The Greatest Man in Universe: Kijana mdogo aliyefanya makubwa na kuacha alama akiwa na umri mdogo

Pamoja na kuishi bila shari na mtu akasalitiwa na bwana Yuda Eskariote na wenzake wachache kisha Pilato akatoa hukumu ya akasulubiwa akafa kisha akapaa mbinguni

Mwandishi ni pepo au nani.

mbona humalizii maandiko.

Kwenye uzi wako unasema alikufa.;


hapa tena unasema alikufa then akapaa mbinguni,


SEMA WALIMSURUBISHA, AKAFA, AKAFUFUKA NA KUPAA MBINGUNI.


unakosea wapi nduguuuuu!
 
Mwandishi ni pepo au nani.

mbona humalizii maandiko.

Kwenye uzi wako unasema alikufa.;


hapa tena unasema alikufa then akapaa mbinguni,


SEMA WALIMSURUBISHA, AKAFA, AKAFUFUKA NA KUPAA MBINGUNI.


unakosea wapi nduguuuuu!
Huwezi kukosoa kwa hekima?
 
Huwezi kukosoa kwa hekima?
Ok sorry! Very sorry.


Ila mbona umeandika vizuri sana . Umekosa tu kitu hicho halafu hata unapowajibu wengine ni kama sio mtafiti kwa sababu ya kutokukamilisha nguzo za ujio wa Yesu Kristo.

Msingi mkubwa wa Yesu unapomuelezea ni muhimu kuaininisha alizaliwa sio kwa kawaida, alikufa sio kwa kawaida na alilifufuka na kicha akapaa mbinguni.

unajua unapomtaja Yesu (unataja ukombozi yaani Kuzaliwa,kufa na kufufuka kwake).
 
Upo sahihi kiongozi wangu.. nikiri hapa kua nimekosea kutotaja matendo matati haya makuu aliyoyafanya Kristo, lakini msingi wa mada hii ni kumzungumzia yesu yule ambae ni mtu. (To the matter of fact nimekosea kutitaja utatu huo )
 
Karma mimi nilikua namweliezea Yesu yule mwanadamu ila angalia watu walivyonipiga mawe.. sijui hawaelewi sentesi.. Mungu aliyejifanya mtu
 
Yesu aka Yeheshua au Joshua alikuwa msomi wa ngazi ya digrii ya juu sana. Licha kwamba alizaliwa kama binadamu mwingine Roho yake ilikuwa kamilifu, wanazuoni wa elimu ya nyota na tabiri (Mamajusi) kutoka mashariki ya mbali walitabiri uzaliwaji wake, ambao ndio waliwajulisha Wayahudi juu ya matajio ya kuzaliwa kwa Roho tukufu ya Yesu katika nchi ya wayahudi, walipitiliza pale waliposema atakuwa Mfalme kitu kilicho mchonganisha na Mtawala wa wayahudi wakati huo Helode, kumtambulisha kuwa atakuwa mfalme kwao haikuwa makosa kwani kwa tamaduni zao huko mashariki ya mbali huwa mwenye high spiritual attainment ndio alikuwa anakuwa kiongozi, waliona kuwa kwa ukuu wa utukufu wa Roho ya Yesu waliona alifaa hata kutawala dunia nzima, wasijue kuwa itaibua mtafaruki mkubwa kwenye utawala wa Helode mpaka kuibuka njama za kutaka kumuuwa. Helode aliwapa zawadi wampelekee mtoto Yesu ili baada aweze ku trace mahali alipo ili aje kumuuwa. Akitegemea kuwa wale Mamajusi baada ya kumuona na kumkabidhi zawadi wangerudi kwake na kumhabarisha alipo Mtoto Yesu.

Waligundua njama za Helode hivyo hawakurudi kwa Helode bali waliwataharisha wazazi wa mtoto Yesu na kuwashauri wamtoroshe, lakini pia walingia makubaliano na wazazi kuwa Yesu anahitaji kuelimishwa na wao juu ya kusuduo au sababu za kuzaliwa wake, hivyo wamtaka Joseph, awapelekee mtoto pindi afikapo umri wa kwenda shule na wao watamsomesha bure katika chuo chao. Yesu akiwa mtoto alitoroshewa Misri, baada ya kifo Helode walirudi na kama ilivyokuwa kwa taratibu za wayahudi mtoto alipelekwa kusomea dini ya kiebrania kwa ma Rabi (kama ilivyo kwa waisilamu mtoto huenda Madrasa). Yesu alikuwa muelewa kiasi cha kuwabishia walimu wake. Alipofika miaka 12 historia inonyesha Yesu alitoweka na kurudi tena akiwa na miaka 30 akiwa na elimu ( spiritual knowledge ya ngazi ya juu ya kimashariki) ambayo ilipingana kabisa na ile ya Kiebrania. Alishindwa hata kuhudumu kwenye Masinagogi, alifundisha vitu vilivyopingana na mila na desturi za kiyahudi, waliokuwa wanaishi kwa kufuata amri kumi za Mungu walizopewa na Nabii Musa.

