KwetuKwanza
Senior Member
- Mar 13, 2023
- 127
- 245
INEC pia ilitangaza upande wa nafasi za Ubunge wa Majimbo, Udiwani, CCM ilitangazwa kushinda kwa kishindo katika maeneo mengi.
Wakati na baada ya Uchaguzi huo kilichotokea ni kubaki kwa alama ya kipekee na ya kusikitisha, kwani nchi iliingia katika machafuko, Watu wakajeruhiwa, wengine wakauawa, wakapoteza mali, wapo waliobaki na ulemavu wa maisha n.k
Mawakala wa Vyama wakila Kiapo cha kutunza Siri kwenye maeneo yao kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika 29 Oktoba zoezi hilo la kuwaapisha limesimamiwa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Kata Okt 22, 2025. Picha bagamoyodc
Katika uchaguzi huu, Nilijipa kazi kubwa ya kufanya uchunguzi eneo moja lililohusisha Mawakala wa Wagombea kutoka Vyama vya Upinzani.
Nilijiuliza Je? Hawa Mawakala hasa wa upinzaji huwa wanakuwa huru kutekeleza majukumu yao kisheria?
Lengo la uchunguzi wangu ilikuwa kujua kama kweli uchaguzi ni huru na haki kama ambavyo wengi wa watawala wanajinasibu, nilitembelea mikoa miwili kuifanya kazi hiyo, ambayo ni Simiyu na Shinyanga.
MAWAKALA WALIKUWA “MASTAA WA SHOO”
Nilibaini asilimia kubwa ya Mawakala wa Vyama vya Upinzani walipewa viapo kama ilivyo kwa Mawakala wa CCM lakini walichokifanya ni hatari kwa demokrasia na wameonesha uchaguzi haukuwa huru na haki.
Kwa ufupi ushindi wa asilimia kubwa kwa CCM ulitokana na wasimamizi wa uchaguzi katika vituo kutimiza “michezo yao michafu” kwa ukamilifu.
Baada ya mawakala wa vyama vya upinzani kutoweka na wakabaki wale wa CCM zoezi la kutiki karatasi za Kura lilianza kufanyika likiongozwa na wasimamizi wa uchaguzi kwenye vituo.
Vituo vingi vya Kupigia Kura, Mawakala wa Vyama vya Upinzani hawakuwepo licha ya kupewa viapo, wengi walisusia, wengine walitolewa baada ya “kuelewana” na wale wa upande wa pili.
Mawakala waliofika Vituoni kufanya kazi, wengi wao walirubuniwa na wakapotea kwa hiyari katika mazingira tata…
…Kuna vituo vinne katika mkoa wa Shinyanga, niliambiwa na Wasimamizi kuwa baadhi ya Mawakala “walilamba Sh 50,000” kila mmoja, ndio maana maeneo mengi hayakuwa na vuta nikuvute kama ilivyotokea katika chaguzi zilizopita.
Mawakala wa Vyama wakila Kiapo cha kutunza Siri kwenye maeneo yao kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika 29 Oktoba zoezi hilo la kuwaapisha limesimamiwa na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Kata Okt 22, 2025. Picha bagamoyodc
Wagombea wengi wa upinzani hawakuwa vizuri kiuchumi, uwezo wa kulipa Mawakala wao posho ulikuwa mdogo, hivyo ilikuwa ni rahisi kwa Wawakilishi wao kununulika kirahisi.
Pili, upinzani uliooneshwa kwenye Uchaguzi haukuwa imara. Chama Kikuu cha Upinzani (CHADEMA) hakikushiriki, hivyo wale walioshiriki hawakuwa na nguvu ya kushindana na CCM.
KARATASI ZA KURA KUTIKIWA NA WASIOHUSIKA
Baadhi ya vituo wasimamizi walikuwa ndugu zangu, wengine marafiki zangu pia, hivyo walikuwa huru kunionesha kilichokuwa kikiendelea.
Kuna kituo kimoja nilielezwa kuwa walifika Wapiga Kura 23 kati ya 420 waliotakiwa kupiga Kura.
Rafiki yangu ambaye alikuwa Msimamizi tena ni Mwalimu, alisema katika kituo chake walifika Wapiga Kura 19 kati ya 300 waliotakiwa kufika.
Kituo kingine, mmoja wa Wasimamizi alisema eneo lake kulikuwepo na vituo vinne, vyote hakuna aliyemaliza kitabu kimoja cha Wapiga Kura, na hakuna ambaye alifikisha Wapiga Kura 20.
JE, HATA WANA-CCM WALIGOMA KUPIGA KURA?
Kilichoshangaza ni kuwa kama watu hawakujitokeza inamaanisha hata Wana-CCM nao hawakujitokeza?
