The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Tetesi
NAPOLI YAMFUKUZIA KIUNGO WA CITY


Napoli itaanza upya jitihada za kumsajili kiungo wa Manchester City Oleksandr Zinchenko kwenye dirisha la uhamisho Januari, kwa mujibu wa TuttoMercatoWeb .
Zinchenko alijiunga na City mwaka 2016, lakini msimu uliopita alikuwa akitumika kwa mkopo PSV kabla ya kuivutia Napoli majira ya joto.
 
Tetesi
Manchester City itataka kumsajili beki wa kati wa West Brom na Ireland kaskazini Jonny Evans, 29, ama beki wa Real Sociedad Inigo Martinez mwezi Januari. (Telegraph)
 
TIMU ya Manchester City iliyokuja na mtindo wa kugawa dozi kwa kila timu ya Ligi Kuu ya England, Jumapili itakuwa ugenini kucheza na wenyeji Crystal Palace huku Arsenal wakitifuana na West Bromwich Albion.
Mpaka sasa Man City wanaongoza ligi wakiwa na pointi 58, tofauti ya pointi 15 dhidi ya Manchester United yenye pointi 43.

Crystal Palace mpaka sasa ina pointi 18 nafasi ya 16 kwenye msimamo.
 
Mechi za Ligi Kuu kesho Jumamosi

Man United vs Southampton,

Watford vs Swansea City,

New Castle United vs Brighton,

Liverpool vs Leicester City,

Huddersfield Town vs Bunley,

Chelsea vs Stoke City,

AFC Bournemouth vs Everton.

Man city vs Crystal Palace
 
Tetesi
Manchester City itampatia beki Nicolas Otamendi kandarasi mpya.Mchezaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 29 alitia kandarasi ya miaka 5 mwaka 2015(ESPN)
 
Mshambuliaji nyota wa Manchester City Gabriel Jesus atakuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na jeraha alilopata wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace Jumapili ambapo walitoka sare 0-0, meneja Pep Guardiola amesema.
Mbrazil huyo wa miaka 20 alionekana kuumia kwenye goti kipindi cha kwanza wakati wa mechi hiyo uwanjani Selhurst Park.
Aliondolewa uwanjani akitokwa na machozi.
Kiungo wao Kevin de Bruyne pia huenda akakosa kuwachezea kwa muda baada ya kuondoka uwanjani akiwa amebebwa kwa machela.
Mbelgiji huyo hata hivyo alionekana nje ya uwanja baada ya mechi, dalili kwamba huenda hakuumia sana.
"Nafikiri Gabriel atakuwa nje kwa mwezi mmoja hivi au siku chache zaidi, naye Kevin tutasubiri Jumatatu tujue iwapo aligongwa tu kidogo au ameumia sana," alisema Guardiola.

Ni lazima ukubali ukali na ugumu wa ukabaji Ligi ya Premia, lakini waamuzi wanahitaji kuwalinda wachezaji, hilo ndilo naomba pekee."
Jesus atakosa mechi dhidi ya Watford Jumane.
De Bruyne naye ambaye ameng'aa sana msimu huu na kusaidia ufungaji wa mabao tisa Ligi ya Premia msimu huu aliumia baada ya kukabiliwa na kiungo wa Palace Jason Puncheon.

Kuna mstari ambao unapouvuka inakuwa hatari," amesema Guardiola.
Palace walifikisha kikomo mkimbio wa kutoshindwa mechi 18 wa City, lakini walivuka mwaka wakiwa na alama 14 mbele kileleni.
Sergio Aguero ndiye mshambuliaji wao pekee aliye sawa, lakini Guardiola amekataa kuthibitisha taarifa kwamba wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez Januari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…