The Finest: Mwana FA apata wakati mgumu

The Finest: Mwana FA apata wakati mgumu

Mdakuzi

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
4,294
Reaction score
6,872
Na Herieth Makwetta
Mwanamuziki Hamis Mwinyijuma, maarufu Mwana FA amepata wakati mgumu kwa kulazimishwa na mashabiki kutaja jina la Lady Jay Dee baada ya kuliruka jina hilo alipokuwa akiimba wimbo wa Mabinti ambao ndani yake kuna jina la Lady Jay Dee.
Tofauti na ilivyozoeleka katika wimbo wa Mabinti, kwa mara ya kwanza Mwana FA aliruka jina la mwanamuziki Lady Jay Dee 'Anaconda' hali iliyowafanya mashabiki wamtake arudie tena na kutenda haki.
Mwana FA alisita kwa muda na baadaye aliamua kuurudia wimbo huo na ilipofikia kipengele cha kumtaja Jide aliimba kwa kumtaja, hali iliyoufanya ukumbi ulipuke kwa shangwe na mashabiki kumtaka arudie tena na tena.
Kutokana na hilo FA aliamua kufunguka, "Tunaishi na watu hivyo lazima mtagongana, hata mapacha wanakosana na kusameheana, lakini wakati mwingine shida inawafanya mnapata," alisema Mwana FA.
Awali shoo ilitangazwa kuwa ingekuwa ya watu 400 tu. Lakini mpaka inafika saa nne kasoro usiku, muda uliotangazwa kuanzwa kwa shoo hiyo watu waliokuwa wamefika walikuwa 250 tu.
Saa nne kamili mwanamuziki Hamis Mwinyijuma, Mwana FA alikanyaga 'red carpet' akiwa na mbunifu wa mavazi Sheria Ngowi, na baada ya kuchukuliwa picha kadhaa alianza kuelekea nje ya ukumbi katika sehemu waliyosimama watu wakipata chakula na vinywaji, watu walizidi kufurika lakini kila aliyeingia alikuwa alwatan kidogo.
Waliendelea kuwasili mastaa na shoo inaanza mashabiki wanaanza kuingia ukumbini saa tano kamili baada ya kupata chakula na vinywaji nje, huku muziki wa taratibu ukipigwa na bendi ya muziki wa dansi ya Njenje.
Mashabiki wanaendelea kubadilishana mawazo mpaka inapotimu saa tano na robo usiku, ambapo Mwana FA anapanda jukwaani.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
Aibu kwa Mwana FA, japo ni miongoni wasanii wachache ninawakubali kazi zao ila kwa kumkana timu Anakonda ameniboa.

Nimetia mgomo kusikiliza nyimbo zake kwenye hard disk yangu hadi upepo utakapo poa.
maana nyimbo za zamani kama hawajui,Mimi na mabinti,bado niponipo,ingekua vipi,nyama choma naaa Siwezi kuzitupa kamwe.!!!
 
Hii ni aibu kwa waandaaji wake(Clauds Fm/Prime time) ambao wameharibu show nzima na taswira nzima ya mwanaFA.
Duh!!! Kumbe hata waliokuja kuhudhuria show ya mwanaFA walikuwa ni mashabiki wa Lady JD.
 
Hii ni mojawapo ya mazingira ninayoteseka kama mshabiki ,kiukweli wote wawili ni watu ninaowashabikia kwa sana!
 
Kwa jinsi jide alivyokubalika ni ngumu kumfunika.unaweza kumchukia jide kama jide lakini kazi zake ni ngumu kutozikubali..
 
Mwanafa anaharibu jina lake kwa kukubali kutumiwa na Clouds jina lake ni kubwa na kazi zake ni nzuri sasa sijui kwanini anishindwa kusimama yeye kama yeye mpaka akubali kutumiwa Jide ni kitu kingine ukijaribu kupambana nae bila sababu utaishia kupoteza mashabiki tu
 
Back
Top Bottom