The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

The Manchester City (The Citizens) | Special Thread

Gundogan alifunga goli la kwanza kwa kichwa akiunganisha kona ya Leroy Sane dakika 14 baada ya wenyeji kuumiliki mpira dhidi ya Spurs na waliendelea kutawala mchezo.
Shuti la De Bruyne liliwavunja nguvu Spurs baada ya mpira kuzama wavuni na Sterling aliweka kimiani mara mbili kwa shuti la karibu baada ya kukosa goli la wazi kufuatia Gabriel Jesus kukosa penalti ambayo iligonga mwamba.

Chrstian Eriksen aliipatia Spurs goli la kufutia machozi dakika za mwisho lakini pengo lao dhidi ya vinara hao wa ligi limeongezeka hadi pointi 21.
City wameshawafunga mahasimu wao wote wa taji Ligi Kuu Uingereza msimu huu na mbio zao kuelekea ubingwa wa Uingereza zinaonekana kukosa mpizani.

Walifunga goli lao la kwanza kupitia nafasi yao ya pili, Baada ya Gundogan kuwahadaa mabeki wa Spurs na waliruhusu goli kirahisi mno kupitia Raheem Sterling aliyetupia goli la tatu.
Ukungu ulishuka kwenye uwanja wa Etihad lakini haukuweza kuwazuia City kufanya mambo yao na Hugo Lloris alilazimika kulinda lango hadi kwenda mapumziko wakiwa wa wamefungwa 1-0 tu, Kipa huyo wa Kifaransa aliokoa mara mbili kumzuia Gundogan kufunga goli la pili.

Harry Kane alipiga shuti bomba ambalo lili gonga mwamba Spurs walipotishia kufunga kwa mashambulizi ya kushtukiza, na Mshambuliaji huyo wa Uingereza alikaribia kufunga goli la kusawazisha alipomlazimu Ederson kujinyoosha kuokoa baada ya mapumziko.
Spurs waliongeza nguvu yao lakini mashambulizi ya kushtukiza yaliwagharimu pale De Bruyne alipoweka kimiani dakika ya 70.

Jan Vertonghen alimwangusha De Bruyne ndani ya boksi kwa penalti iliyokuwa dhahiri, lakini Jesus aliyeingia kutokea benchi alipiga mwamba kabla ya Sterling kujaribu kumalizia na kushindwa kwani mpira ulipaa juu.

Sterling alifuta makosa yake ya kukosa magoli ya wazi akiweka kimiani goli rahisi dakika ya 80, kabla ya kufunga jingine kwa kutumia makosa ya Eric Dier baada ya kumpiga tobo Lloris kuipatia City goli la nne.
Spurs wamefanywa zilichofanywa timu nyingine zote zilizotembelea Etihad msimu huu,na Eriksen hakushangilia alipofunga goli la kufutia machozi kwa Spurs dakika za mwisho.
 
Guardiola anasema beki wa kulia wa Manchester City Kyle Walker, 27, ni "mojawapo ya walio bora duniani" katika nafasi yake hivi sasa lakini ananuia kumfanya mchezaji huo wa timu ya kimataifa ya England kuwa bora zaidi. (Daily Express)
 
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola anasema "kamwe" hawaambii wachezaji wake wacheze fauli, kauli aliyomjibu kocha mpinzani wake wa Manchester United, Jose Mourinho aliyesema kuwa upande wake unacheza "fauli za kupangwa". (Guardian)
 
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola anasema "kamwe" hawaambii wachezaji wake wacheze fauli, kauli aliyomjibu kocha mpinzani wake wa Manchester United, Jose Mourinho aliyesema kuwa upande wake unacheza "fauli za kupangwa". (Guardian)
Asante kwa taarifa mkuu.
 
Manchester City watafanya mazungumzo na meneja wao Pep Guardiola kuhusu mkataba mpya majira yajayo ya joto huku wakiendeleza lengo lao la kuunda himaya ya soka itakayotishia ile ya Manchester United.
United walishinda mataji yao manane kati ya jumla ya 11 Ligi ya Premia wakiwa chini ya meneja wao wa Sir Alex Ferguson.
City wanataka kuiga ubabe kama huo.
Walilaza Tottenham 4-1 Jumamosi na kuendeleza mkimbio wao wa kushinda mechi mfululizo ligini hadi 16, na kusalia alama 11 mbele ya United kileleni.

