The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Mara ya mwisho kufungwa zaidi ya goli 1 ndani ya game 6 mfululizo ilikua mwaka 1963.

Mara ya mwisho kutupa taulo tukiwa tunaongoza goli 3-0 ilikua mwaka 1989.

We are in trouble.
 
Nimeona hapo juu baadhi ya member wakiulizana ilikuwaje ukaanza kuishabikia timu flani. Na zinazotajwa hapa ni chelsea, arsenal na city.
Iko hivi. Kwa mfano hapa bongo kwa sasa. Kwa miaka minne iliyopita Yanga ndio club iliyovuna mashabiki wengi kuliko club yoyote. Sababu kubwa kabisa ni kufanya vizuri kwa misimu hii minne. Kuwa mabingwa mfululizo. Kusajili wachezaji wenye vibe kama Mayele. Wote mtakumbuka Mayele ameingiza washabiki watoto kuipenda Yanga. Kwa stayle yake ya ushangiliaji.
Ukienda kule nje haswa PL. Nitazungumzia vilabu vi3 ambavyo vilikuwa vya kawaida kabisa.
1. Arsenal. Arsenal ndio club iliyokuwa ya kawaida ya kwanza kuzoa mashabiki wengi africa haswa baada ya ujio wa Digital setillite Television almaarufu DSTV.
Arseal ilianza kujizolea mashabiki barani africa kuanzia 1998 baada ya mzee wenger kumsajili Nwanko KANU ambaye alitokea kuwa kipenzi cha washabiki wa soka africa na duniani kote. Kanu alikiwasha kule marekani kwenye michezo ya olimpic iliyofanyika kule atalanta akiwa na kina Taribo West na kina Tijani Babangida. Wakati huo alikuwa akikipiga pale Ajax. Kanu ndio mtu aliyeitangaza Arsenal barani afrika kuliko mchezaji yoyote.
2. Chelsea. Ujio wa Tajiri wa Kirusi.,Abromovic. Chelsea ya wakati wa kabla ya Abromovic ilikuwa haifatiliwi sana na wapenda soka na haikuwa na washabiki na wapenzi kama ilivyo sasa. Lakinj baada ya kuja kwa Abromovic na kufanya mabadiliko makubwa, ya kimfumo. Kuanzia benchi la ufundi na idara nyingine. Ujio waJose Mourinho na drogba ndio kwa kiasi kikubwa kimeiongezea chelsea mashabiki huku africa.
3. City. Kila mtu anajua ukubwa wa kocha Joseph Pep Guandiola. Maada ya utangulizi ma makocha Mancini na yule jamaa wa chile ambaye kwa sasa yupo villareall ndio akaingia mwamba Guandiola. Aina ya soka linalochezwa pale ittihad ni soka la kupendeza na kuvutia. Hivyo ujio wa Guandiola ndio sababu kubwa ya kuongezeka kwa wapenzi na mashabikj wa city barani aftica.
Nakumbuka hata Mbwana Samata alipoenda Villa villa kwa hapa bongo ilianza kupata mashabiki na game za vila zilianza kuonyeshwa kwa wingi kwenye luninga za hapa bongo.
 
Mkuu, umeeleza vyema.

Sasa mtu ameshabikia arsenal ama Man U miaka ya 90 mpaka 2000's sababu ya mafanikio ya club, soka safi ama kwa kufata mkumbo wa marafiki, ndugu n.k anakuja kukushangaa mtu unayeshabikia City ama Chelsea leo hii kwa sababu hizohizo.
 
Mpaka sasa tuko nafasi ya 15, leo kuna timu zikishinda tunazidi kudidimia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…