dolevaby
JF-Expert Member
- Aug 25, 2013
- 12,958
- 9,516
Povu at workHadithi yako inatufundisha nini? Au ndio ramli yenyewe na dua la MWEWE halimpati KUKU
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Povu at workHadithi yako inatufundisha nini? Au ndio ramli yenyewe na dua la MWEWE halimpati KUKU
Rwanda, Burundi na Congo Zaire zilitawaliwa na wabeligium.RwaMfan rwanda
Congo Burundi
Ndio dawa yao na wao inabidi kuwachenjia tuwaliyemuweka pia akawa dikteta hatari..hakung'ooka tu miaka ys 70..angesingiziwa kula watu na yeye
jiwe jiandaehabari zenu wana jf
bila kupoteza muda twede sambamba kumsoma huyu jamaa.
Safari ya Jean-Bedele Bokasa ilanza vibaya ikaisha vibaya .
Kwanza alikua yatima katika umri mdogo akawa mku wa majeshi akawa raisi wa nchi ,akala, akanywa akaoa,akafukuza,akatesa,akaua,akapinduliwa,akakimbia nnchi akarud akafungwa akaachiwa akafa ni mzee wa miaka 75 tena lofa.
ikumbukwe akiwa na miaka 6 alishuhudia baba yake akipingwa mpka kufa na wakoloni wiki moja badae mama yake alijiua.
mwaka 1927 ulikua mwaka wa shetani kwa bokasa hataivyo hakufa moyo alifurukuta mpka kuibukia jeshi la ufaransa na kupigana vita ya pili ya dunia.
mwaka 1962 alirudi nyumbani baada ya kuitwa na cousin wake David dacko ili wajenge nchi yeye akaharibu nnchi .
Tar. 1 Januari 1966 Bokassa akampindua rais Dacko na kumsweka ndani miaka 3 hakumuua akajitangaza kuwa rais mpya akafuta katiba ya nchi. Bokassa alisaidiwa mara kadhaa na Ufaransa. Mwaka 1967 aliomba na kupata msaada wa wanajeshi Wafaransa ili apate kuimarisha utawala wake.
Bokasa akaingia mjengoni kunywa, kula,kuoa na kuzaa alioa wanawake 17 na watoto zaidi ya 50 achilia mbali wale wa michepukoni alikua na kila sampuli ya wanawake mchina,mgerman,Sweedish,mtunisia,mromania,mvietinam,mlebanoni nawengineo siwajui alimaliza mabucha yote kumbe nyama ni ileile mpka mabinti wa kizungu walizaa na bokasa.
Safari za kila Siku kwenda kwa wake zake zilisumbua sana mji tena kwa foleni ndefu wakezake waliishi mbali mbali.
Bokasa alikua mwizi na muuaji lakini hakupenda wengine waibe aliamuru wezi wakatwe masikio na mikono wakati mwingine walipigwa nyundo kichwani huku akishuhidia kifo chao.aliua wanafunzi wote walio shindwa kununua uniform kwa dola 100 tena zilizoshonwa na mkewake kipindi hicho pato la mtu wa kawaida lilikuwa ni dola 150 kwa mwaka apo hata mimi angeniua.
April 1926 alimchinja waziri wake Alexandri banza kwa tuhuma za kutaka kumpindua bokasa mwenyew alimfunga kamba na kumchinja kwa kisu badae askari walichua mwili wa waziri na kuuzungusha jeshin kama fundisho
Septemba 1976 Bokassa aliachia serikali yake akaanzisha "Halmashauri ya Mapinduzi ya Afrika ya Kati": 4 Desemba 1976 akatangaza jamhuri kuwa milki na weyewe kuwa Kaisari kwa mfano wa Napoleoni. Bokassa alirudi katika kanisa katoliki, akawaalika wageni wengi na katika sherehe iliyogharamia dollar milioni 30 akajiwekea taji la Kaisari "Bokassa I".
Serikali yake iliendelea kuwa ya kidikteta. Wapinzani waliuawa hovyo au kupotea magerezani.
Ufaransa iliendelea kumsaidia.
Wakati wa Januara na Aprili 1979 wanafunzi waliandamana. Upinzani huu ulikandamizwa kwa msaada wa jeshi la Kongo. Wanafunzi wengi walikamatwa wengine kupigwa sana na kuuawa. Kwa jumla ni wanafunzi na watoto zaidi ya 100 waliuawa.
Katika hali hii Bokassa alisafiri tena kwenda Libya. Wapinzani walichukua nafasi ya kumpindua Bokassa wakiongozwa na aliyewahi kuwa raisi David Dacko tar. 21 Septemba 1979. Milki ilifutwa na Jmahuri kurudishwa.
Bokassa alipewa hukumu ya mauti lakini hakuhudhuria kesi. Aliporudi mwaka 1986 alikamatwa na kuhukumiwa tena afe. Adhabu ilipunguzwa baadaye kuuwa miaka 20.
1993 aliachiwa gerezani na rais André Kolingba akaishi miaka kadhaa akafa 3 Novemba 1996 huko Bangui. Bokassa aliacha wake 17 na watoto 50.
huyo ndo bokada kwa ufupi .
ahsanten
Sent using Jamii Forums mobile app