Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, umeeleza vyema.Nimeona hapo juu baadhi ya member wakiulizana ilikuwaje ukaanza kuishabikia timu flani. Na zinazotajwa hapa ni chelsea, arsenal na city.
Iko hivi. Kwa mfano hapa bongo kwa sasa. Kwa miaka minne iliyopita Yanga ndio club iliyovuna mashabiki wengi kuliko club yoyote. Sababu kubwa kabisa ni kufanya vizuri kwa misimu hii minne. Kuwa mabingwa mfululizo. Kusajili wachezaji wenye vibe kama Mayele. Wote mtakumbuka Mayele ameingiza washabiki watoto kuipenda Yanga. Kwa stayle yake ya ushangiliaji.
Ukienda kule nje haswa PL. Nitazungumzia vilabu vi3 ambavyo vilikuwa vya kawaida kabisa.
1. Arsenal. Arsenal ndio club iliyokuwa ya kawaida ya kwanza kuzoa mashabiki wengi africa haswa baada ya ujio wa Digital setillite Television almaarufu DSTV.
Arseal ilianza kujizolea mashabiki barani africa kuanzia 1998 baada ya mzee wenger kumsajili Nwanko KANU ambaye alitokea kuwa kipenzi cha washabiki wa soka africa na duniani kote. Kanu alikiwasha kule marekani kwenye michezo ya olimpic iliyofanyika kule atalanta akiwa na kina Taribo West na kina Tijani Babangida. Wakati huo alikuwa akikipiga pale Ajax. Kanu ndio mtu aliyeitangaza Arsenal barani afrika kuliko mchezaji yoyote.
2. Chelsea. Ujio wa Tajiri wa Kirusi.,Abromovic. Chelsea ya wakati wa kabla ya Abromovic ilikuwa haifatiliwi sana na wapenda soka na haikuwa na washabiki na wapenzi kama ilivyo sasa. Lakinj baada ya kuja kwa Abromovic na kufanya mabadiliko makubwa, ya kimfumo. Kuanzia benchi la ufundi na idara nyingine. Ujio waJose Mourinho na drogba ndio kwa kiasi kikubwa kimeiongezea chelsea mashabiki huku africa.
3. City. Kila mtu anajua ukubwa wa kocha Joseph Pep Guandiola. Maada ya utangulizi ma makocha Mancini na yule jamaa wa chile ambaye kwa sasa yupo villareall ndio akaingia mwamba Guandiola. Aina ya soka linalochezwa pale ittihad ni soka la kupendeza na kuvutia. Hivyo ujio wa Guandiola ndio sababu kubwa ya kuongezeka kwa wapenzi na mashabikj wa city barani aftica.
Nakumbuka hata Mbwana Samata alipoenda Villa villa kwa hapa bongo ilianza kupata mashabiki na game za vila zilianza kuonyeshwa kwa wingi kwenye luninga za hapa bongo.
Anajikuna sana para Hilo, huko ndo kuchanganyikiwa kwenyewe.Manjesta shite
View attachment 3163122
Alikua anajikwaruza yeye mwenyewe.We unaona alifanyaje mpaka kupata hiyo mikwaruzo!?