Kitambi chakufutia tachi
JF-Expert Member
- Jun 16, 2019
- 1,063
- 2,566
Sio bandiko tu hadi comment nimesoma ndio maana nikaandika hicho nilichokiandika.Umesoma bandiko lote...?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio bandiko tu hadi comment nimesoma ndio maana nikaandika hicho nilichokiandika.Umesoma bandiko lote...?
Mleta mada unasema umri wako ni miaka 20 kama ni kweli basi Mungu atakuwa amekujalia kipawa fulani. Ninachojua vijana wengi wa umri Kama wako wamejikita kwenye mambo ya kipuuzi tu . Mambo yasiyowasadia hata kidogo. Wengi wao wako kwenye vibanda wakibenti mechi za ligi za Ulaya.
Wengi wao hawana uwezo wa kusoma hata makala fupi yenye aya 10 kumi tu.
Wengi wao wake kwa waume wanashinda wakitazama thamthlia za Korea na India bila hata kuelewa maudhui ya senema hizo.
Katika umri huu mdogo ulio nao nani kakufundisha maarifa haya yote?
Nani kakupa hii hekima?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani wewe ulisema maada ubishane?Sang'udi Otorong'ong'o mtu wenu huyu hapa mm siwez bishana nae
Haya umeyatoa wapi?.Roho ya Uokozi hurudi duniani pale maovu yakiongezeka utakatifu na utukufu wa mungu ukipungua. Kabla ya kuwa Roho hiyo kuzaliwa kuwa Yesu ilizaliwa kabla Uhindini miaka 2000 kabla yaa 4000BC, akijulikana kama Krishna, kumbuka wale mamajusi watatu waliojua tabiri uzao wake kwa kufuata nyota na kuitambulisha Dunia kuwa mwokozi atazaliwa walikuwa wakijua kuwa Roho ya Krishna imezaliwa, kwa kufuata position ya nyota ikawaepeleka kufika Israel, na kwa makubaliano maalumu na Joseph, walimuonya kuhusu njama za Mfalme Herode za kutaka kumuawa, na pia kwamba wao kama wajuzi wa masuala ya kiroho (spiritality) walipaswa kumtambulisha na kumuandaa ili ayakabiri majukumu yake, walimchukaa Israel akiwa na miaka 12 kumsomesha kwenye chuo ya elimu ya uumbaji ( kiroho), nyota na utabiri, na alirudi Israel akiwa na miaka 30 akiwa Enlighten being akitegemea kuwa atawakuta waisraeli wakiwa na shauku ya kumjua mungu wa kweli, akakuta kinyume na matarajio yake, waisrael walishikilia imani yao na tamaduni zao, hakuweza hata kuhutubu kwenye Sinagogi, akabidi ahutubu nje kwenye hadhala za wazi, muda mfupi alipata wafuasi wengi ambao wengi walienda kuhakiki mahubiri ya makuhani na sheria za mafalisayo, kwa umahili na uhodari wake watu wengi walimfuata, lakini wengine kwa kujua historia yake kuwa ni mtoto wa Yusufu (Joseph) fundi selemara walimdharau. Lakini kwa uwingi wa wafuasi, na miujiza aliyoifanya, alijijengea uadui mkubwa na Makuhani na Mafalisayo kwa zaka na sadaka zilipungua. Pia alionyosha wazi kutokufuata amri kumi za torati ambazo ndio ilikuwa sheria kuu ( katiba), kama kuto tii Sabato, kutengua Jino kwa jino badala yake alitaka wasameeane, kutofuata mfumo dume, kuchanganya mkusanyiko wa wanawake kwa wanaume, kutoa mafundisho bila kubagua ( alikuwa na wanafunzi wayahudi na wasio wayahudi, alikuwa na wanafunzi wanawake kwa wanaume), alioa mwanamke ambaye hakuchakuguliwa au kati ya binamu zake. ( Aliishi na Marry Magdalane yule kahaba alitaka pigwa mawe) ndio alikuwa kiongozi na best ya wanafunzi wake. Pia kitendo cha kujitamka hadhalani kuwa yeye ni mwana wa Mungu na Mfalme wa Mbinguni kinyume na moja ya amri kumi " kuwa usilitamke bure ya jina la bwana mungu wako...." hiyo ilipelekewa kufanya Uhaini na kushitakiwa na kupatwa makosa na kuhukumiwa kifo.
