Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijui umetembea kiasi gani duniani. Ila ungelikuwa umtembea sana na kuona heshima anayopewa PELE hadi leo, ndiyo ungelijua huyu kweli ni KING. Wengi walibisha kama wewe hadi yalipowakuta.
Romario alikuwa akiamini kuwa yeye ndiyo zaidi. Siku moja akiwa kwenye mataa, akawekewa bastola dirishani mwa gari, akashusha kioo na jamaa kuchungulia wakamuona PELE, wakamsalimia na kuwaambia waende. Next time wakamsimamisha tena na alikuwa peke yake, gari ikaenda.
Muangalie kipande kidogo tu kwenye hii Video ujuwe maana ya AUTO-PASS yaani jinsi ya kujipigia pass mwenyewe.
Just start from 1:00 min.
sijatembea sana, kiasi tu kuniwezesha kuwa na judgement yangu mwenyewe bila kuangalia wangapi wanaikubali ama wanaipinga, + napenda kusimama mwenyewe, sio na crowd. pia nimetembea vya kutosha kuniwezesha kutopagawa na compiled videos zilizopo kwenye mitandao.
Kama nilivyosema mwanzo, naheshimu mtazamo wako, ila ntabaki na wangu.
heshima ya pele ni ya kupikwa na wale mafioso wanaitwa fifa, wanaoua the beautiful game maradona alionyesha uungu wake uwanjani, hakusubiri kutengenezewa video za animation wala fake status na mafioso
eti king ambaye alishindwa hata kucheza soka ulaya, pele is overrated
Angalia video hiyo juu: https://www.youtube.com/watch?v=953rOfQ8Y0w
Kuanzia dakika ya kwanza na njoo tuongee. Angalia style mbili ambazo Raul aliyekuwa Real Madrid alikuwa akicheza, zilianza na Pele. Hizi Pass wanacheza Barcelona hado leo, Pele aliziansha zamani sana na wanaziita Auto-Pass.
Naona mpaka magoli ya animation ya Pele, namwona jamaa anasukumana tu na kudandiana na watu na magoli kama ya Stoke City.
Unasema Pele anaheshima Duniani, Maradona kuna watu walianzisha dhehebu la kumwabudu Dios, heshima hata Lunyamila anayo, what's heshima bana!
Hahahaha, unajua jamaa nikiwawekea Video, hata hawaangalii.
Kama wangeliangalia na wakumbuke kuwa enzi Pele anacheza, mpira ulikuwa mzito na viatu vibaya, ndiyo atajua nini maana ya Pele kuitwa KING. Ukiangalia hii Video, kuna style nyingi ambazo Neymar na C Ronaldho wanazicheza leo hii.
Hii ya kupiga watu matobo, Neymar anajaribu tu ila Messi na Ronaldho wa Brazil ndiyo walizi-copy haswa. Check 2:50
pasi wanazocheza Barcelona ni pasi za kawaida ambazo mchezaji yoyote anapiga.
Tofauti ni kwamba mfumo wanaocheza ndo unaona zile pasi kama zina utofauti ila hazina utofauti wowote ule.
kitu ambacho naweza kusema ni kwamba wewe ushabiki wa Pele umezidi mipaka.
Pele kaanza tu kufanya hivyo vitu kwa kuwa yeye kaanza kucheza mpira kabla ya wengine.
Hata Maradona angeweza fanya kama angekuwa kabla ya Pele.
Mkuu Nzi heshima yakooooo... Nimeona hilo tusi aseeeh,, teh teh teh teh...
Asa mkuu cheki watu walivotukana na kuonyesha dharau za hali ya juu,,
Eti Ronaldo de Lima ni hatari na ni bora zaidi ya mfalme wa kabumbu ulimwenguni.. Blaza PELE!???
Hivi nyie mnaosema PELE hakua na skills ndani ya soka mnauhakika!?? Hapa hanidanganyi Mtu kwa sababu nimeona Pele akifanya yake ktk dimba kupitia mikanda ya video tangu nikiwa mdogo.. Mzee wangu ilikua akikerwa na Mtu huchukua kanda hizo na kuangalia ufalme halisi.. Kwa uhakika Ronaldo de Lima hamfikii Pele hata robo.
Eti mnasema Ronaldo ana skills kuliko MFALME PELE.. ZIPI HIZO!?? NARUDIA ZIPI HIZO... Au mnazuzuka na ule mkasi wa mguu m1 aliokua anaupiga!?? Nasema Hivi De Lima hana skills zozote za kumzidi MFALME PELE,,ILA Ronaldo ana lijua lango vema, akabebwa na urefu na stamina tu...
Ronaldo hana kitu/hajui lolote mbele ya PELE.... HEEE KUMBE NIPO NJE YA MADA...
Jamani Nesta ni Hatari ktk defence.. Lakini kinachompa uzuri ni kujua kucheza na mpira lakini kama kukaba kuna njemba ni hatari zaidi yake...
Afu nyie mnaoleta mada za Messi acheni, kiumbe wa ajabu huyu.
Una AKILI SANA.
Heshima ya pele ni ya kupikwa na wale mafioso wanaitwa Fifa, wanaoua the beautiful game
Maradona alionyesha uungu wake uwanjani, hakusubiri kutengenezewa video za animation wala fake status na mafioso
Eti king ambaye alishindwa hata kucheza soka Ulaya, pele is overrated
pale wachambuzi wa taarabu wanapovamia fani ya mpirakweli kabisa mkuu, Messi hastahili kutajwa humu.
sijabahatika kumuangalia pele ila Ronaldo de Lima nimemuangalia.
Ronaldo de Lima analijua lango vibaya mnoooo, yaani jamaa akiwa hana mpira anajua kabisa akipata mpira basi anaenda kufunga sehemu flani. Alinikoshaga sana siku moja wakati anaingia Real Madrid, aliletewa mpira akatuliza kifuani kisha akageuka na mpira bila kumuangalia kipa, fastaa akapiga shuti la kudundisha mpira kwa chini kisha mpira ukaingia wavuni. De Lima akikaa na kipa basi una uhakika hapo kuna goli linaingia, alivyoenda AC Milan ndo kaenda kufa kabisaaa, kama Gaucho vileee.
Pele ni habari nyingine aisee ila hunishawishi pele mbele ya Maradona, Pamoja na De Lima kuwa bora ila pele ni bora kuliko yeye, pele alikuwa akikata misitu na kichambua watu mmoja baada ya mmoja na kwenda kufunga, kama Messi yaani.