The devil’s bible (the codex gigas)

The devil’s bible (the codex gigas)

TexasR

Member
Joined
Jan 31, 2017
Posts
67
Reaction score
91
CODEX GIGAS au kwa kiswahili (kitabu kikubwa),ndio kitabu kikubwa Zaidi kuwahi kuandikwa duniani tangu medieval periods ( karne za kumi kumi).The codex Gigas kina ukubwa wa (urefu sm 92, upana sm 22) na uzito wa kilogramu 75.Kitabu hichi pia kinaitwa “Devil’s bible” au biblia ya shetani kutokana na historia yake ,Pia katikati mwa kitabu hiki cha maajabu kuna picha kubwa ya malaika wa zamani aliyetupwa yaani ibilisi na shetani ambayo inaongeza utata juu ya kitabu hichi kikongwe.

Kitabu hiki kiliundwa mwaka (karne ya 13) mwanzoni huko monastery of podlacize ndani ya mji ambao kwa sasa unaitwa CZECH REPUBLIC.

Ndani ya kitabu hichi kuna biblia ya kiitaliano (latino) inayoitwa VULGATE BIBLE ikiwa ndiyo biblia ya kwanza kwa lugha ya kiitaliano mwishoni mwa karne ya 4 ambayo baadae ndiyo ilikuwa kuwa biblia halisi ya kikatoliki. Vitabu vingine mashuhuri vilivyomo katika codex gigas ni pamoja na baadhi ya maandishi ya agano jipya na agano la kale la biblia ya wakristo wengine pamoja na medica books au vitabu vya uganga.

Baada ya miaka mingi kupita baada ya kuandikwa kitabu hiki,kilifika katika maktaba ya PRAGUE ambao ndiyo mji mkuu waCZECH,ambapo baada ya vita iliyoitwa “thirty years’ war”, maktaba hiyo iliharibiwa vibaya na vitabu vingi kupotea,pia na codex gigas nayo ilipata madhara lakini ilisalimika haikuweza kuungua baada ya mtu mmoja asiyejulikana kuibeba na kuitupia dirishani nje ya maktaba ambapo ilianguka juu ya mtu ambaye alikuwa amesimama chini ya maktaba hiyo na kumdhuru vibaya kwa sababu ya uzito wake.

Baada ya hapo biblia hii kubwa ilichukuliwa mpaka maktaba kuu ya mji wa Sweden huko Stockholm ambapo sio kila mtu anaruhusiwa kuiona.

Codex Gigas kimefanyiwa binding kwa mbao, pia karatasi zake au velum ambapo maandishi yameandikwa zimetokana na ngozi za punda wapatao 160 ambacho kina jumla ya page 320.Kwa sasa kitabu hiki kina page 310.

Mpaka sasa kuna maswali mengi juu ya karatasi 10 zilizopungua,huku ikiwa haijulikani ni nani au kwanini karatasi hizi hazipo huku wengine wakisema labda ziliungua siku ile ya moto maktaba nk.Maandishi ya kitabu hiki yameandikwa kwa mwandiko wa aina moja yakiwa na rangi za kijana, buluu, nyekundu na dhahabu.

Kitu kingine kinastaajabisha juu ya kitabu hiki ni picha mbili,moja ya mbingu na nyingine ya dunia wakati wa uumbaji.

HISTORIA YAKE (FROM LEGENDS)

Kutokana na kumbukumbu,codex gigas iliandikwa na HERMAN THE RECLUSE mjiniCZECH ambaye alikuwa ni MONK.Monk huyu inasemekana alikuwa amevunja(amefanya kosa) baadhi ya sharia zao za kimonk, hivyo alihukumiwa kifo kibaya cha adhabu kali kinachoitwa “walled up alive” yaani unajengewa kijumba chako kidogo sana ambacho hakina upenyo ,kisha unaingia kwa kusimama mpaka utakapokata roho.

kuepuka adhabu hiyo,monk huyu aliamua kutoa ahadi kwa wakubwa zake na miungu yao kua atatengeneza kitabu kimoja kikubwa kwa usiku mmoja ambacho kitakuwa na hekima yote ya dunia hii na kuwatukuza mamonks wote milele na Ili milele.

Alipoanza kufanya hiyo kazi,katikati ya usiku alianza kuona kuwa hawezi kuandika kitabu hicho akamaliza kwa usiku mmoja peke yake hivyo alihitaji msaada. Alifanya maombi maalumu sio kwa Mungu bali kwa Lucifer ama shetani ili amsaidie hiyo kazi. Legends zinasema Lucifer alikubali kumaliza hiyo kazi huku akitaka roho ya Herman kama shukrani kwake.Hivi ndivyo kitabu kilivyoandikwa na kuna sababu za msingi nyingi ambazo zinathibitisha kitabu hiki hakikuandikwa na mwandamu moja wapo hii hapa.

1. Kwa mahesabu ya wanasayansi wanasema kama kitabu hiki kingeandikwa na mwanadamu basi kingechukua Zaidi ya miaka 30 kukiandaa kutoka na umakini ambacho kinacho hiki kitabu,ikiwemo marembo mengi tena yasiyopishana hata kidogo.
 
