia ngurumo na bijan ni wakongwe kwenye mambo ya kiroho,nilijiona Kama nacheza na moto.
Mara nyingi nikiwa kwenye situation Kama hizi namkumbuka mzee fabi,huyu mzee nilipenda kumwita"wisest person in the world" nilijua tu huyu mzee hatashindwa kunisaidia,hivyo nikapata wazo la kusafiri na kwenda A town,nilitaka nisafiri kimya kimya bila hata kumwambia mzee fabi.
Safari kuelekea chuga
Nilifanya maamuzi ya kukimbilia chuga ili ile siku ya kutoa ng'ombe ikifika,mimi nisiwepo,niwe chuga mafichoni,nilichukua baadhi ya nguo na vitu muhimu,nikaondoka.....
Nilifika A town,moja kwa moja nikamcheki fabi,nikamwambia niko town kwa dharula(fabi alinielekeza anapoishi,safari hii alikuwa anaishi kwake,ametoka pale kwa mzee wake)
Nilifika kwa fabi,tukapiga story za hapa na pale,lakini sikumwambia nimekuja chuga kufanyanini..(baada ya maongezi,nilimwomba fabi aniruhusu nikapumzike,maana nilikuwa nimechoka kimwili na kiakili)
Baada ya kuingia chuga na kuonana na fabi,niliamua kuzima simu ili ngurumo akinitafuta asinipate.
Kesho yake
asubuhi wakati fab anajiandaa kwenda job na mimi nilijiandaa ili tuondoke mwote(kumbuka saa hiyo fabi anafanya kazi palepale kwa mzee wake).
Tulifika dukani kwa mzee fabi,tukapanda juu mpaka kwenye ofisi ya fabi(ofisi yake ni kama hatua kumi kutoka ilipo ofisi ya mzee wake)
Nilikaa pale ofisini kwa fabi ili nimsubiri mzee fabi.....
Baada ya muda kidogo mzee fabi aliingia,nikamfuata ofisini kwake.
Mm: nimekuja tena mzee wangu, changamoto haziishi!
Mzee fabi(alicheka,kisha aliendelea kusema)..isee wewe ni kiboko, changamoto gani hizo zisizo kwisha?
Mm:mzee umenisaidia mambo mengi ila kwa sasa napita kwenye wakati mgumu,hata sijui nifanyaje?(ilibidi nimweleze mzee fabi kila kitu sikumficha,mambo ya giza yote niliyofanya nilimwambia....hapa kwa Mara ya kwanza navunja lile sharti la kwanza la kutunza siri)
Mzee fabi:kijana unapita mahali pagumu(aliongea huku akinyanyuka na kwenda kwenye shelfu ya vitabu)
Mzee fabi:nilikuambia elimu ya maisha ipo kwenye vitabu,tangu nimekupa kile kitabu cha "dark path" je kuna kitabu kingine ulisoma?
Mm:baada ya kusoma kile kitabu sikuwahi kugusa kitabu tena..
Mzee fabi akiwa pale kwenye shelfu,akachomoa tena kitabu kimoja akanipa,akaniambia nenda kasome na hicho.
Mm:mzee wangu nahitaji kinga ya kiroho ili mzee ngurumo na wale viumbe wasiweze kunidhuru,kitabu hakiwezi kunisaidia.
Mzee fabi:akaniuliza,kwenye mchezo wa mbio za farasi ni farasi gani mara zote anashinda?
Mm:kwa kweli sijui
Mzee fabi:farasi anayeshinda mara zote sio mwenye mbio kuliko wote,sio mwenye nguvu kuliko wote,sio mwenye umri mkubwa,sio mwenye umbo kubwa bali ni yule ambaye ni mwepesi kufuata maelekezo ya jockey (rider)
Mzee fabi alimalizia kwa kusema"winning is in following instructions"
Baada ya mzee fabi kunipa huo msemo ilibidi niwe mpole,nifate kile anachoniambia...
