Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,583
Sasa hapa utapata nafasi ya kuongea na watu walioishi na Nyerere na kwenda Ikulu na kumuomba tausi mmoja tumchukue tuende naye nyumbani, na Nyerere akalifikiria jambo hilo na kucheka.Mkuu uko detailed sana unachosema kinawezekana. Sikuishi kipindi chama kimeshika hatamu mambo mengi nimejufunza tuu. Kuna speech moja ya Nyerere sikuweza kuilewa kwa haraka. Nilipoona na hiki chenu tena kinanipa tabu kukielewa nika refer kwa kile cha Nyerere. However my assumption kuwa mli attend middle school was right.
Watu ambao tumempiga ngumi mtoto wa Mwinyi darasani, kwa sababu kaja na kuturingishia shilingi moja mpya yenye picha ya baba yake na wengine tulikuwa hatufagilii mtu kujifanya mtoto wa rais darasani, tukamwambia "kama baba yako rais ni huko huko nyumbani kwenu, hapa darasani, wote wanafunzi sawa, chukua ngumi hiyoo".
Na wala hatukufanywa kitu na Mwalimu yeyote.
Egalitarianism. Look that up if you do not know the meaning.
Hizo ndizo enzi hizo ninazosema Nyerere alijenga a semblance of a classless society.
Sasa ukimlaumu mzee wa watu kashatangulia mbele ya haki, ukimlaumu kwamba alitaka kuwa confuse elite class kwa Kiingereza, nitakuona humjui Nyerere. Kwa sababu Nyerere kiukweli kabisa alitaka kujenga a classless society. Kama alishindwa ni kwa sababu ya dynamics za kiuchumi na kisiasa, si kwa sababu ya kukosa nia.
Sasa nikiona unataka kumlaumu huyu babu - ambaye ana mengi sana ya kulaumiwa- kwa sababu ya kwamba alitaka ku confuse elite class, wakati yeye mwenyewe hakuamini katika elitism, nakuona hujamuelewa bado. Labda tuliokuwapo enzi zake tukueleweshe.
Leo mtoto wa kapuku akimpiga ngumi mtoto wa rais kama nilivyompiga mimi mtoto wa Mwinyi sijui itakuwaje!
Uzuri wa JF ni kwamba kuna vijana wanamsoma Nyerere kama legend aliyefariki na wengine tushamuomba Nyerere tuchukue tausi Ikulu tuwapeleke nyumbani wakati hatujui kwamba tausi ni nyara za taifa ambazo hazitakiwi kuchukuliwa nje ya mamlaka ya Ikulu.