Acha unafiki! Tangu lini Kikwete akashine!? 😕 Kwa kipi hasa alichokifanya mpaka akashine!? Ufisadi umenshinda maana mafisadi ndiyo waliombeba hadi akaingia Ikulu anawaogopa kupita kiasi maana anajua wanajua yaliyofanyika hadi akaingia Ikulu. Ahadi zake za "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana" "Nitaipitia upya mikataba ya uchimbaji wa madini yetu" na "Ari mpya nguvu mpya na kasi mpya" zote ni bure kabisa hakuna hata moja aliyofanikisha. Sasa ni lipi aliloshine? Haya makubaliano na CUF kama tunaweza kuita hivyo ni usanii tu wa kuelekea 2010. Miaka 4 tangu aingie madarakani hajafanya chochote ili kufikia muafaka sasa miezi 11 kabla ya uchaguzi tunaambiwa kuna makubaliano, baada ya uchaguzi wa 2010 mkishaiba kura tena Zenj kama kawaida yenu ugomvi unarudi pale pale. Kweli Bravo Kikwete chaguo la mafisadi!
kwa kuisisitiza hii hoja yako , na kwa faida ya wengine, haya mazungumzo ya seif na karume hayana msaada wowote kutoka kwa kikwete. huyo kikwete mwenyewe yamemuacha akiwa kashangaa mdomo wazi,hajui yalikuwaje. na kuna asilimia kubwa kwamba kikwete hayafurahii haya mazungumzo anajifanya kuyapongeza kindumilakwili tu. kwahiyo huyo nchimbij aache kumfagilia kikwete kwenye jambo ambalo hakushiriki wala kuhusika.