Can you revisit and Paraphrase your words in plain Swahili.
"Though it is a thin line between natural pride of heritage and illusions bound for almost Aryan-like "country supremacy", I choose to carefully tread it, on the side of anti-patriotism, at least in the divisive "We shall defeat you" almost evangelical exorcism, if not medieval crusade, presented here."
I real want to know because, In myopic translation you sound as if you are demanding that, we dont have right to challenge the authority leave alone telling it that we will go agains it and defeat it.The whole of the ruling class, including balozi wa nyumba 10 za CCM, are replaceable because they are not decendants of royal families. It also sounds as if you caught some phrases from Bible that insit every individual to adhere to the authority we have because it is from God?!!!!
If that is the case, then my Big Question is this authority came into being???
Didi they get it straight from HIM??
Did they, in particular time in the past, challenged, pushed to the limit and defeated other authorities??
Did God send them to challenge the authority?
After all, even royal families who rule and demend to hounered no matter what,spilled blood of many other opponent royal families and their followers to remain the only thug on the Throne.
CAn you paraphrase yor words for sake of UPEs?? Please.
Mkuu Madela,
Nilichosema hapo, ni kwamba, kwa kutumia minajili ya utaifa, mataifa huuzwa. Kauli za uzalendo na utaifa zisizo na mipango ya kutuweka sawa tujue itikadi na jinsi gani tutashinda vita hii inakuwa haina tofauti na kutuuzia mbuzi kwenye gunia, hatujui kama ni kanyaboya au ndio kitu kweli.Siku hizi kuna ufisadi hata katika kupambana na ufisadi, kwa hiyo inabidi tuwe makini tujue details za wito huu zikoje?
Muandishi anaposema "tuna" au "tuta" anawaongelea kina nani? Amepewa ruhusa yao? Anawakilisha mawazo yao? Au amejisikia kuwashwa kuandika tu akaamua kuandika vitu kutoka kichwani kama anavyoandika hekaya zake?
Hii "nchi yetu" anayoizungumzia ni nchi gani? Je ni Tanzania? au Tanganyika? maana kuna wengine hawataki Tanzania wanataka Tanganyika, kuna wengine hawataki Tanganyika wanataka Tanzania, wengine hawazitaki zote mbili wanataka East African Federation.Huu ni mfano tu wa kuonyesha kwamba hii miito iliyojaa kaulimbiu zisizojishikiza katika uwazi, na zilizojaa ubunifu wa kutumia maneno, zinaweza kuwa propaganda za kuamsha hisia zaidi kuliko za kuleta uelewa na kutaka kujenga hoja za msingi zinazoweza kutumika katika vita dhidi ya ufisadi.
Hayo maneno uliyoyakazia hapo juu, ingawa mimi si mkalimani mzuri, nasema, ingawa naelewa kwamba mstari unaotenganisha kujivunia asili ya mtu na maruweruwe yendayo kwenye utaifa unaokaribia u-Aryan wa kudai "nchi yangu ndiyo ya kwanza" ni mwembamba sana, nachagua kuupitia kwa uangalifu mkubwa, kwenye upande wa kupinga uzalendo, angalau kwa maana ile ya kugawanya ya "tutakushinda" kama vile walokole wanavyotoa mapepo, kama sio vita vya kidini vya kale, iliyoletwa hapa.
Nina hakika translation imeharibu zaidi badala ya kusaidia, if not in Russian Dostroyevsky is never the same.
Mimi sikatai hii vita dhidi ya mafisadi, ninachokataa ni haya mahubiri yaliyojaa cliche bila kuleta arguments na positions.Mahubiri kama haya yanafaa kuwachota watu hisia bila kukubaliana mnafanya nini, vipi, wapi, kwa kufuata mfumo gani, kwa wakati gani na kwa kutumia mkakati gani yataturudisha hapa bodini kila siku, wakati mafisadi wanafanya vitu vyao.
Ndiyo maana nayakataa mahubiri haya, nayaona kama hekaya za Mwanakijiji tu, tofauti ni kwamba kaacha kuongelea romance na kabadilisha tune kaweka siasa, lakini ukiangalia practicality unaona haipo.Hamna plan, hamna strategy, hamna organization, hamna plan B, hamna intellectual engagement, hamna facts, hamna figures, hamna timeline, ni story juu ya story juu ya story tu.
Na usiseme mimi nina mpango gani, hata kama mpango wangu ni kuikosoa mipango isiyo mipango na hivyo kuiboresha huu ni mpango murua tu.
Lazima tuwe na quality assesment miongoni mwetu kabla ya kuenda kuwavaa mafisadi.Vinginevyo itakuwa kama Rostam na waandishi wa habari wa kibongo katika press conference yake, aibu.