The Igbo Apprenticeship System

Mtambachuo

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
1,907
Reaction score
3,560
Habari wana jamvi.

Twende kwenye Mada yetu,

Igbo ni kabila linalo patikana Kusini Mashariki mwa nchi ya Nigeria na nchi nyingine jirani. Kabila hili limesambaa nchi nzima ya Nigeria hasa kwenye majiji makubwa kama Lagos. Lakini sio hivyo tuu wamesambaa ulimwenguni pote wakifanya biashara.

Igbo ni kabila tajiri na lililo fanikiwa zaidi Afrika wana miliki biashara kubwa ndani na nje ya Afrika. Wana bidii sana ya kazi na ujanja wa mjini, Yani ni Smart guys. Wanafana kwa kiasi na Wakikuyu na Wachagga.

Pia ni kabila lenye akili zaidi Afrika yani wana akili za kuzaliwa sio za kukariri kariri, wakina Echukuemeka na wengine ndio wanaongoza kwenye mtihani ya kitaifa huko Nigeria. Mara nyingi ukisikia mtu mweusi kafanya maajabu kwenye vyuo vikubwa kama Havard mara nyingi wanakuwa ni hawa Igbo.

Hawa jamaa hata ukiwapeleka jangwani miaka michache utakuta Makasri na biashara nyingi hapo ndio maana jamii nyingi za kiafrika zina waonea wivu hawa watu na kuwapa kashfa mbaya mbaya kisa wamefanikiwa kuwazidi wao.

Sasa kilicho nifanya niandike uzi huu ni juu ya utaratibu wao wa Apprenticeship yani wana bebana sana na kurithishana spirit ya biashara ndiyo maana wao wana endelea kuwa wafanya biashara vizazi baada ya vizazi.

Ni kwamba mtu mwenye biashara yake ana mchukua kijana mdogo anaenda kufanya kazi kwake mara nyingi wana kuwa either mtoto, ndugu au jirani, kwa hiyo mzazi ndiye anaye mkabidhi, anafanya kazi ndani ya miaka 3 hadi 5 bila malipo sana sana zaidi ni anapata huduma za chakula, malazi na mengine ya lazima. Baada ya miaka hiyo 5 ya kufanya kazi kwa bidii kwenye mazingira ya biashara ndio anachwa kuwa huru na yeye ana anzisha biashara yake na mara nyingi wanapewa mitaji hapo alipkuwa anafanyia kazi.

Huu umekuwa ni utaratibu wao wa muda mrefu yani mtu anafanya kwa vitendo na ndio inafanya kabila hilo kufanikiwa kibiashara kwa sababu wana ujuzi mwingi na sio nadharia pekee.

Je utaratibu huu upo kwenye jamii gani hapa Tanzania.? Na unafaa kuigwa..?
 
Ni utaratibu mzuri, umasikini unatoweka haraka miongoni mwa jamii zenye mtindo huo. Hata wachaga na wapare wanabebana kidogo sana kulinganisha na waigbo
 
Bro siku ukienda vijijin kwa hawa watu masaki utapaona mbagala. Anambra cjui ambra State huko nina mshikaji nilikutana nae mila hiyo ya mapambano akaja kuwa mshikaji ni hatar na nusu. Sisi tubaki kulogana tu na uchawa
 
Watu wengine ni mkikuyu, mbochana, mtutsi, kuna kabisa lipo south Africa karibu na Namibia, baganda, na kabila la rais wa Congo DRC, msomali hasa kusheti, shona to mansion a few. Hawa watu ukikutana nao front ni nouma.
 
Ni utaratibu mzuri, umasikini unatoweka haraka miongoni mwa jamii zenye mtindo huo. Hata wachaga na wapare wanabebana kidogo sana kulinganisha na waigbo
Sana mkuu ni utaratibu mzuri jamii hizi mara nyingi hazina wivu zinabenana sana.
 
kwa mtu mwenye akili ya chungulia pale ataseme ni utumwa
Ndio kwa wavivu na wenye uelewa mdogo ila hawa Igbo wanafanya kazi kwa hao Master wao kwa bidii sana na kwa kiasi kikubwa anaona kama ni sehemu ya mmliki kwa hiyo mwisho wa siku anapata mtaji wake anaaza biashara yake.

Na familia ya kijana inakuwa haimsumbui huyo Master/ inampa support na kumueleza kijana wao awe na bidii na mwaminifu wa kazi mpaka Apprenticeship hiyo ikamilike. Yani wapo mbali sana wenzetu.
 
Watu wengine ni mkikuyu, mbochana, mtutsi, kuna kabisa lipo south Africa karibu na Namibia, baganda, na kabila la rais wa Congo DRC, msomali hasa kusheti, shona to mansion a few. Hawa watu ukikutana nao front ni nouma.
Aise safi sana naona una waelewa vizuri sana.
 
Bro siku ukienda vijijin kwa hawa watu masaki utapaona mbagala. Anambra cjui ambra State huko nina mshikaji nilikutana nae mila hiyo ya mapambano akaja kuwa mshikaji ni hatar na nusu. Sisi tubaki kulogana tu na uchawa
Anambra state na state nyingine zote za Igbo yaani mabilionea waliopo huko ni hatari na wana utaratibu wa kujenga kwao hata kama wapo mjini kuna mahekalu na makasri yakutosha.
 
Bro ni kwetu ila mi nakuambia huwafiki hata robo ya niliyoyakuta kwa hawa jamaa.
Yani huko ni habari nyingine hao watu wana bidii ya kazi na kunyanyuana wanabidii sana. Walipaswa wapate ile nchi yao ya Biafra.
 
Nawewe fanya kazi miaka mitano kwa malipo ya chakula tu. Mnasifia ujinga
Na wewe kukaa miaka mitano unabet na kuishi kwa shemeji yako ndio akili.

Anaishi kama nyumbani na mwisho wa siku anapewa mtaji wa kuanza biashara wewe unafikiri hao vijana wa Kichagga hapo Kariakoo walitoka Moshi na kuanza biashara moja kwa moja bila kupata ujuzi wa vitendo.

Biashara ya kwenye makaratasi ni tofauti na kufanya kwenye uhalisia wewe fikiri kijana aliye drop darasa la saba au form four akipitia hiyo system akifanya kwa miaka yake 3 akapata mtaji anafanya utamkuta wapi. Kupumbuka biashara sio kiasi kikubwa ina hitaji skills na ni kitu watu wengi hawana.
 
Unafahaa kuigwa na jamii zote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…