Mapingano ya Mafundisho yake na Mafalisayo na Makuhani yaliopelekea kuwa kama muhaini;-

1. Kwenye Amri kumi kuna amri inayotoa katazo la kutokuitaja jina la Mungu, Yesu alijitanabaisha kuwa yeye ni Mwana wa Mungu. Haikuwaingia akilini kuwa mtoto waokuwa wanamuona akimsadia baba yake kama selemala msaidizi eti baada kutoweka kwa muda na kurudi ghafla anajimwambafai kuwa ni mwana wa Mungu wanapaswa kumuheshimu na kumuogopa, kwanza walimchukulia kama mtu aliyechanganyikiwa na kuwa ni kichaa wakamdharau.

2. Wakati kuna katazo la kutofanya kazi yeye alitenda matendo ya uponyaji siku ya sabato.

3. Aliweza fanyafujo mahekaluni kama kupindua meza na kuwatawanya waumini mahali wao walipatambua kuwa ni patakatifu.

4. Katika makutano na mafundisho yake hakuwa na mfumo Dume. Wayahudi wanaamini dhambi imeletwa na Eva(Hawa) hivyo mwanamke alitengwa hata kwenye ibada, au jumuishi mbalimbali, hakusikilizwa na hakutakiwa hata kutoa mchango wake wa mawazo, wanawake walitengwa kabisa na ukikuta myahudi anaongea na mwanamke basi ujue ni ndugu yake yaani mkewe, dada, shangazi au binamu. Yesu hakufanya hivyo alikuwa huru kuongea na mwamke yeyote. Kumbuka alivyokutwa akiongea na yule mwanamke msamaria pale kisimani wanafunzi wake walishituka. Alikuwa na wanafunzi wanawake pia kama Mary Magdalene ambaye inasemekana alikuwa mke wake.

5. Hakuwa mbaguzi, wayahudi walijiona ni taifa teule hivyo wakuwa wanajitenga na makabila mengine, katika wanafunzi wake kulikuna wengine wasio wayahudi.

6. Yesu alidharau sheria na mila kandamizi za kiyahudi, kama kupiga mwanamke aliyefumaniwa mawe hadi kufa na au lazima ya kufanya tohala. Licha ya yeye kufanyiwa tohala akiwa kachanga, aishasikika akiwaambia wayahudi waliotaka kusibitisha kuwa tohala ina umuhimu gani kwenye mila yao, aliwaambia kama tohala ingelikuwa kitu muhimu na lazima sana basi Baba yangu yaani Mungu angewatahili mkiwa mimba tumboni mwa mama zenu kitu ambacho kilikuwa ni kama dharau kwa wayahudi.

7. Uwezo wa kufanya miujiza na mafundisho yake kufuata njia ya uzima wa milele yaliwavutia sana watu, mpaka makuhani walipungukiwa kabisa waumini na sadaka kupungua lakini pia Yesu alikuwa kama mamlaka ya rufani, akiyapinga na kuyapa changamoto maaumuzi mengi waliofanywa wanasheria (mafalisayo) watu walipenda kupata second opinion kutoka kwa Yesu. Hivyo akasabisha mkanganyiko wa hatari ya watu waliozoea kujiona muhimu kudharauliwa yaani Makuhani, Mafalisayo na Watoza ushuru, na kupelekea kuonekana ni muhaini. Akajengewa mashitaka kwa watawala na kuamriwa kuhukumiwa kwa kosa la uhaini na kupata adhabu ya juu.

Kwahiyo sio kweli kwamba yesu alikuwa hana elimu, pia familia yake haikuwa masikini, umasikini ulikwisha siku alipozaliwa kutokana za zawadi kutoka kwa Mamajusi na Helode. Kumbuka zawadi kuubwakati huo ilikuwa vipande vya dhahabu.

Hongera kwa kupenda kujielimisha kweni mengi umeongea karibu na ukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante sana mkuu...
Maelezo yako yako bomba sana..Hongera
 
You categorized jesus as a MAN?
He was a Man with God's Spirit that why he was referred God as His Father. And He as Son of God. Creation is the Game where God pray by Himself following rules set by God Himself.

Ili aje Dunian kwa Mwanadamu basi itabidi aache utukufu wake azaliwe kama mwanadamu na anapitia yote ayapitiayo mwanadamu haijalishi umungu wake, iliatimize yale yaliyomleta hutanguliza watao mwongoza ili at point in time apate God realization au ajitambue.

Kwa hiyo mtoa maada hakuwa amekosea, walioishi nae walimuona ni binadamu wa kawaida wenye mitazamo tofauti, kuna waliomthamini na walimdharau na kumdhihaki pia. Kwani kimwili hakutofautiana nao alikuwa na mahitaji sawa na wao. Iko dhana ya kutaka kumtukuza kimwili ambayo ni potofu, utukufu wake ni wa kiroho, mwili hauwezi kuwa mtukufu kwani unamapungufu, ni Roho tuu ukiondoa unafsi inaweza kukamilika na kuweza pata Umoja mtakatifu (Oneness) na kuwa na Mungu kwa Mungu. Rohoni unakuwa ( to be) wakati mwili unaishi wakati fulani kwa muda fulani, hauwezi kuwa mahala pote wakati wowote. Mwili uko limited in time with space.

Kwa kuwa alikuwa mwilini basi alikuwa limited na time na space na hivyo hakuwa perfect so he was a person.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hukukosea kujiita msafiri lazaro.. you so smart mam. Hongera
 
Nimekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…