Huu ni muendelezo wa majadala ulioanza mwishoni mwa mwaka jana. Unakumbuka wakati ule Benki Kuu ilitangaza kwa wateja wote wa mavenki kwamba wanapaswa kufanya mambo Fulani,na wakati ule,nikaandika something negative kuhusu Benki,ndipo ndugu mmoja hapa akaniuliza,kama hutaki watu waweke hela benki,unataka wafanye nini? Nikasema nitaeleza baadae. Mwaka ulipoanza ameniuliza,mwaka mpya ndio huu,mbona bado hujatoa maelezo?
Kwa hiyo nimeitayarisha hii makala,kwa sababu hili swala la pesa ndiyo the heart of the matter,ili kuelewa mambo yanayoendelea sasa. Unakwenda Benki,unapewa makaratasi mengi,yanaitwa mkopo,baadaye,ukishindwa kulipa,wanakuja watu kukunyang'anya nyumba yako[foreclosure].