Ila kuna kauzembe flani hivi nimekaona
Baada ya kuchukua treble.
Haaland kacheza juzi na team yake ya taifa kafunga goli 2 ,lakin kwetu kashacheza game 4 ,0 goal...unataka kusema team ya taifa ina midifilder kama kdb ndio maana kafunga ? Jibu Ni hapana ...
Nawezasema tunawinger na no 10 wabinafsi wasiopenda kupiga pass kumtafuta Haaland ,MTU kama kdb alishasema kabisa yeye katika maisha yake ya mpira anapenda Sana assist kuliko kufunga ,ndio maana kupiga pass kwenye angle ngumu kumtafuta Haaland anafanya Bila wasiwasi ,.,.....
Ndio maana kdb akiwa uwanjan Haaland hatulii Ni chance after chance mpira unamfuata ,Ni yeye tu kutia kambani ....
Alavrez Ni mchezaji ambaye naweza Sema alitakiwa kucheza Namba ya kdb ,maana Ni mzuri kwenye freekick ,movement ,Kasi ,nguvu ,lakin ukimwangalia Kwa undani Zaidi Alvarez anacheza kama kumprove wrong pep kuwa yeye Ni Zaidi ya Haaland ,hivyo usije tegemea Mtu kam Alvarez kupiga penetration pass kumtafuta Haaland hata kwenye tight space ..
Foden ,doku , Grealish Hawa Ni winger ambao wanapenda ku dribble kuingia ndani cut-in na kama bado wanaenerg wanashot golin ,hivyo basi Ni ngumu mnoo kumpigia Haaland cross kumpa afunge ,harafu wote wanacheza kukaa kwenye score sheet kama vile wanajitafutia record zao badala ya kumpa Haaland mpira ....
Ukiangalia Hao wote Ni wachezaji waliotakiwa kutengeneza link up kubwa na Haaland ,Kwa sababu halaand Ni goal machine Kila MTU anajua ,Ni striker mkubwa anauzoefu na kucheza na CB kibao kama nafasi zipo ...
Mbaya Zaidi Foden ,doku , Grealish, Alvarez wanacheza kivyao ndio maana unaona mbele hakueleweki Kila MTU anajitafutia Namna ya kufunga ,mwisho WA siku wote wanaishia kubabaisha,Haaland anafanya movement mpira haufuki Hao Hao kina foden wakataka kufunga Hakuna space wanaishia kubutua butua tu ,mpaka rodri ndio huwa anaamua kupanda mbele kusaidia kuaamua baadhi ya game ....
Na rodri anapenda mbele kufanya hivyo Kwa team ambazo ziko na shambolic midifilder,team kubwa usijetegemea rodri kupanda juu Sana tutapigwa mvua ya magoli ....
Tunahitaji midifilder mwingine mwenye mentality kama ya kdb ya kuassit kuliko kufunga ,MTU kama Foden toka game ya Kwanza alionesha uchoyo hadharani Kwa Haaland mpaka watu wakaenda kwenye page yake Instagram kumtukana Foden "pass the fucking ball to Haaland" game inayofuata ndio Foden akawa anajitahidi kinyonge kumpa Haaland na kwenye IG akaja kuandika "finally I assisted you Haaland" so unaweza kuona jinsi tulivo na mawinga selfish ...
Mbaya zaiid Hao mawinga Bora wangekuwa finisher kama mahrez ila ndio hivo tunaishia kubabatiza ....
Game against Arsenal tunapiga shots 4 ,on target 1 ,wakati kdb akiwa uwanjan Ni chance after chance,Cross's kuingia kwenye box zinakuwa nyingi either mabeki wajifunge au Haaland afunge ,kdb anapiga cross Bila hata kuangalia anajua Haaland Ni mrefu kuanzia mwili na miguuu atafikia hata asipofikia hatachoka kumpigia ....lakin saizii tuko na watoto kina foden ,doku ,Grealish , Alvarez wanacheza na wao kutaka kuonekana kwenye score sheet ,Hakuna team work hopeless kabisa ...
Natamani hili pep alione lakin itakuwa too late ,now Haaland anaonekana kama kaflop kumbe kuna vijana wadogo wanacheza kujitafutia record zao , Haaland akishafunga team inakuwa imeshinda tayari ,ila ndio hivo wacha tusubili kdb ....