Sent using Jamii Forums mobile app
kasome tena hilo andiko na pia hilo bandiko hapo juu ni toleo la ngapi na mwaka gani maana huyu jamaa aliye andika hii kitu #1 alimuweka nabii muhammad (pbuh).Shakespeare or Edward de Vere
vitabu vyingine walifungia chapati shule vikapotea ndio maana ikaletwa quran kitabu kinachowaweka watu wasio kuwa na bahati ya kukisoma mashakani kwani kinatoa ule ujinga uliokuwa nao kama reality yako na kukupa reality mpya na pure.Tusaidie kurani inasema vitabu vilivyotelemshwa Kuna torati,zaburi ,injili na kurani.
Kurani tunaiona.Hivyo vitabu Vingine viko wapi? Waislamu tuonyesheni
Kwa hio Muhammad ni famous kuliko Yesu?kasome tena hilo andiko na pia hilo bandiko hapo juu ni toleo la ngapi na mwaka gani maana huyu jamaa aliye andika hii kitu #1 alimuweka nabii muhammad (pbuh).
Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuelewa sana mkubwa DA'VinciSalute
Mnamo mwaka wa 4BC jijini Galilaya katika kitongoji kiitwacho Nazareth kulikuwa na familia ya Bw. Joseph na mkewe Maria; walipata mtoto wa kiume wakamwita Jina Yeheshua au Yesu.
Ilikua ni moja ya kaya ya kimaskini, Bw. Joseph alikua anajishughulisha na shughuli za uchakataji wa mbao yaani useremala pia mkewe Bi. Maria alikuwa anajihusisha na shughuli ndogo ndogo za mikono. Yesu alifundishwa kusoma na kuandika tu maana wazazi wake hawakuweza kumudu gharama za kumpeleka shule zaidi, lakini alisoma pia masomo ya dini kwa walimu wa kiebrania waitwao “Rabi”. Kijana huyu alikuwa akisaidiana na baba yake kufanya shughuli za uchakataji mbao.
Alipotimiza miaka 30 kijana huyu ndio nyota yake ya mafanikio ilipoanza kung’aa, alianza kazi zake za kufundisha watu kama “Rabi” mambo mbalimbali yahusiyo falsafa ya maisha. Alifundisha kwa muda wa miaka mitatu tu, so alipokua na miaka 33 alifariki dunia kwa kuwambwa msalabani na dola ya Rumi iliyokua inatawala nchi nyingi kipindi hicho.
Kosa lake lilikua ni uhaini kwa kujiita mfalme wakati nchi hiyo ilikuwa ina mtawala ambaye ni Herode na Gavana Pilato wakiwa chini ya mtawala Kaisari Tiberius, pia kuweka maandamano yasiyo na kibali.
Japo aliishi miaka 33 na kufanya kazi yake kama rabi kwa mmuda wa miaka 3 aliweza kufanya mengi makubwa ambapo mpaka leo hii ulimwengu hautamsahau kamwe. Japo kafariki takribani miaka 2000 iliyopita lakini kila siku wafuasi wake wanazidi kuongezeka, hapo zamani kulikuwa na watu mashuhuri na maarufu wengi sana waliofanya mambo mengi kama vile Mose, Imhotep, Caesar Augustus, Archimedes, Pharaoh Rammiress II, Socrates, Spartacus, Leonidas, Plato, Alexander the Great, Aristottle, Ibrahim, Nebucadnezar na wengineo wengi. Lakini kijana mdogo sana ndani ya miaka mitatu tu aliweza kuvunja rekodi za watuwote hao mashuhuli na kubaki yeye ndiyo kinara.
Miaka imepita lakini mpaka leo hakuna mtu ambaye ameweza kuvunja rekodi yake, anafahamika kama mwanafalsafa, mtabiri na mwanasayansi nguli aliyewahi kuishi na hatokuja kutokea kama yeye.
Vitabu vyenye mafundisho yake ndio vinaongoza kuuza kuliko vyote, ni binaadamu ambae jina lake linazidi kukua kila siku badala ya kufifia japo ni miaka 2000 imepita. Wafuasi wake wengi wamekuja kuwa ni watu mashuhuri na wanafalsafa wakubwa kama vile Paulo, Thomas aquinus, Francis of Assis, Ignatus Luyola, St Luke, Francis Xvery, John Paul II, nk.
Kaacha miongozo ambayo ilikuja kutengeneza taasisi kubwa yenye nguvu na washirika wengi ambayo ni Catholics. Inaonyesha watu wengi mashuhuri duniani wamepita kwenye taasisi hii au ni wafuasi wa mafundisho ya huyu kijana mdogo. Yeye ndiyo binaadamu zaidi maarufu ulimwenguni. Kaacha historia ambayo haiwezi vunjwa maisha yote maana jina lake limeshindwa kufutika. Hebu fikiria kama alifanya mambo yake kwa muda wa miaka 33 tu ila umaarufu wake unazidi kukua na wafuasi wanazidi kuongezeka siku baada ya siku.