Waroma ni wabishi sana,sijui wamelishwa nini huko vatikan,ni mawakala wa lucifer na ni lazima wakubali ili wapate wokovu,hicho kitabu pia nakala yake ipo vatikan...sijui tutumie lugha gani!wahubiri wanayo kazi kubwa mno.
 
Ndugu yangu hangaikia roho yako kwanza ujue itafika wapi siku ukifa. Ninyi ndio kama wale watu waliotaka kumpiga yule kahana mawe ati ni mdhambi sawa sisi wakatoriki ni mawakala wa rucifer. Je ww ni mwema sana? Hii nguvu unayotumia kuuongea ukatoriki ungetumia kwako kupunguza uzinzi
 
Usihukumu usije ukahukumiwa
 
Nilitarajia mkatoliki uje kwa nguvu hii,angalia usipotee ilhali unayo nafasi ya kupata maarifa ndugu yangu.
 
Kitabu hiki kiliundwa mwaka (karne ya 13) mwanzoni huko monastery of podlacize ndani ya mji ambao kwa sasa unaitwa CZECH REPUBLIC.[/QUOTE]

Kitabu huundwa au huandikwa?
Czech Republic(Jamhuri ya Czech) ni Nchi siyo mji.

Baada ya hapo biblia hii kubwa ilichukuliwa mpaka maktaba kuu ya mji wa Sweden huko Stockholm ambapo sio kila mtu anaruhusiwa kuiona.

ukisoma kwa utaratibu utagundua kwamba hizi taarifa zako ni uzushi uliotungwa rasmi kwa ajili ya kupumbaza watu na kudhalilisha jamii ya imani fulani dhiki ya nyingine.

Ni kweli kwa mujibu wa kitabu cha MITHALI unaonekana u mpumbavu Mimi nipoje kwani?
Siku gani?
Miyo ya wakina nani?
Itafunguliwa kutoka wapi?
Nani aliifunga?
Itafunguliwa na nani?
Tutaelewa nini?
Nimeamini ukiona mtu anaimba wimbo mbaya ujue hana mzuri wa kuuimba,nikujibu kwa kifupi tu kama itasaidia lakini
1:uko hivyo(namna unavyojibu nk)kwa sababu bado unaamini hicho unachokiamini(na napata shaka ni 'Yesu' yupi uliyempokea kwa mujibu wa maelezo yako flani humu jf,kama ni 'Yesu' wa huko upande uliko basi kazi unayo...mkimbie huyu aliyetajwa kwenye 2wathesalonike 2:3-4....Ukishakaa mbali na huyo baas maswali yako yote hapo juu yatajibiwa,la vinginevyo tutakesha hapa mkuu.
 
Waroma ni wabishi sana,sijui wamelishwa nini huko vatikan,ni mawakala wa lucifer na ni lazima wakubali ili wapate wokovu,hicho kitabu pia nakala yake ipo vatikan...sijui tutumie lugha gani!wahubiri wanayo kazi kubwa mno.

Umeambiwa kimeandikwa na Monk halafu wewe unawashambulia Wakatoliki. Na Pia nani alikuambia nakala yake ipo Vatican?
 
Waroma ni wabishi sana,sijui wamelishwa nini huko vatikan,ni mawakala wa lucifer na ni lazima wakubali ili wapate wokovu,hicho kitabu pia nakala yake ipo vatikan...sijui tutumie lugha gani!wahubiri wanayo kazi kubwa mno.
Mkuu

Naomba msaada wako,kama unajua zaidi kuhusu hii codex
 
Ujinga wa walokole ni kudhani wana tikiti ya mbinguni mkononi.Ukisoma tu hiyo biblia yenyewe waongofu wote hawakujihesabia haki.Kujihesabia haki ni ufarisayo na wengi wa hawa jamaa zangu ni mafarisayo bila kujijua.Mngejua Mungu ni mtakatifu kiasi gani ungeililia nafsi yako.Hao wakatoliki unaowasema ndio waliokusanya hicho kitabu na kukitunza kwa uaminifu kabisa mpaka nawe ukajua kuna Mungu na kuna kitabu chake.Maelezo ya mtoa mada yanajichanganya ni vipi mtu aliyeishi karne ya 13anasibishwe na kitabu cha karne ya nne?Maelezo yangekuwa:Alinakili kitabu cha warumi cha karne ya nne na kukiingiza kwenye kitabu chake.Hii ingeeleweka.Kumbuka hupati wokovu kwa kuwachukia wengine.Mwalimu Gamaliel alisema "Ikiwa jambo hili ni la wanadamu litakufa tu ila ikiwa ni Mungu hatuwezi kuzuia."We unazungumzia kanisa lenye zaidi ya miaka 2000 na kufananisha na la kwako hilo lenye miaka nane na akifa mchungaji kanisa hakuna.Acha kuongelea mafundisho usiyoyajua kamwe
 
Mkuu

Nashindwa kuelewa haya,naomba msaada

1.what is bible,and why gigas codes it is so dubbed?

2.why codex imefichwa,na monks wanajua hilo kua kuna fella wao aliandika kitabu?
 
Back
Top Bottom