Mimi naona City hawajapoteana sana kama watu wanavyosema, ninachoona City wana tabia ya kukubali pressure kirahisi kama timu yangu Nyumbu united, kujiamini kupo chini sana hasa wakiongoza goli au magoli au pressure ya aina yyte ile kama vile kushambuliwa na kukaliwa rohoni. Misimu iliyopita Man City hata umkalie rohoni atakuwa na utulivu wa Hali yuu na kurecover haraka.
Sasa basi watu wengi hawajui kuwa sifa hii ndiyo humpa Real Madrid ushindi kwasababu wale jamaa wanaweza wasicheze vizuri kabisa lakini wanakufunga kwasababu wanajua kuhandle ile presha na vichwani mwao wanajua tu hili litapita hivyo hata ukiwafunga unaona sura zao zilivyo Wala hawapaniki kabisa na wanacheza vile vile kama hujawafunga, Sasa hivyo man city ndo inatakiwa iwe hivyo.