The Economist na Mauongo Yao Kuihusu Tanzania: Waidanganya Dunia Tuna Torture Wakimbizi! Wanapata Faida Gani? Kwanini Tunanyamazia Uongo Huu?

MAYALLA PASCHAL huko chamwino list ya watu 23 ishatangazwa, Wewe vipi mkuu umeambulia chochote??
 
Ndugu yangu bandiko hili angepaswa kuliona Pascal Mayalla!!

Nikianza hilo la Wakimbizi kunyanyaswa sana, nadhani kila aliye timamu atakumbuka wakati fulani hata hapa JF tuliwahi kujadili hilo la Wakimbizi wa Burundi, na baada ya watu kupiga kelele sana, serikali ikahalalisha udhalimu wao kwa kutumia mwanya wa hicho hicho ulichosema... kwamba Wale ni Wahamiaji Haramu na sio Wakimbizi!

Dah! The burden of proof!!! Yaani sipati picha Uhamiaji wanavyotumia huyo mwanya kupiga pesa hata za Wakimbizi halali manake majority ya hao Wakimbizi sidhani kama wanaweza kutofautisha kati ya illegal na refugee!

Anyway, nilifuatilia sana hilo la Wakimbizi kutoka Syria hadi nikafikia kusema " a woman will always be a mother" huku nikimchukulia Angel Merkel jinsi alivyokuwa amewapambania Wakimbizi wa Syria ingawaje baadhi yao walikuwa wanaonesha ushenzi usiovumilika hata chembe!

Na moja ya mambo ambayo walinekera sana hawa Wakimbizi kutoka Syria ni pale vijana wawili au watatu (sikumbuki vizuri) walipombaka msichana mmoja huko ukimbizini!

Nikabaki kujiuliza, ikiwa Wazungu ambao kitamaduni na Waarabu ni kama mbingu na ardhi lakini bado wanawavumilia kwa sababu za kibinadamu, hivi watu kama sisi tunakosaje ubinadamu kwa watu ambao kimsingi "we're one and the same" almost in all aspects of life!! Yaani Wazungu ambao they've nothing to share culturally Arabs lakini ingawaje miongoni mwa hao Arabs ni total monsters wengi wao ni watu wema... kwanini tuhukumu wote at the cost of few monsters!!
 
Wakimbizi waliotendewa ukatili ni raia wa burundi na sio ambao wapo kwenye kambi ya wakimbizi kigoma, ukipata muda soma ile taarifa ya HRW unaweza kuelewa

Halafu kama haya hayana ukweli, serikalinyetu haijakanusha popote na haijajibu batua ya HRW ambayo imetaka wajibu hizo shutuma

La mwisho, ni kosa kumfukuza mkimbizi, ninachojiuliza ni kwa nini serikali ilikataa kuwapokea wakimbizi na mbaya zaidi jeshi letu limewatendea ukatili, kuna mambe mengi hapa ya kusikitisha na yanahitaji majibu na sio propaganda
 
Paskali ndugu yangu taharifa zako tunazo kuwa we ndio unatuma hizo article kwa mabeberu .take care
 
kwanini umeileta hiyo ripoti hapa?, Kua mzalendo kwa nchi yako ,ungeicha huko wala watu tusingeiona, hili jarida lina chuku na serekali yetu ila Raisi wetu Magufuli hatishiwi nyau na vijarida uchwara
 
Taifa linhitaji RECONCILIATION kwa matatizo yetu ya ndani kisiasa,wapinzania wamegeuzwa wkimbizi ndani ya nchi yao na wanatengwa bila ya kusikilizwa na kuhujumiwa kila kona.heri hao wakimbizi wao wanaye wa kuwasemea, Wapinzania ni kama yatima nchi hii.
 
Hili gazeti litakuwa linatumiwa na viongozi wa Chadema kuchafua taswira ya nchi yetu. Maana tokea aingie JPM madarakani na kufanya kazi nzuri,wanaisakama Tanzania. Na mengi wanayoandika yanaakisi kile wanachama na wafuasi wa Chadema huwa wanakisema dhidi ya taifa letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…