Mkataba wa Guardiola wa sasa utamalizika 2019.
Guardiola, ambaye awali alikuwa mkufunzi Barcelona na Bayern Munich, aliteuliwa meneja wa City majira ya joto2016.
Msimu wa kwanza walimaliza wa tatu Ligi ya Premia lakini klabu hiyo iliendelea kuwa na imani naye.
 
Tetesi
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, amekataa mshahara wa £400,000 kila wiki kutoka kwa klabu moja ya China kwa sababu anataka sana kuhamia Manchester City. (Sun)
 
Tetesi
DE BRUYNE MBIONI KUSAINI MKATABA MPYA CITY


Kevin De Bruyne anakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu Manchester City, kwa mujibu wa BBC .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameibukia kuwa mmoja wa viungo bora katika ulimwengu wa soka akiiwezesha timu ya Guardiola kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwa pengo la alama 11.
 
Tetesi
DE BRUYNE MBIONI KUSAINI MKATABA MPYA CITY


Kevin De Bruyne anakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu Manchester City, kwa mujibu wa BBC .
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ameibukia kuwa mmoja wa viungo bora katika ulimwengu wa soka akiiwezesha timu ya Guardiola kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwa pengo la alama 11.
Asante kwa taarifa mkuu.
 
Ni miamba wa London Chelsea na Arsenal kukutana Kombe la Carabao nusu fainali hatua ya nne za mwisho.
Vinara wa Ligi Manchester City wataikabili Bristol City ya daraja la chini, ambao walifanikiwa kuinyuka Manchester United Jumatano.

Chelsea waliongoza kwa kiwango kikubwa mechi yao dhidi ya Bournemouth, lakini goli la dakika za majeruhi kutoka kwa Dan Gosling liliwalazimisha kucheza muda wa ziada, bali goli la dakika za majeruhi kutoka kwa Alvaro Morata liliwapa ushindi Blues kutinga nusu fainali.
Arsenal walikuwa na ahuweni zaidi kwani walishinda 1-0 bila taabu dhidi ya West Ham Jumanne.

Timu za hatua ya nusu fainali zitacheza mechi ya kwanza Januari 9 na 10 na mechi ya marudiano Januari 23 na 24.
Washindi watacheza fainali kwenye uwanja wa Wembley Februari 25.
 
Manchester City bado ina hamu ya kumsajili Alexis Sanchez lakini huenda ikalazimika kusubiri hadi dirisha la uhamisho litakapofunguliwa ili kujaribu kupata saini ya mshambuliaji huyo wa Arsenal.
Jaribio la City kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 lilikubaliwa katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho mwezi Agosti lakini mpango huo ukashindwa kufua dafu.
Mkufunzi wa klabu hiyo Pep Guardiola tayari amefanya mazungumzo na usimamizi wa klabu hiyo kuhusu wachezaji anaolenga katika kipindi cha miezi 18.

Kuna hofu kwamba kumsajili Sanchez mnamo mwezi Januari kunaweza kuharibu mpangilio wa kikosi cha Guardiola .
Inaaminika kwamba City inadhani kwamba Arsenal inaamini kwamba kuendelea kumlazimisha mchezaji huyo kusalia katika klabu hiyo ni makosa na kwamba iko tayari kufanya biashara mwezi ujao.
Hatahivyo, huku kikosi cha Guardiola kikiwa na pointi 11 juu ya jedwali la ligi, kuna hisia kwamba ujio wa Sanchez unaweza kuvuruga kikosi hicho.
 
Tetesi
Arsenal na Manchester City zinamkagua beki wa Burnley James Tarkowski, 25, kwa lengo la kumvutia katika dirisha la uhamisho la mwezi ujao.(Times - subscription required)
 
Tetesi
Kiungo wa kati wa Barcelona na Hispania Sergio Busquets, yupo kwenye rada za Manchster City kwa dau la Paundi milioni 50 na Yaya Toure. (Daily Star)
 
Yeyesi
Mshambuliaji wa Nice Mario Balotelli,27, anataka kuhamia timu kubwa na ameichagua Manchester City kwa uhamisho wa bure. (Daily Mirror)
 
Tetesi
Manchester City wanaangalia hali ya mambo ya mlinzi wa AC Milani Leonardo Bonucci mwenye miaka 30 ambaye inasemekana hana raha katika klabu hiyo.(Gazzetta dello Sport - in Italian)
 
Tetesi
Manchester City wanaangalia hali ya mambo ya mlinzi wa AC Milani Leonardo Bonucci mwenye miaka 30 ambaye inasemekana hana raha katika klabu hiyo.(Gazzetta dello Sport - in Italian)
Asante kwa taarifa.
 
Back
Top Bottom