pale wachambuzi wa taarabu wanapovamia fani ya mpira
teh teh teh teh teh
Achana na Messi Pele hamkumuona mnamsifia
kipindi hicho mtu anamiaka 50 anacheza mpira
refa anaingia na suti uwanjani huku ameshika fimbo
Off side hakuna hebu vuta picha Messi angefunga magoli mangapi
Ha ha ha ha ha ha ha hii ya Offside kutokuwepo ndo ilikuwa balaa, yaani mtu anavizia anavyotaka. Sasa atashindwa kuwa na Magoli 1,000.pale wachambuzi wa taarabu wanapovamia fani ya mpira
teh teh teh teh teh
Achana na Messi Pele hamkumuona mnamsifia
kipindi hicho mtu anamiaka 50 anacheza mpira
refa anaingia na suti uwanjani huku ameshika fimbo
Off side hakuna hebu vuta picha Messi angefunga magoli mangapi
usimsahau Codoba na kitasa Cambiaso....hapo bado kuna kibabu Zanetti
"Ronaldo is the hardest attacker I've ever had to face. He was impossible to stop." - Alessandro Nesta.
Nesta katika ubora wake...
Chifu, huwezi kusema kitu bila kutukana? Siyo ustaarabu katika jukwaa la michezo. Kama humkubali mchezaji fulani, basi potezea tu.
Allesandro Nesta, beki bora zaidi kuwahi kutokea duniani baada ya Franco 'Piscinin' Baresi
Nessi alikutana na Nesta 'Babu' hakumkuta Nesta akiwa kwenye peak na bado andunje hakufurukuta.
Please msimfananishe Ronaldo 'El Phenomenon' na haka kaandunje, it's the greatest crime in football
Unachozungumza mkuu ndicho kweli... Messi ni kiumbe wa ajabu ktk soka, bila kujali umbile lake mambo anayoyafanya ni hatari.. Wanamtukana sana tena kwa kumuita NeSSI!??? Sisi tukimgusa 'nabii' wanalalama.
Best all time defender....Nesta
Best all time defensive partnership ....Nesta na Maldini
'Pascinin' namkubali mno....Headmaster
Of course katika forwards watano Duniani, andunje hawezi kukosa lakini mshambuliaji bora kati ya Ronaldo de Lima na Messi, Ronaldo atashinda hicho kinyang'anyiro kila siku.
Simchukii andunje na nikutaarifu tu mimi ni Juventini, sio kila anayem challenge Nessi basi ni Madrid, punguza kukariri
Sijui ni nani anaweza kucheza soka la ulaya bila kuwa na nguvu na speed, simjui kwa kweli.
Hawa kina nessi na christina wanatamba kipindi ambacho washambuliaji wamekua vimungu mtu uwanjani, wakiguswa tu faulo, kadi n.k tena huyo christina ndio kabisaa, akiguswa kidogo anaruka kama kapigwa kombora, credit to Messi though, hardly kumuona andunje akifanya simulation
But what about the art of defending in modern football, ambayo ndio inabeba theme ya hii thread? Siku hizi mabeki wanaogopa hata kufanya tackling kwa sababu kina christina wanaweza kugalagala uwanjani kama wamepigwa na kiguruneti bana? Sheria za siku hizi zinazidi kuwabeba washambuliaji na kuwakandamiza mabeki, hata tuzo siku hizi ni kwa ajili ya forwards tu, enzi hizo kulikua na msemo "Strikers win games, defenders and goalkeepers win championships."
Hahahaha, unajua jamaa nikiwawekea Video, hata hawaangalii.
Kama wangeliangalia na wakumbuke kuwa enzi Pele anacheza, mpira ulikuwa mzito na viatu vibaya, ndiyo atajua nini maana ya Pele kuitwa KING. Ukiangalia hii Video, kuna style nyingi ambazo Neymar na C Ronaldho wanazicheza leo hii.
Hii ya kupiga watu matobo, Neymar anajaribu tu ila Messi na Ronaldho wa Brazil ndiyo walizi-copy haswa. Check 2:50
Hatari ya kukabiriana na king Leo
Heshima ya pele ni ya kupikwa na wale mafioso wanaitwa Fifa, wanaoua the beautiful game
Maradona alionyesha uungu wake uwanjani, hakusubiri kutengenezewa video za animation wala fake status na mafioso
Eti king ambaye alishindwa hata kucheza soka Ulaya, pele is overrated
Kuna siku waandishi wa habari walikua wameenda kuangalia mazoezi ya Italy wc 2006 ile kufika wakamuona mtu ananawa amelowesha nywele zake wakauliza kwa kushangaa khaa hadi wanawake wanacheza mpira pamoja na wanaume
Akaambiwa yule unayemuona anaitwa Alesandro Nesta akiwa katika ubora wake na nywele zake za siha nyeusi
Huyu jamaa nuksi kishenzi beki wangu huyu
Ronaldinho Gaucho ndo huwa namuona hero of all time in football.
Pele kakaa kwao tu na wala hajatoka nje, kipindi ambacho pele anacheza sidhani kama kulikuwa na msisimko wa mpira kama sasa.
Wachezaji wanajulia mpira wakiwa wakubwa na wanapata namba.
Hii ni tofauti na sasa, mtu akiwa na miaka 10 anafundishwa soka la darasani na vitendo kabisa kisha akikua anaingia uwanjani.
Sasa Pele yeye alikuwa anawaburuza vibabu tuu.
Hili la kutocheza Ulaya..Wakati Pele yuko Santos walikua tishio Dunia Nzima alikua hana haja ya kwenda Ulaya..Gap limekuja baada ya timu nyingi za Amerika Kusini kuyumba kiuchumi.
Na Maradona alienda Ulaya kwanza kusaka Maisha wakati huo Boca walikua hawana ela kiasi icho kama alizo ahidiwa akienda Ulaya..
kwa io ichi kigezo cha Ulaya inabid mkifikirie mara mbili.
Vizuri umeona jambo la hawa mafioso wa Fifa kutupikia masuperstar na kutuaminisha kwamba they are the greatest ever..
Namuangalia mtu kama Zidane jinsi Fifa ilivyompika na Media zao kumfanya jamaa aonekane the best midfielder of the game wakati ukifuatilia technically jamaa sidhani kama he has ever been better than Pirlo, Iniesta and Ronaldinho..