Wakuu mimi kiukweli namuonea sana wivu huyu kijana, haiwezekani kwa muda wa miaka 20+ niliyoishi hapa duniani sijawahi kufanyiwa Happy birthday, sidhani kama kuna mtu mwingine tofauti na mama anayekumbuka siku yangu ya kuzaliwa. Lakini kijana mdogo aliyekufa miaka mingi sana iliyopita karibia dunia nzima wanajua siku ya kuzaliwa kwake na hua wanasherhekea nyumbani huwa wanapika wali kabisa na kuchinja yule mbuzi mnene tuliemchunga muda mrefu halafu mimi first born kwenye kumbukumbu yangu ya kuzaliwa sijawahi pewa hata andazi.
Kinachoniumiza zaidi najua siku nikifa tu watu watanisahau mara tu baada ya kutandua msiba wangu, sitakumbukwa na yoyote kama yesu tunavyomkumbuka labda nyie wa huku JF mtanikumbuka kwa posts zangu.
Kiukweli mimi sikubali, kwanini Yesu atushinde watu wote wakati alikuwa binadamu sawa kama sisi? Tunakosea wapi? Kweli tumeshindwa kuvunja rekodi zake nasi basi tukumbukwe hata kwa muda wa miaka 10? Lakini je, huyu kijana mdogo alifanyaje hadi akaweza kufanya mambo makubwa yote haya ndani ya muda mdogo?
Maneno yote huko juu ni kuonyesha jinsi huyu kijana alivyoweza fanaya mambo mengi ndani ya muda mchache lakini kubwa la msingi ni kujua je aliwezaje? Alitumia nini?
Yesu aliwezaje?
Ukichunguza utajua kabisa huyu mtu alikuwa ana vitu anafanya ili kutimiza mipango yake hiyo yenye matokeo makubwa. Yesu alitumia vitu vitatu ili kufanya yote hayo. Kwanza kabisa alikua anajtambua (nilishaliongelea hili), pili alikuwa anafahamu kusudi lake (nitaliongelea hili panapo majaliwa) tatu alijali muda kuliko kitu chochote. Yes! Hapa ndiyo kwenye kiini cha mada yetu; Time Management. Jinsi nidhamu nzuri ya matumizi ya muda inaweza kukuletea mafanikio makubwa.
Japo Yesu hakuwa na elimu kubwa lakini alijitambua na alitambua kusudi lake mapema mno ndiyo maana alitumia muda wake vizuri sana akaweza kufanya mambo mengi makubwa. Alithamini muda wake alifanya kazi yake kwa nidhamu ya hali ya juu muda ukiwa ndio silaha yake kuu.
Kuna mtu aliwahi muuliza The Godfather Mwl. Julius Nyerere kwamba anawezaje kufanya mambo mengi kama vile kuhudhuria vikao, kuwa na familia yake, kuandika vitabu na makala kwenye magazeti, kuongoza nchi, kufanya ziara n.k kwa wakati mmoja? Nyerere alisema yeye anaheshimu muda. Muda wa kula anakula tu, muda wa kikako anakua kikaoni, kutembea anatembea tu, muda wa kulala analala tu n.k n.k
Najua humu wengi wetu hili ni ngumu sana. Unakuta mtu yupo anatembea kwenda mahali fulani lakini muda huohuo anasimama kuchat, muda wa kulala yeye anasoma kitabu, muda wa kusoma yeye anakula, muda wa kula ndiyo kwanza anaanza kuongea na simu, muda wa kazi yeye anaingia JF, muda wa kutafuta watoto yeye anapiga stori na mwenzi wake.
In short, muda hatuuthamini hasa huku kwetu Afrika, ndiyo maana Wachina wanatuendesha sana na tunaona kuwa wanatunyayasa huko makazini maana wao wamekulia kwenye malezi ya kufanya kitu kutokana na muda unaruhusu kufanya nini, sasa ile silka yao wakiileta huku twaona hawa watu wapo kama mashetani.
Kijana amka jali muda wako ulionao. Kwani nyie wenzangu hamumuonei wivu huyo jamaa huko juu aliyefanya mambo mengi ndani ya muda mfupi? Moja kati ya utajiri mkubwa binaadamu alionao ni muda.
Kama umefanikiwa kuwa na leo basi wewe ni tajiri mkubwa, leo hii ndio muda wako amka ukafanye yale unayotamani kufanya. Usisubiri kesho, kesho haipo siku zote ipo leo tu! Achana na kupoteza muda wako kwa kwenda location kupiga picha za kupost Facebook upate like 300, unadhani siku ukifa kuna mtu atakukumbuka kwa kuacha picha zenye like nyingi na quality nzuri huko FB? Sahau hili.