Sasa ilikuwaje wagombea wa Ubunge, Udiwani, Urais wa CCM wakatangazwa na INEC kuwa wameshinda kwa kushindo?
Moja ya mambo niliyoshuhudia wakati wa zoezi la kupiga kura ni; ilipofika Saa Nane Mchana, Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Wilaya wakishirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri, walianza kupiga simu katika kila kituo kwenye maeneo yao kwa Wasimamizi wa Vituo wakiulizia hali ya upigaji kura.
Walipoelezwa kuwa hali ni mbaya walianza kuwashinikiza wasimamizi wote kwenye vituo kujikusanya na kuanza kutiki karatasi za kura, walikuwa wanatiki kwa wagombea wote wa CCM kwa kuwa majina ya Wapiga Kura yalikuwepo, NIDA zao hata picha…
Mtoa taarifa mmoja msimamizi wa kituo kimoja katika Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu anasema “….Tulijikusanya na kuanza kutiki, ilikuwa ni lazima maana viongozi walitutaka kufanya hivyo kwa lazima, ukigoma unachukuliwa hatua na kutishiwa maisha au kutishiwa kutopewa posho…”
Anaongeza kuwa katika kituo chake Mgombea Urais wa chama tawala hakupata kura hata moja, wasimamizi wa kituo walitiki na kura zilipanda kutoka sifuri hadi 320.
Kuthibitisha hilo, kuna video nyingi ambazo zimesambaa zikiwaonesha Wasimamizi au Watu kadhaa wakijaza rundo la karatasi za Kura kwenye maboksi ya Kupiga Kura.
Pia, nilibaini kuwa mchezo huo ulikuwa unasimamiwa na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Viongozi wa Chama Wilaya na Mkoa pamoja na Mfumo wa chama.
Hali hiyo niliibaini wakati wa kutangaza matokeo, ilikuwa inawachukua muda wasimamizi kutangaza matokeo, kwani kulikuwa na vikao vizito vya ndani ambavyo viliwajumuisha Polisi pamoja na wawakilishi wa nafasi hizo nilizozitaja, baada ya hivyo vikao ndipo matokeo yalitangazwa.
Hakika naamini hii ni sehemu ndogo ya sura ya giza ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (The dark side of Tanzania General Election 2025) na jinsi Mawakala walivyosimamia shoo.
SADC: UCHAGUZI HAUKUWA WA HAKI
Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) nao ulitangaza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa 2025 haukukidhi viwango vya Kidemokrasia kutokana na vitisho vya viongozi wa upinzani, vikwazo vya uhuru na ukosefu wa uwazi wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.
Zaidi - SADC yasema Uchaguzi wa Tanzania uligubikwa na dosari - BBC News Swahili
Taasisi ya Thabo Mbeki ilipinga Uchaguzi
Taasisi ya Thabo Mbeki ambaye ni Rais wa zamani wa Afrika Kusini nayo ilionesha kupinga mchakato wa Uchaguzi ulivyokuwa na kugusia vurugu zilizosababisha mauaji ya Watu wengi.
Taasisi hiyo ilisema matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania hayakuakisi matakwa ya wananchi, na badala yake utawala uliopo umewekwa kwa watu kupitia mchanganyiko wa nguvu na ulaghai.
Zaidi soma: Taasisi ya Thabo Mbeki: Tanzania kwa sasa haina Serikali halali, maridhiano ya kweli yatapatikana kwa kukiri kipi hakikwenda sawa ili kirekebishwe
Bunge la Ulaya nalo likapinga.
Bunge la Ulaya, Novemba 27, 2025 lilijadili azimio linalohusiana na matukio ya Oktoba 29, 2025 siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi nchini Tanzania, haki za binadamu, ikiwemo kesi ya kiongozi wa upinzani, Tundu Lissu (CHADEMA).
Bunge hilo litapiga kura juu ya azimio la kutaka Tume ya Ulaya, EU kusitisha kuunga mkono moja kwa moja mamlaka ya Tanzania, kufuatia kile kilichotokea siku ya uchaguzi na baada ya baada ya uchaguzi: ukiukwaji wa haki za binadamu.
Pia soma: Rasmi, Bunge la Ulaya lapiga kura zote 539 za NDIYO kuzuia misaada Tanzania, wahusika wa kadhia ya Oktoba 29 kuwekewa vikwazo
Marekani yatoa neno
Mara kadhaa Ubalozi wa Marekani ulitoa taarifa zilizoonesha unashaka na kilichofanyika wakati wa Uchaguzi, ikiwemo kuhoji kuhusu Demokrasia, Haki za Binadamu, Uwajibikaji na Utawala Bora ndani ya Tanzania.