Hii ilikuwa ndio ile siku ya kuwatoa wale ng'ombe,ilibidi nitafute chaka moja la bata pale town walau nipoteze mawazo,niliingia milestone bar,pale panasifika sana kwa chama choma,nilivuta muda pale mpk saa nne usiku,nikarudi kwa fabi.
Niliamka asubuhi na hangover,nikasema ngoja nifungue simu nione kama ngurumo alinitafuta...ile kuwasha simu,meseji zilianza kuingia... kucheki ni meseji za ngurumo.
Sms 1
Kijana nakupigia hupatikani,muda ndio huu,fanya haraka tukutane kwa siku ile.
Baada ya lisaa,akatuma tena meseji nyingine.
Sms 2
"kijana umeingia mitini sio,umegoma kuwatoa hao ng'ombe?
Sms 3
Umevunja masharti,nilikuambia mambo haya usimwambie mtu,wewe umemwambia huyo mzee wako,umeikasirisha mzimu.
Sms 4
Umeenda kujificha huko Arusha,unadhani sitajua,kwa usalama wako njoo utoe hao ng'ombe,nakupa siku saba la sivyo kitakacho kupata tusilaumiane.......
hizi meseji za ngurumo zilinitetemesha,nilifikiria nirudi nikaombe msamaha au niendelee kukomaa na msimamo wangu...
Baada ya kusoma zile sms ilibidi nizime tena simu,maana nilihofia anaweza kunipigia na nikakosa cha kusema..baada ya kuwaza sana nilifanya maamuzi ya kurudi kabla hizo siku saba hazijaisha....maana ule mkwara wa ngurumo haukuwa wa kitoto.
Niliingia home usiku mnene
Nimefika home,nikafungua mlango,nikazama ndani...nakuta meza,makochi zimepinduliwa,tv imepigwa chini,vyombo vimesambaa kila mahali,yaani ndani kulikuwa hakutamaniki..nilijiuliza kitu gani kimetokea mle ndani,sikupata jibu....niliingia chumbani nakuta vioo vimepasuliwa,gogoro limechanwa chanwa,nguo zimetapakaa kila mahali......
*******************************
Nini kimetokea kwenye pale nyumbani kwangu,nani kafanya ule uharibifu...............usikose episode ya mwisho(episode
Huyo bijana alikuwa wa umbo gani, sura gani, rangi gani, nywele aina gani na aanavaa maavazi gani?Stability ni ngumu kutenganisha mvuto na utajiri,ukilifata giza,kafara haziepukiki na mwisho zina madhara makubwa...fatilia huu uzi mpk mwisho,utapata kitu.
Bijan alikuwa kama waarabu wa iran,ana umbo la kawaida,urefu futi sita tulilingana,Mara nyingi alitokea na mavazi ya zambarau na mara chache sana alivaa mavazi meusi,hizi nguo ni kama kanzu..Huyo bijana alikuwa wa umbo gani, sura gani, rangi gani, nywele aina gani na aanavaa maavazi gani?
Tusaidie ili twende sambamba
Sawa sawa ahsanteBijan alikuwa kama waarabu wa iran,ana umbo la kawaida,urefu futi sita tulilingana,Mara nyingi alitokea na mavazi ya zambarau na mara chache sana alivaa mavazi meusi,hizi nguo ni kama kanzu..
shusha uzi mkuuBijan alikuwa kama waarabu wa iran,ana umbo la kawaida,urefu futi sita tulilingana,Mara nyingi alitokea na mavazi ya zambarau na mara chache sana alivaa mavazi meusi,hizi nguo ni kama kanzu..
LUKA 4:5Kafara za nini?
Wanyama, binadamu, au kafara za aina gani?
Kama kutoa kafara ndio ingekuwa inafanya utajiri kuongezeka, Basi Elon musk ndio angekuwa mtoa kafara namba moja duniani.
Lakini sivyo, Kuna wakati Elon musk utajiri wake hushuka na si kwamba eti hajatoa kafara ndio maana utajiri umeshuka hapana, Ni kwa sababu hisa zake, uzalishaji wake umepungua kwa kiasi fulani ndio maana anapitwa na wengine.
Hakuna shetani anayetoa utajiri.