Yesu alijitambua mapema ndiyo maana aliweza fanya mambo makubwa, jitambue kijana mwenzangu hautakumbukwa kwa kuweza kutaja kikosi kizima kinachocheza ligi daraja la tatu huko Italy au England. Tumia muda wako huu ulionao leo kwa kufanya mambo yatakayoacha alama isiyofutika hapa duniani.
Huyo ndio Yesu the Greatest man, hakuna mtu mwingine kama yeye, hakuna atakayeweza kuvunja rekodi zake alizoacha sana tunaweza fuata matendo yake ili kufanya mambo makubwa kwenye maisha ila kumpita tuache legacy kubwa kuliko yeye haitawezekana kamwe.
Tujali muda jamani, ipo siku tutajutia huu muda tuanaopoteza kufuatilia mwanamke mmoja miezi sita halafu kila siku unatumia zaidi ya masaa 4 kuwasiliana nae wakati muda huo ungefanya mambo mengi ya msingi ndani ya miezi hiyo 6 yakamfanya huyo mwanamke akajileta mwenyewe.
Utajiri wetu mkubwa sisi watoto wa maskini ambao tunaweza kuutumia kupunguza kiwango cha umaskini kwenye familia zetu kama Yesu alivyofanya kwenye familia yetu ni MUDA. Jali muda utakutunza uzeeni.
JE WEWE BINAFSI NI NANI UNAONA NI GREATEST MAN ALIYEFANYA VITU VIKUBWA AMBAE TWAWEZA KUJIFUNZA KUPITIA YEYE?
Ahsanteni.
Like & Share
Da’Vinci
El maestro.
Kumeibuka watu wengi wakidai Yesu hakuwahi kuwepo,ni stori tu za kutunga,tena wanadai na ushahidi kbs stori ya maisha ya Yesu ni ya kukopi kutoka kwa watangulizi wake km Osiris,Buddha na Krishna.Mmojawapo wa watu wanadai hivyo ni former pastor Ray Hagins.Salute

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Sang'udi Otorong'ong'o mtu wenu huyu hapa mm siwez bishana nae
Alizaliwa kwenye HORI na siyo HOLI kama uoivyosemaUongo mtupu ulioandika Maria na Joseph hawakuwa Kaya maskini.
Wote walikuwa ukoo wa kifalme .Ukoo wa Mfalme Daudi..Kasome mathayo sura ya kwanza.Koo za kifalme hazijawahi kuwa Kaya maskini miaka hiyo Hadi Leo hii
Maselemala Sio watu maskini.Nenda keko dar es salaam kaangalie maselemala waliopo pale Wana magari ya mamilioni nyumba za uhakika na huuza funiture zao Hadi nje ya nchi.Aliyekuambia selemala ni mtu maskini Ni Nani?
Hata Yesu alizaliwa kwenye Holi la ng"ombe Sio sababu familia ya Joseph walikuwa Kaya maskini Bali sababu nyumba ya wageni ilikuwa imejaa.Pesa za kulipia walikuwa nazo
Na Jesus hawezi kuwa ni Yesu!Abuu Dharr,
Issa sio Yesu
Lete ushahidi. Tatizo ni namna watu wanavyomchikulia as if alikuwa anaonekana special na ali behave kitakatifu. Kama ingelikuwa hivyo basi asinge sulubiwa na kukataliwa.Hao walikua ni watoto wa Joseph sio maria
Yesu kafufuka jana mkuu.. unasemaje juu ya hiloLete ushahidi. Tatizo ni namna watu wanavyomchikulia as if alikuwa anaonekana special na ali behave kitakatifu. Kama ingelikuwa hivyo basi asinge sulubiwa na kukataliwa.
Utakatifu ulikuwa ni wakiroho sio mwili.
Kufufuka ni pale Roho inpata enlightenment.Yesu kafufuka jana mkuu.. unasemaje juu ya hilo
Umefanya tafiti kwa kutumia source gani? Uliuliza watu au ulifanyaje Huo utafiti unataka kuniambia google wamekosea utafiti wao hila ww wa tandale kwa mtogole umepatia wakati google wapo dunia nzima na wana resources za kutosha kufanya utafiti ww Huo utafiti umefanya mtaani kwenu ndio uandike universe ungeandika greatest man wa Hapo mtaani kwenu sawa Hawa ndio wana resources za kufanya research hyo Kwako kawadanganye mtaani KwakoMkuu mm nimeleta tafiti yangu hapa je kwanini nawe usilete hapa hayo uliyoyaona huko