Nenda pale Zanzibar uwaambie hayo ya wao kuwa Tanzania, kwanza huwa wanachukia sana na wanaishi kwa majungu kwamba mumewakoloni. Mnawajazia wanajeshi wengi zaidi ya raia...
Hebu fuata hii mada hapa
Zanzibar ni nchi, ila Tanganyika ni sehemu ya jamhuri ya muungano, Tanzania ipo wapi?
ZANZIBAR NI NCHI ILA TANGANYIKA NI SEHEMU YA JAMHURI WA MUUNGANO. TANZANIA IPO WAPI?
Katiba ya zanzanibar inaitambulisha zanzibar kama ni nchi, wananchi na viongozi wao wameapa kuilinda. Katiba ya muungano inasema zanzibar si nchi ila ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tuache ubabaishaj, zanzibar hawautaki muungano. wamejiandaa kwa kila kitu kuwa nchi.
Nimeishi zanzibar ndo mana ninaujasiri wa kusema haya.
Wana wizara zao zenye majukumu na majina tofauti na bara, (ie wizara ya elimu na mafunzo ya amali). majeshi yao (ingawa sisi tunaviita vikosi), mamlaka za mapato ZRB, (sio TRA),bendera yao ya Taifa, nembo ya utaifa yao, usajiri wa vyombo kama magari na vingine, vitambulisho vya utaifa, benk zao (kama benk ya ya wananchi wa Zanzibar), Mtanganyika haruhusiwi kuomba ajira zanzanzibar.
Kwenda lazima usachiwe kila kitu bandari ya dar na pia ukifika bandari yao. (vua hadi mikanda ya suruali na heren na vyote vya chuma), ukinunua electronic, kama computa na video screen, na vingine lazima ulipie ushuru mara mbili ZRB, na TRA. wana WIMBO wao wa taifa, TV na REDIO za bongo haziruhusiwi kule, utaikuta ZBC na CCTV tu. Rais na mawaziri wa Tanzania hawana mamlaka yoyote zanzanzibar, muundo wa serikal wa zanz ni tofaut kabisa na wa TZ,( ie makam wawili wa rais)
JAMANI
.! HIVI KWANINI TUSIUNGANE KWA PAMOJA KUIDAI TANGANYIKA YA BABU ZETU.
Tukumbuke wazazi wetu walimwaga damu, kuiipigania Tanganyika, hakuna
maana ya kuendelea kusherehekea uhuru wetu wa dec 9 kama tunashindwa kujipigania wenyewe. sisi tusipokuwa wazalendo nani atakuwa mzalendo, wazanzibar ni wazalendo ndo mana wanalipigania taifa lao.
SERIKALI TATU ZINAWEZEKANA.
Tuyapuuze maneno ya wanaotutisha kwa kutaka serikali mbili, kwanza
hakuna muungano wa serikali mbili zenye mamlaka kamili duniani. mfano mzuri, Rais wa USA (Barack Obama) anasimamia wizara tatu tu, yaan FEDHA, MAMBO YA NJE, na ULINZI, na anaongoza serikali kama
52 za marekani. kwani yeye anaish kwenye ardhi gani, pesa anapata wapi?
tusiwe na ubongo mdogo kiasi hicho.
KAZI KWETU
. KWAHERI
..!